Freelancer
JF-Expert Member
- Sep 22, 2008
- 2,965
- 2,141
Huna hoja ya msingi.Kwa namna ulivyoteua ma-DC sioni kama uko serious. Nafasi ya u-DC inashuka hadhi kila kukicha, kwa sababu inaonyesha kila mtu anaweza kitu ambacho si kweli.
DC ni mtu ambaye anatakiwa atoe dira ya maendeleo ya wilaya yake lakini kwa baadhi ya hawa uliowateua ni sawa na wapiga debe wa daladala! DC ni mtu ambaye anatakiwa kumshauri RC kudumisha amani ndani ya wilaya yake lakini hawa ni ma-DJ watakaokesha katika kumbi za starehe. DC ni mlezi wa vijana katika wilaya yake lakini hawa ni comedians.
Kwa kifupi hakuna uongozi katika wilaya, hakuna mlezi, hakuna busara uliyopeleka wilayani bali kuna washereheshaji! Tafadhali Rais Samia hebu kuwa serious kidogo wananchi tupate imani! Nalilia nchi yangu inavyoangamia! Hawa vijana wako angalau wangepewa orientation ya uongozi!
Mungu ibariki Tanzania!