Hivi kweli Rais Samia umedhamiria kuleta maendeleo nchini?

Hapana, usahihi ni tumetoka kwenye moto mkali tumeingia kwenye kikaango.
EeeenHeeee!

Nacheka huku nikilia machozi kwa nchi yangu Tanzania.

Tunatoka kwenye kikaango tunaangukia kwenye makaa ya moto mkali.

Mungu Ibariki Tanzania.
 
Hapana, usahihi ni tumetoka kwenye moto mkali tumeingia kwenye kikaango.
Nilipata shida kidogo kuiweka nilivyoiweka; kwa sababu mwanzo nilitaka kuiweka kama ulivyoiweka hapa wewe.

Kwa vyovyote na iwavyo, hakuna nafuu kokote.
 
Mkuu ungekuwa specific basi, unamaanisha woooote hawafai...yaaani mpaka na Jokate !!?
Kwa namna ulivyoteua ma-DC sioni kama uko serious. Nafasi ya u-DC inashuka hadhi kila kukicha, kwa sababu inaonyesha kila mtu anaweza kitu ambacho si kweli.

DC ni mtu ambaye anatakiwa atoe dira ya maendeleo ya wilaya yake lakini kwa baadhi ya hawa uliowateua ni sawa na wapiga debe wa daladala! DC ni mtu ambaye anatakiwa kumshauri RC kudumisha amani ndani ya wilaya yake lakini hawa ni ma-DJ watakaokesha katika kumbi za starehe. DC ni mlezi wa vijana katika wilaya yake lakini hawa ni comedians.

Kwa kifupi hakuna uongozi katika wilaya, hakuna mlezi, hakuna busara uliyopeleka wilayani bali kuna washereheshaji! Tafadhali Rais Samia hebu kuwa serious kidogo wananchi tupate imani! Nalilia nchi yangu inavyoangamia! Hawa vijana wako angalau wangepewa orientation ya uongozi!

Mungu ibariki Tanzania!
Yaani kweli Nikki wa Pili anaenda kulisimamia na kuwa juu ya jeshi la polisi la wilaya pamoja na maafisa usalama wilaya???
 
Mmeanza uchawi wenu siyo?

Si huwa mnademka humu kwamba mama yuko vizuri?

Ulitaka ateuliwa Lisu au? Mtanyooka tu wapuuzi nyie!

Mibavicha sijui mna matatizo gani?

Mods unganisha huu uzi na ule wa uteuzi

Tuliza Wenge wewe ,Nyinyi kila kitu kusifia,hautakiwi kusifia kila kitu mkuu ,mtu akifanya vizuri anasifiwa akifanya vibaya anaambiwa ukweli....Huo ndio uhuru wa kutoa maoni.
 
Halafu kwa uelewa wangu, nilikuwa najua ma DED angalau ni wale waajiriwa wa serikali wenye uzoefu, mfano wakuu wa idara katika halmashauri. Kwa sababu mkurugenzi anaenda kusimamia uchumi wa halmashauri. Ngoja tusubiri tuone.
Yatakuwa yaleyale maana Mwendazake aliteua makada waliofeli ubunge wote kuwa ma DED,ma DC,ma Das kwa hiyo usitegemee tofauti hivi ni vyeo vya Wana system.

Kingine kwani kupanga maendeleo ya Halmashauri kunahitaji elimu gani maana changamoto zinajulikana ni ufinyu wa vyoo,vyumba vya madarasa, hospital,maji nk ..Sasa mambo hayo yanahitaji uwe na elimu?
 
Huo ni ujinga uliopita kiwango cha lami. Alikuwa makamu wa rais. Je, alikuwa hashirikishwi? Kama ni hivyo kwa nini hakuachia ngazi? Huwezi kuongoza nchi kama NGO, ndio mawazo ya kutumia BTC hayo.
Ondoa Uboya, angeachia ngazi angepata hiyo nafasi kivipi? Yule jamaa aliwahi kumshirikisha nani? Uliwahi sikia wapi mtu kuondoka benchi la sub kwakuwa aliye uwanjani anacheza vizuri au vibaya?
 
DC ni cheo ambacho hata kisipokuwepo hakuna kitakachokwama.

Sema maRPC ndio watakaopata tabu, imagine utatakiwa kuwaheshimu hao kama wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama

Uaskari ni kazi ngumu sana.
sema ma OCD sio ma RPC.

rpc ngazi yake ni RC.kama yeye ni mzito basi kazi anayo.
 
Back
Top Bottom