Hivi kweli, mfumo dume si ni laana ya mwanamke?

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,502
Reaction score
911,255
Tacaids na Unicef jana walikoroga majambozi!
Ugomvi wao ni kubeza mfumo dume na hawana jipya!
Wadai mabinti "wakipigwa", chanzo ni mfumo dume!
Mabinti wanapotusonga "tuwawezeshe" lawama mfumo!
Hivi kweli, mfumo dume si ni laana ya mwanamke?

Kabla ya bibie kuumbwa, dunia ilikuwa shwari.
Alipofinyangwa kutoka ubavuni kwangu ukawa mzuka!
Hata bustanini alinikwepa na akazururazurura kivyake!
Nyoka alipomwona kazubaazubaa, alimkazia kibuti!
Hivi kweli, mfumo dume si ni laana ya mwanamke?

Yawaje bibie atamani kufanana na Muumba asisulubiwe?
Yawaje atamani kujua mema na mabaya asiwe uchi?
Yawaje arubuniwe na nyoka ategemee asitawaliwe?
Yawaje aniletee shombo ya nyoka halafu nisimtawale?
Hivi kweli, mfumo dume si ni laana ya mwanamke?

Muumba ni mwenye haki, hakika tusimkejeli kamwe!
Muumba ajua yote hata kututendea haki sote!
Muumba aliiona tamaa ya bibie na kumfunza nayo!
Muumba alimweka alama ya tamaa bibie lawamani!
Hivi kweli, mfumo dume si ni laana ya mwanamke?

Tamaa ya kuwa Muumba sasa yachakachuliwa!
Tamaa ya kuwa mjuaji sasa yageuziwa kibao!
Tamaa ya makubwa sasa ni mtaji wa siasa!
Tamaa ya bibie sasa ni shubiri yake apende au la!
Hivi kweli, mfumo dume si ni laana ya mwanamke?

Mfumo dume ndo utamaduni sahihi, manake upo mpaka kwenye vitabu vitakatifu vya Mungu

Mungi...wanaoukataa mfumo dume wamemkataa Muumba a amri zake kwetu sasa watarajie mabaya kuwakuta.............
 
Last edited by a moderator:
Na kwenye kutoa pesa na kuwatunza wake zenu MUWE MSTARI WA MBELE HIVIHIVI sio masuala ya kiuchumi mnajivua gamba na kutaka michezo kisasa ya cost sharing!

Mwanume hana lolote kimbelembele ndo yake haiba
Vitabu vitukufu kaandika yeye, basi hakusita ukubwa kuubeba
Kumdidimiza mwenzie ili hali sote binadam ndo wake ujuba
Ukimchuna utapunguza machungu si haba
Wanaume walikuwa zamani siku hizi migumegume

Mleta mada nyimbo zimekuisha huna sera
Wanaume wa siku hizi migumegume isiyo na sera
Ndoa zimeshinda wazikimbia kutwa kukwea mipera
Wassio oa wagoma gomo kuachana na ukapera

Kuzaliwa mwanamke tayari ni mtaji tosha
Waishi kwa raha wala huna haja ya kujichosha
Ukiolewa ukiona shida shida wasema babu yatosha
Warudi kwenu hukawii kumpta utayemtosha

Hapana sifikirii kama ni laana. Tatizo binaadamu ameuchakachua huo mfumo kwa kuondoa/kuacha mambo ya msingi katika huo mfumo. Ili mfumo huo uweze kufanya kazi iliyokusudiwa kila upande unazo haki lakini pia una majukumu unatakiwa kufanya/kutimiza. Sasa kwa kiasi kikubwa, tunabaki kudai haki inayotokana na mfumo huo bila ya kutumia nguvu hiyohiyo kutimiza majukumu yetu.
 
lara 1 bisha khodi kwa kuukana mfumo jike
pekuapekua kwanza uone mfumo jike anavyokutesa.
Wanaumme kukimbia baada ya kuwalambisha asali
Wao wanataka kisaidizi siyo bosi wa pili ndani ya jumba
Bisha tena khodi nami nitakupokea kwa ukunjufu...............
 
Last edited by a moderator:
Hapana sifikirii kama ni laana. Tatizo binaadamu ameuchakachua huo mfumo kwa kuondoa/kuacha mambo ya msingi katika huo mfumo. Ili mfumo huo uweze kufanya kazi iliyokusudiwa kila upande unazo haki lakini pia una majukumu unatakiwa kufanya/kutimiza. Sasa kwa kiasi kikubwa, tunabaki kudai haki inayotokana na mfumo huo bila ya kutumia nguvu hiyohiyo kutimiza majukumu yetu.

SMU tuanze kukiri mfumo dume ni matakwa ya Muumba ila usitumike kuwanyanyasia wenzetu..........marekebisho yanahitajika lakini siyo kuuponda kama jana nilivyona kwenye luninga.........
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Mie wanawake zangu wooooooteeee wananikubali sababu ya mfume dume nawahudumia ipasavyo........!:madgrin:
 
Kimbweka hebu mbipu lara 1 maana hizo nd'o zake hizo.............
 
Last edited by a moderator:
na kwenye kutoa pesa na kuwatunza wake zenu muwe mstari wa mbele hivihivi sio masuala ya kiuchumi mnajivua gamba na kutaka michezo kisasa ya cost sharing!

Mwanume hana lolote kimbelembele ndo yake haiba
vitabu vitukufu kaandika yeye, basi hakusita ukubwa kuubeba
kumdidimiza mwenzie ili hali sote binadam ndo wake ujuba
ukimchuna utapunguza machungu si haba
wanaume walikuwa zamani siku hizi migumegume

mleta mada nyimbo zimekuisha huna sera
wanaume wa siku hizi migumegume isiyo na sera
ndoa zimeshinda wazikimbia kutwa kukwea mipera
wassio oa wagoma gomo kuachana na ukapera
wanaume walikuwa zamani siku hizi migumegume

kuzaliwa mwanamke tayari ni mtaji tosha
waishi kwa raha wala huna haja ya kujichosha
ukiolewa ukiona shida shida wasema babu yatosha
warudi kwenu hukawii kumpta utayemtosha
wanaume walikuwa zamani siku hizi migumegume
umemweza kweli kweli
 
Na kwenye kutoa pesa na kuwatunza wake zenu MUWE MSTARI WA MBELE HIVIHIVI sio masuala ya kiuchumi mnajivua gamba na kutaka michezo kisasa ya cost sharing!

Mwanume hana lolote kimbelembele ndo yake haiba
Vitabu vitukufu kaandika yeye, basi hakusita ukubwa kuubeba
Kumdidimiza mwenzie ili hali sote binadam ndo wake ujuba
Ukimchuna utapunguza machungu si haba
Wanaume walikuwa zamani siku hizi migumegume

Mleta mada nyimbo zimekuisha huna sera
Wanaume wa siku hizi migumegume isiyo na sera
Ndoa zimeshinda wazikimbia kutwa kukwea mipera
Wassio oa wagoma gomo kuachana na ukapera
Wanaume walikuwa zamani siku hizi migumegume

Kuzaliwa mwanamke tayari ni mtaji tosha
Waishi kwa raha wala huna haja ya kujichosha
Ukiolewa ukiona shida shida wasema babu yatosha
Warudi kwenu hukawii kumpta utayemtosha
Wanaume walikuwa zamani siku hizi migumegume

Kuna Mindumendume siku hizi hujakutana nao nini......?
Full midolali.....!:becky:
 
Mwanamalenga Rutashubanyuma nakubaliana na wewe kuwa Mwanamke hawezi kuwa sawa na Mwanamke japo sote tu viumbe tulioumbwa na Mungu lakini Mwenyezi Mungu alitupa uwezo na majukumu tofauti. Naona tabu si mfumo dume bali Wanaume wanaoabuse mfumo huo kwa kutokuwa responsible enough na kutambua uzito wa jukumu walilopewa
 
Last edited by a moderator:
umemweza kweli kweli

nivea nawe kumbe umo kwenye hili kundi la waliopotea na wanajitutumua? Kidume wa kweli hawezi kukuvumilia na itakula kwako.........
 
Last edited by a moderator:
Kuna Mindumendume siku hizi hujakutana nao nini......?
Full midolali.....!:becky:

Kimbweka siku za lara 1 zinahsabika kabla hajakutana na saizi yake na hapo ndipo tutasikia kilio chake....njemba haitamkawiza.......
 
Last edited by a moderator:
asante sana kwa maelezo yakinifu kwa kweli Rutashubanyuma nieleze tafadhali wahindi hutumia mfumo gani katika maisha yao and you see themm living that happy?nijibu tafadhali

nivea mfume dume ndiyo unampa mwanamke hauweni................ukiona ana unafuu basi ujue ni mfumo dume hakuna cha usawa kabisa........dume wa kweli lazima awe kichwa na mwanamke ni mkia wake tu.................vinginevyo ngumi itamrekebisha.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom