Hivi kweli mtu anasomea Pharmacy miaka 4 kuja kugawa dawa tu? Serikali rekebisheni hili

Umeusemea vyema mjadala:

1: Kila mmoja ni muhimu kwa mwenzake.

2: Kila mmoja amesoma masomo ya mwenzake ila akijielekeza zaidi kwenye sehemu yake.

3: Wote wanakutana katikati katika kumhudumia mgonjwa.

4: Kazi ya mfamasia si kugawa dawa tu kama watu wanavyowatizama. Wafamasia ni sehemu ya drug molecules development/ugunduzi wa dawa.

5: Wafamasia ni watu wanaotakiwa kufanya compounding of molecules/kutengeneza michanganyiko ya dawa kulingana na mahitaji ya taasisi husika kwa usalama.

6: Mfamasia ni sehemu ya mnyororo wa manunuzi ya dawa na vifaa tiba kwa taasisi.

7: Mfamasia ni srhemu ya mnyororo wa utunzaji salama wa dawa na vifaa tiba.

8: Mfamasia ni mratibu wa matumizi ya dawa na vifaa tiba.

9: Mfamasia ni mratibu wa makosa yasiyokamilika/near miss kwenye utoaji wa tiba.

10: Mfamasia ni mratibu wa mpangilio wa dawa kwenye eneo la kazi.

11: Mfamasia ni mratibu wa madhira tarajiwa na yasiyotarajiwa ya dawa kwenye eneo lake.

12: Mfamasia ni mtoa elimu ya matumizi ya dawa kwa wateja anaowahudumia.

13: Nk.👇

Hivyo, hawa watu wanahitajiana sana. Mtu mmoja kutokutekeleza au kuzembea majukumu si sababu ya kulaumu fani nzima au kuishusha thamani na kinyume chake.

Kutokupata nafasi ya kutimiza majukumu yako kifasaha si sababu ya kuhitaji kazi nyingine kutoka fani tofauti. Tujitahidi kuelewa majukumu ya watu kabla ya kuwajadili na kutoa hitimisho.

Ukiondoa majivuno ya kibinadamu, mfamasia ana nafaai ya kumshauri daktari na daktari ana nafasi ya kumshauri mfamasia. Ni suala la uelewa tu.
Safi sana
 
Hiyo TGHS D ni sawa na TGS D au inakuwa juu kidogo.
TGS D sio sawa na TGHS D
TGS ni ndogo sana ..
TGS(Tanzania Government Scale)
TGHS D( Tanzania Government Health Scale)

Kabla ya ongezeko la Mwaka 2022
TGHS D ilikuwa 1,215,000 (1.2 mil)
TGS D ilikuwa 710K
IMG_20231120_125212_496~3.jpg
IMG_20231120_125149_720~3.jpg
 
ila na mimi naona kama mtoa mada ana hoja,
ila kwanini Pharmacist wasipewe mchakato mzima wa kuanzia ku test dawa, kuotesha wadudu wa ugonjwa, kumimini solution ya dawa , ku test wadudu wamekufa wangapi, kupima ni moles ngapi za compound fulani zimeuwa wadudu wenye miligramu ngapi. kisha ku develop equation ya hiyo reaction. kisha wakafundishwa kwenye real world ni udongo gani ambao una tabia ambazo unaweza kuuchimba sehemu na kuu- subject kwenye equation hiyo zikazalisha dawa ?
Kutest dawa as How?
Maana michakato yote ya madawa wanafanya Pharmacist..
Ila swala la Kuotesha wadudu Hapo utagombana na Scientist (Lab scientist) watakuja juu na wenyewe Hapa 😅😅😅

Maana wao ndo wanaohusika na shughuli zote za Maabara pamoja na Wadudu wote iwe ni microbiology au parasite

Na maswala ya Udongo watu wa SUA ma Agrochemistry watakuua 🤣🤣
 
Dah Mkuu umesoma Chuo gani ambacho kinakushindwa kujua kuwa...
Wote Daktari na Mfamasia Husoma Pharmacy ila tu Daktari husoma kwa Kiasi kile kimachohusiana na Mgonjwa...

Daktari hubase katika pharmacokinetics na kidogo Pharmacodynamics na Pharmacognosy
na mfamasia hu base kwenye Pharmacodynamics sana na pharmacognosy sana kuliko Daktari...

na ndo Maana daktari hawezi kuelelezea Dawa Ya Amoxycilne imatengenezwaje kwa sababu Hakusoma Pharmacognosy ila Ukimuuliza Dawa inafanyaje kazi kwa Mwili wa Binadamu atakuelezea mpaka inapotolewa na hata madhara yale hutokea vipi...

kwahyo usipotoshe umma Kuwa Kwenye Dawa Daktari hajui...
Japo mfamasia hajui How we Prescribe dawa na Dose maintanance na Kujua Dx ,Hx na Mx..

unaweza ukajua Dawa DUNIA NZIMA ZINATENGENEZWAJE NA ZINAKUWAJE DAWA LAKINI UKASHINDWA KUJUA DAWA GANI INAFAA KWA MGONJWA..

NB: BAHATI MBAYA MGONJWA HATAKI KUJUA DAWA INATENGENEZWAJE NA WAPI NA IMETOKANA NA NINI ANAACHOTAKA NI KUPONA NA DAWA IMLETEE MATOKEO MAZURI
Wewe jamaa umemuelekeza kwa hekima sana.
 
Naam mkuu,tusaidie kuchambua na mchango wa Watu wa Maabara upoje katika tiba.
Kama umesoma vyema, hakuna anaeweza kusema ni muhimu zaidi kuliko mwingine. Wote tunashirikiana.

Daktari anapofika sehemu na Differential diagnosis, huitaji mtu wa maabara kumtatulia utata kwa labda kuthibitisha au kukanusha mambo. Kama mtu wa maabara akiamua atafute umwamba kwa mtoa huduma mwingine basi tutaokota watu wengi mtaani. Ukipewa majibu ya sukari iko juu, tayari utaenda kuua. Ukiambiwa hana malaria wakati anayo hapo ni shida.

Hivyo, tunahitajiana kwa kiasi kilekile kwa kila/fani au mmoja mmoja ni suala la kuthamini kazi ya mwenzako hata kama una exposure nayo.

Ni kila mmoja atimize wajibu wake na kufuata miongozo.
 
Daktari ni mtaalamu wa tiba ambaye anajihusisha na utambuzi, matibabu, na kuzuia magonjwa. Wanaweza kuwa na ujuzi katika fani mbalimbali kama vile upasuaji, ndani ya dawa ya ndani, au upasuaji wa akili.

Mfamasia, au mtaalamu wa dawa, ni mtaalamu wa dawa na anajishughulisha na utoaji wa dawa na ushauri wa kiafya kuhusu matumizi sahihi ya dawa. Wanaweza kufanya kazi katika maduka ya dawa, hospitali, au kampuni za dawa.

Kwa ujumla, daktari ni mtaalamu wa tiba anayefanya utambuzi na matibabu, wakati mfamasia ni mtaalamu wa dawa anayetoa huduma za dawa na ushauri kuhusu matumizi sahihi ya dawa.
 
Nje ya mada,, hivi hii mitihani ya leseni huwa ina umuhimu gani? Wakat mtu kashafaulu mitihani yote kwanzia level ya kwanza mpka level ya mwisho.... yaan mtu unasoma mwaka wa kwanz mpka wa mwisho unafaulu vizuri alf tena unatakiwa ufanye mtihan wa leseni na maswali yanayo toka yanaanzia mwaka wa kwanza semestr ya kwanza mpka mwaka wa mwisho semestr ya mwisho...ni kwamba hao Pharmacy council wanataka wajiridhishe kwa lipi?? Alf maswali yenyew unakutana na snalio za kutosha??
Mwenye uelewa jamn anisaidie
 
Nimewahi kuwaza hili ingawa Mimi siko kwenye tasnia ya afya.
Anayeandika au kuamuru mgonjwa atumie dawa ipi ni doctor, anayeamua mgonjwa atumie vipi dawa ni doctor. Sasa rule ya pharmacist ni nini?

yani vituko tu,wafamasia walipaswa wawe viwandani au kwenye maabara kugundua na kutengeneza dawa sio kungangania dirisha la kugawa dawa.
 
Back
Top Bottom