Hivi kwanini Tanzania hatuna Wapelelezi Binafsi (Private Investigators)?

Desprospero

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
887
2,201
Suala la Ulinzi na Usalama ni agenda muhimu duniani. Mfumo wa Kipolisi peke yake haiwezi kuweka mazingira salama.

Nitoe mifano michache nchi kama Marekani, Uingereza, Canada, Urusi, India, China, South Afrika, Misri na hata Israeli. Pamoja na kuwa na vyombo strong vya Ulinzi na Usalama zikiwemo mashirika ya kijasusi lakini still wametoa room ya kuwa na PI zinazoweza kusaidiana na Polisi, Usalama wa Taifa nk kufanya Upelelezi ama uchunguzi kubaini masuala ya usalama.

Mashirika haya hulipwa na ama na Serikali au makampuni na hata watu binafsi yenye kuhitaji huduma zao. Siamini vyombo vyetu vinaweza kila kitu. Yapo matukio hapa nchini naamini tungekuwa na PIs yangewezekana. Mfano kupotea kwa watu katika mazingira tatanishi.

Nashauri Bunge kutunga sheria itakayoruhusu kuanzishwa Kwa taasisi kama hizi kwa nia njema kusaidiana na vyombo vya usalama. Sio kila suala la investigative lazima kufanywa na Polisi na TISS.

Nawasilisha kwa majadiliwno ya kujenga.
 
Ili wakiumbue chama chetu?na serikali Kwa vifo tata ambavyo hatuna ushahidi navyo isipokua ule was kiroho TU yaani nafsi kugoma kama wengi tulivogoma kuhusu jiwe!
 
Hakika, tumechelewa sana kama nchi. Jambo hili lilipaswa kuanza pindi tu nchi ilipoingia kwenye uchumi wa soko huria. Tatizo dola inaona kama bado ni mmiliki wa usalama wa watu/Taifa na kwa upande mwingine kikatiba suala la ulinzi na usalama ni wajibu wa kila raia. Huduma hii kwa upande mwingine itazalisha ajira!
 
Hata zikiwepo zitakuwa za makada wa CCM
Hapana hapo tutaangalia Professionalism. Si kila taaluma uajiriwe na Serikali. Ulinzi ni taaluma kama zingine. Mtu anaweza kujiajiri maadamu asivunje sheria na miiko Yao.

Kama wewe umesomea Uanajeshi ukaamua kuachana na JWTZ unaweza kuuanzisha kampuni ya Ulinzi na ukasaidia nchi. Kwa nini wanaosomea uTISS wasiwe na makampuni Yao ya security?
 
Hapana hapo tutaangalia Professionalism. Si kila taaluma uajiriwe na Serikali. Ulinzi ni taaluma kama zingine. Mtu anaweza kujiajiri maadamu asivunje sheria na miiko Yao. Kama wewe umesomea Uanajeshi ukaamua kuachana na JWTZ unaweza kuuanzisha kampuni ya Ulinzi na ukasaidia nchi. Kwa nini wanaosomea uTISS wasiwe na makampuni Yao ya security?
Ndiyo hao watakuwa makada wa CCM, vinginevyo hawatapewa leseni
 
Unataka wachunguzi huru wamtie hatiani chairman wa ufipa maana pale kwenye cov-19 kuna signature ya KM na Mnykt!
 
Suala la Ulinzi na Usalama ni agenda muhimu duniani. Mfumo wa Kipolisi peke yake haiwezi kuweka mazingira salama.

Nitoe mifano michache nchi kama Marekani, Uingereza, Canada, Urusi, India, China, South Afrika, Misri na hata Israeli. Pamoja na kuwa na vyombo strong vya Ulinzi na Usalama zikiwemo mashirika ya kijasusi lakini still wametoa room ya kuwa na PI zinazoweza kusaidiana na Polisi, Usalama wa Taifa nk kufanya Upelelezi ama uchunguzi kubaini masuala ya usalama.

Mashirika haya hulipwa na ama na Serikali au makampuni na hata watu binafsi yenye kuhitaji huduma zao. Siamini vyombo vyetu vinaweza kila kitu. Yapo matukio hapa nchini naamini tungekuwa na PIs yangewezekana. Mfano kupotea kwa watu katika mazingira tatanishi.

Nashauri Bunge kutunga sheria itakayoruhusu kuanzishwa Kwa taasisi kama hizi kwa nia njema kusaidiana na vyombo vya usalama. Sio kila suala la investigative lazima kufanywa na Polisi na TISS.

Nawasilisha kwa majadiliwno ya kujenga.
Naunga mkono hoja, Tanzania tunayo sheria ya private prosecution ila unaomba kibali kwa DPP, hivyo PI itakuwa ni unaomba kibali kwa DCI.

Baada ya Serikali yetu kushindwa kulichunguza shambulio la Lissu, watu humu, tulijitolea kusaidia WanaJF, je tuisaidie Serikali yetu inaposhindwa au tusubiri ishindwe, tuibeze na kuizomea kuwa haiwezi?
P
 
Back
Top Bottom