Hivi kwanini maafisa uajiri wanajisikia sana?

The Humble Dreamer

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
6,889
2,000
Wakuu Salaam;

Hawa watu wanaosimamia idara ya rasimali watu wanatakiwa watambue kua wao nao ni binadamu kama watu wengine na lazima waheshimu utu wa mtu yeyote achilia mbali hadhi ya huyo mtu.

Hawa Hr's wa kampuni hua na majibu ya hovyo sana wawapo kazini bila kujali anamjibu nani.

Leo nimeenda kuulizia tenda kwaajili ya kuleta mazao fulan kwa hiyo kampuni kwaajili ya kutengeneza vyakula vya kuku, nikaambiwa Hr ndiyo yupo kwa leo, ile kuonana nae tu akaniambia 'kaa hapo'. Kwa hii kauli nilitaka nivue kiatu changu nimzibue nacho nikajizuia. Nikajikaza kukaa dakika 2 nikaondoka zangu bila kumwelezea kwa upana biashara yangu na nia ya kufika kwenye kampuni. Hajajua Mimi nikileta mazao kampuni mwao ndiyo bidhaa zao zikiuzwa wanakuja kulipwa badaye mishahara.

Kufika nje nikamwelezea mfanya kazi mmoja akanishauri nimsubiri Mkurugenzi mwenyewe. Mfanya kazi akanieleza kua kwa saivi wanahitaji mzigo kwani stock inakaribia kuisha.

Huyohuyo mfanyakazi akaniambia hata wakati akiomba kazi na hata wengine pia walipata shida sana kwa huyo HR kusajiliwa.

Sasa nikajiuliza HR kiburi anatoa wapi wakati ilikua ni bahati mbaya tu kumkuta yeye?

Nyie HR specialists na HR managers msione hizo kampuni ni zenu, Bali toeni Huduma kwa jamii kwa weledi na kuheshimu utu wa mtu kwani wote tuko kwenye utafutaji.

Je, wewe binafsi Ulishawahi kukereka na HR kwa lolote?
 

MIGUGO

JF-Expert Member
Dec 3, 2011
1,780
2,000
Crdb na bank kibao wanatoa salary advance kwa simu banking asikubabaishe kanywe bia.Naona huna hela leo.
 

Madame S

JF-Expert Member
Mar 4, 2015
15,466
2,000
Kuna kidada kimoja ni HRO wa ofisi fulani jijini tanga yan huyu had kazi anafanyiwa na SPRO yan huyo SPRO ndio anampanda kichwani yeye akisema tusisaini hawasaini ana ubaguzi mno mno na ni wa wazi wazi sjui wanajikuta wao ni nani yan hua namwambiaga hicho kiti walikalia wengi kabla yako hata wewe utakiacha na wengine watakuja watakiacha usijisikie sana as if unapumua pumzi grade A tena free sisi wengine tunapumua labda kwa mkopo
 

munkango

JF-Expert Member
Sep 12, 2016
314
500
Ulikuwa na miadi naye muda huo?, yaani mtu kukuambia usubiri kidogo basi unaondoka baada ya dakika mbili na kuja kuleta malalamiko hapa?
 

jikafhplgmb

JF-Expert Member
Sep 29, 2018
754
1,000
Tabia ya mtu mmoja usione watu wote hawafai mkuu.

Binafsi ni mwanafunzi wa kozi ya human resources management
Na kwenye Kila course Kuna ethics zake ikiwamo good communication skills

Naomba uyo mtu mlipoti kwa Mkurugenzi atachukuliwa hatua, afu ni ujinga kama hr kuwafanyia watu vibaya kwa sababu Bila wao hakuna company na unajua na umesoma na kufundishwa yote hayo,

Mkuu namuombea msamaha tumekosa, Ila watu wabadilike ata field zingine watu huwa wanazalau sana. Wakati yale ni mamlaka ya mda tu.


Utu ni kitu Cha muhimu Sana.
 

tweenty4seven

JF-Expert Member
Sep 21, 2013
11,336
2,000
kuna kidada kimoja ni HRO wa ofisi fulani jijini tanga yan huyu had kazi anafanyiwa na SPRO yan huyo SPRO ndio anampanda kichwani yeye akisema tusisaini hawasaini ana ubaguzi mno mno na ni wa wazi wazi sjui wanajikuta wao ni nani yan hua namwambiaga hicho kiti walikalia wengi kabla yako hata wewe utakiacha na wengine watakuja watakiacha usijisikie sana as if unapumua pumzi grade A tena free sisi wengine tunapumua labda kwa mkopo
Madame nipe connection yake,nitambadili tabia naja tanga nov
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom