Hivi kweli Rais Samia umedhamiria kuleta maendeleo nchini?

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
7,535
2,000
Kwa namna ulivyoteua ma-DC sioni kama uko serious. Nafasi ya u-DC inashuka hadhi kila kukicha, kwa sababu inaonyesha kila mtu anaweza kitu ambacho si kweli.

DC ni mtu ambaye anatakiwa atoe dira ya maendeleo ya wilaya yake lakini kwa baadhi ya hawa uliowateua ni sawa na wapiga debe wa daladala! DC ni mtu ambaye anatakiwa kumshauri RC kudumisha amani ndani ya wilaya yake lakini hawa ni ma-DJ watakaokesha katika kumbi za starehe. DC ni mlezi wa vijana katika wilaya yake lakini hawa ni comedians.

Kwa kifupi hakuna uongozi katika wilaya, hakuna mlezi, hakuna busara uliyopeleka wilayani bali kuna washereheshaji! Tafadhali Rais Samia hebu kuwa serious kidogo wananchi tupate imani! Nalilia nchi yangu inavyoangamia! Hawa vijana wako angalau wangepewa orientation ya uongozi!

Mungu ibariki Tanzania!
 

Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
7,535
2,000
Mimi naona sawa tu, yuko serious kabisa, kwa nafasi isiyo na "qualification" unaweza vipi kumlaumu mtu kwa machaguo aliyofanya?

Laumu Katiba mbovu tuliyonayo, usimlaumu alietumia mapengo/udhaifu wa Katiba iliyopo kutoa ajira kwa awapendao.
Pamoja na ubovu wa katiba lakini lazima kuwe na seriousness katika maendeleo ya nchi. Tunaweza kuwa na viongozi wasiokubalika kidemokrasia lakini tupate maendeleo!
 

N'yadikwa

JF-Expert Member
Aug 10, 2014
5,721
2,000
Acheni dharau wateule almost wengi wa uDC ni wasomi wazuri sana huyo mfungua mageti wa filamu za Kanumba ana Masters MPA, Nikki ana Masters Simalenga msomi, Mwaipaya Msomi.

...huo u serious mnaoujaji ni upi....wateule wote ni makada wa chama Chao na wenye rekodi safi...acheni roho za kichawi waacheni vijana wenzenu wakafanye kazi na kuijenga Tanzania.

Kuna watu huwa mnajikuta nyie ndio mnastahili sana...mnajihesabia haki...hao waliopata wamekuwa vetted na wana sifa stahiki waacheni wakafanye kazi tuache kutia siasa kwenye kila kitu.

Ukiona unaumia uteuzi au mafanikio ya mwenzio na Huna sababu za msingi jitambue Huna tofauti na MCHAWI
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom