Hivi kwanini Mungu ana wivu?

Hivi kwanini Mungu ana wivu?

Niki kwambia mimi Infropreneur ni Mungu halisi na hakuna mwingine utakubali?

Utakuwa na uthibitisho wa uwepo wa Mungu wako unayesema yupo, uje naye au umwambie aje ani prove wrong kwamba mimi infropreneur sio Mungu, yeye ndio Mungu?

Ataweza kuja?
Kitakachofanya nikubali au nisikubali ni kutokana na ulinganishi wa sifa/ tabia.
kitu hakipo unakithibitishaje?ebu wacha ujinga basi.
Toa reason zenye maana, ujinga ni sehemu ya kujifunza.
 
Wataalamu wa bibilia, nakumbuka kuna siku nilisoma hicho kitabu nikaona historia ya mnara wa babeli Mungu aliposhuka na kuwakuta binadamu wanatengeza ule mnara alishtuka na kuwatenganisha kwa lugha pamoja na maeneo ndiyo yakazaliwa mataifa mengine.

Tukio la pili kwenye sura ya mwanzo Mungu baada ya adamu kula ule mti ambao alikatazwa inaonekana ibilisi alikuwa anajua siri ya mti huo wa uzima japo hakuufahamu haswa ni upi ila baada ya Mungu kuona binadamu na jeshi lake watapanga kuutafuta ndiyo akauficha, nimesahau exactly ni wapi.

Case ya tatu, baada ya kuwatoa Wanaisraeli kupitia Mtume wake Musa aliwaambia kuwa yeye ni Mungu mkuu na anawivu hivyo wasiabudu mwengine isipoikuwa yeye.

Je, kwa kauli ya kusema kuna miungu mengine anafahamu kuwa kuna nguvu nyengine tofauti na yeye?

Je, hajiamini na nguvu zake?

Je, Mungu huyu ni tunayemuabudia wakristo na waislamu?

Je, ni binadamu wa mwanzo ambaye aliwahi kutambua siri za ulimwengu na akajitahidi kuzificha na hatimaye akajitolea taji la uungu?

Nawasilisha.
NI wanadamu tu tumekosa neno la kutumia kukataza ibada za vitu vingine.

Ila kwa ukuu wa Mungu kuona wivu huu wa kibinaadamu haiwezekani.

Kwa nini nnasema hivi?

Ni kwa sababu wivu unahitaji hao wanaooneana wawe wanalingana au basi wanakaribiana katika uwezo wao wa hicho kitu. Mfano mwanafunzi kumuonea wivu jirani ake aliyempita alama 5. Lakini mwanafunzi wa darasa la tano hayuko kumuonea wivu yule wa darasa la sita maana hawalinganishiki. Umeonaa🤔

Sasa kwa UKUU wa Mungu hana anayekaribiana naye hata amuonee wivu. Hicho kitu hakipo.

Ni basi tu vile wanaadamu tumejitahidi kujaribu kuvaa viatu vya Mungu tukaishia kuwa wanaadamu na ndio tukaweka mambo ya wivu. Tumemuanthropomorphize Saa Godi na tumefeli
 
Kitakachofanya nikubali au nisikubali ni kutokana na ulinganishi wa sifa/ tabia.

Toa reason zenye maana, ujinga ni sehemu ya kujifunza.
unajua maana ya reasoning?au ni neno limekujia tu?
 
nimesema wivu sio kinyongo na mtu mpaka awe na hicho kinyongo huwa akili yake haipo katika kufanya kazi.
Nitolee mfano wa hiyo terminology 'wivu' badala ya 'kinyongo'.

Maana yake, mwenzako naviona kama mamba na kenge wakisafiri pamoja
 
kitu hakipo unakithibitishaje?ebu wacha ujinga basi.
Maana ya uwepo ni nini?

Tunasema mhafidhina07 yupo kwa sababu gani? Kwa sababu unaonekana? Au kwa sababu uwepo wako unaaffect utendaji wa binadamu wanaokuzunguka?

Wewe lets say upo Tandale, as long as uwepo wako hapo Tandale hauna effect kwa watu waliopo uarabuni kwenye ulimwengu wao unaexist? Upo hata kwa kufikirika tu?

kuna makanisa kwa jina la MUNGU, kuna masinagogi kwa jina la MUNGU, kuna misikiti kwa jina la MUNGU, kuna mauaji kwa jina la MUNGU, kuna misaada kwa jina la MUNGU, kuna mijadala kwa jina la MUNGU.

Kati ya wewe na jina MUNGU nani ana affect maisha ya binadamu wengi? Binafsi naona MUNGU anaexist sehemu nyingi kuliko wewe unavyoexist.
 
Isaya 40: 28

"Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki."

Naona watu wanataka kujitoa ufahamu, Yaani wewe uumbe kinyago chako alafu kinyago kitake kukuzidi uwezo!😄 Reasoning za Mungu kamwe haziwezi kulingana na reasoning za binadamu! Akili zake ni very far completely kutoka kwenye uelewa wa akili zako mtoa mada, ni kama infinity minus zero! Yeye yupo kwenye realm na time frame ya tofauti na wewe! Kama aliweza kukutengeneza pia hashindwi kukuwekea mipaka ya ufahamu kwenye akili zako!
 
NI wanadamu tu tumekosa neno la kutumia kukataza ibada za vitu vingine.

Ila kwa ukuu wa Mungu kuona wivu huu wa kibinaadamu haiwezekani.

Kwa nini nnasema hivi?

Ni kwa sababu wivu unahitaji hao wanaooneana wawe wanalingana au basi wanakaribiana katika uwezo wao wa hicho kitu. Mfano mwanafunzi kumuonea wivu jirani ake aliyempita alama 5. Lakini mwanafunzi wa darasa la tano hayuko kumuonea wivu yule wa darasa la sita maana hawalinganishiki. Umeonaa🤔

Sasa kwa UKUU wa Mungu hana anayekaribiana naye hata amuonee wivu. Hicho kitu hakipo.

Ni basi tu vile wanaadamu tumejitahidi kujaribu kuvaa viatu vya Mungu tukaishia kuwa wanaadamu na ndio tukaweka mambo ya wivu. Tumemuanthropomorphize Saa Godi na tumefeli
that great bro,nilitaka walau jibu liwe hivyo na kama ulifatilia post zangu za nyuma niliuliza swali je,mungu ameumba nguvu inayokinzana nae?kiini cha swali hili kimetokea hapo nimeona gaps kwenye bibilia.
 
Hitimisho lako ni kuwa hakipo nikumaanisha umethibitisha hakipo, kushindwa kuthibitisha absent yake ni kumaanisha hujui, ni heri ungesema bado sijaikubali knowledge inayoongelea uwepo wa Mungu ningekuelewa ila wewe umesema hayupo hapo nikumaanisha uneshafanya research za kutosha kuthibitisha kauli yako, hivyo nithibitishie kulingana na research zako.

Mimi nakuthibitishia kulingana na maandiko ya biblia pili kukingana theory ya bing bang (time, space, matter and energy) naongelea energy.
Nyie mwanadai kuna Mungu sie twasema hayupo, kimatinki kabisa haiwezekani kuthibitisha kitu ambacho hakipo , wanaodai Mungu yupo wathibitishe ili kukanusha madai yetu ya kutokuwepo kwake.
 
Hahahah Kitu kisichokuwepo Unawezaje kuthibitisha kama Hakipo😅😅

Nimefurahi Conversation yenu Ndo maana nimetia Neno tu..

Kisayansi kuthibitisha kama kipo au hakipo lazma kuwepo kwanza kitu kinachofanana na hicho ili ukifananishe..

kwa mfano unaweza kusema "Mimi sina macho" kwa sababu Umewahi kuyaona Macho au kuyasikia macho..

Ni Vigumu kumwambia Kipofu Athibishe kwa kuelezea tifauti Kati ya Basi na Coaster.. (Kwa sababu hajawahi kuviona)..

Naweka sawa kwamba nimependa Conversation Yenu kuhusu Uthibitisho wa kitu Kisichokuwepo..
Ila....

"I mean no malice toward anybody."
Na ndo hapa sasa swali la tafsiri ya kutokuwepo MUNGU inapozaliwa. Mtu anaposema hayupo, anamaanisha nini?
 
NI wanadamu tu tumekosa neno la kutumia kukataza ibada za vitu vingine.

Ila kwa ukuu wa Mungu kuona wivu huu wa kibinaadamu haiwezekani.

Kwa nini nnasema hivi?

Ni kwa sababu wivu unahitaji hao wanaooneana wawe wanalingana au basi wanakaribiana katika uwezo wao wa hicho kitu. Mfano mwanafunzi kumuonea wivu jirani ake aliyempita alama 5. Lakini mwanafunzi wa darasa la tano hayuko kumuonea wivu yule wa darasa la sita maana hawalinganishiki. Umeonaa🤔

Sasa kwa UKUU wa Mungu hana anayekaribiana naye hata amuonee wivu. Hicho kitu hakipo.

Ni basi tu vile wanaadamu tumejitahidi kujaribu kuvaa viatu vya Mungu tukaishia kuwa wanaadamu na ndio tukaweka mambo ya wivu. Tumemuanthropomorphize Saa Godi na tumefeli
Umejibu kwa akili sana , japo haujawaambia ukwel vijana kuwa Mungu ni nadharia tu.
 
Back
Top Bottom