Hivi kuomba msamaha ni makosa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kuomba msamaha ni makosa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by demokrasia, Jul 15, 2011.

 1. d

  demokrasia Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 6, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nimeingia kwenye ugomvi na girlfriend wangu baada ya kumtamkia maneno mabaya nikiwa na hasira. Sababu ya kufikia hatua ya kumtamkia maneno hayo ni baada ya yeye kunigombeza kwa sababu ya kumtafuta kwenye simu ya rafiki yake baada ya kumkosa yeye kwenye simu yake.

  Jambo hilo lilinikera sana kwa sababu sikuona mantiki ya yeye kunikoromea kwa sababu ya issue ndogo kama hiyo. Hilo lilipelekea nikapata hasira na kumtamkia maneno mabaya. Lakini baada ya hasira kuisha, niligundua kuwa sikufanya jambo jema kumtamkia maneno hayo, hivyo nikaamua kumwomba radhi kwa hilo.

  Kitendo cha kujishusha na kuomba msamaha imekuwa kama ndio nimewasha moto kwa sababu hataki kunisikiliza hata kidogo na hata simu hapokei, na hii ni wiki ya 3 hataki kupokea simu yangu?

  Halafu tatizo ni kwamba ninaishi mbali sana na yeye. Mimi nipo Shinyanga na yeye yupo DSM. Nimejaribu kuhusisha baadhi ya marafiki zake wamweleweshe ili anisamehe, lakini ndio kwanza anazidi kuwa mkali.

  Cha kusikitisha ni kwamba nilipoanza tu kuomba msamaha alinitumia sms kwamba "ameamua tu-break up". Sasa najiuliza, hivi kuomba msamaha ni makosa?

  Wana JF naombeni maoni yenu.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Kuomba msamaha sio makosa.

  Swala la kumtafuta kupitia kwa rafiki yake binafsi sioni tatizo hapo...na ndio maana una namba ya rafikiye (naamini kwamba najua na anafurahia wewe kua nayo) ....

  Kama unavyosema umeshaomba samahani kwa kosa la kumsema vibaya ila hataki kukusikia inabidi ujiulize kwanza maneno uliyomtolea yalikua mabaya kiasi gani.Maana hata kama ni mimi mtu akionyesha kunidharau kupitiliza no amount of samahani will make me take him back...hata kama ntasamehe.Na kama ni mazito sana uliyotoa inabidi utafute namna kweli ya kuonyesha kwamba hukumaanisha na kwamba unajutia...

  Ila sasa kama uliyosema sio mzaito sana jua tu mwenzio alikua anatafuta sababu ya kuachana na wewe na sasa ameipata.

  We ndo unaejua kila kitu kwahiyo piga mahesabu.
   
 3. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,701
  Likes Received: 82,626
  Trophy Points: 280
  Pole sana kuomba msamaha wala si kosa. Ulichofanya ni sawa kabisa, labda alikuwa anatafuta sababu ya kuvunja penzi lenu sasa kaipata.   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  kama kabla hata hamjaona inakua hivyo,Tafuta mwingine.Maana hakuna kitu muhimu kama hicho ulichofanya cha kuomba msamaha, na tena kwa kitu ambacho hukupaswa.Ila kwa aijili ya upendo ilibidi.mtu mgumu kusamahe huwe kwenda nae mbali.
   
 5. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Umechokwa mzee!
   
 6. Roulette

  Roulette JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 5,618
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Amekiukataa sababu umembipiga rafiki yake ulipomkosa yeye na pia sababu alipokuuliza maelezo ukamgombeza. sasa wewe unadhani kakukataa kwa kumuomba msamaha? uko mbali na ukweli.
  Na maybe ukute kakukataa kwa sababu nyingine, alikua anatafuta sababu tu. Dar mji wa wajanja...
   
 7. B

  Bi. Mkora JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 33
  Mungu amekufunulia mapema, na ushukuru ni girl friend, huyo hakufai kabisa kama ulikuwa na mpango wa kumfanya mke basi ndio maono hayo.
   
 8. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
  Kosa halipo kwenye kuomba msamaha....!
  Kama amechoka na hakutaki kuachana is inevitable, kumbuka akufukuzae akwambii toka
  na penzi halilazimishwi, wewe mweleze bado unamuhitaji, na kilichobaki mwachie yeye, uamuzi.
  and dont wait too long kama dalili zinaonyesha hakutaki tena labda ni muhimu kwako ku-move on.
   
 9. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,607
  Likes Received: 6,189
  Trophy Points: 280
  Player huna chako hapo, gf unampigia simu wiki 3 hapokei wewe hupati meseji tu? Ukimtafuta kwenye simu ya rafiki yake (anything can happen, labda yuko hospitalini) anakuja juu?

  Angalia usawa mwingine tu, huna chako.
   
 10. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Anatingisha kibiriti. Hebu kula ganzi kwa muda uone atafanyaje.
   
 11. CPU

  CPU JF Gold Member

  #11
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kama Mungu nae angekuwa anachagua makosa ya kusamehe basi hakuna atakaepona.
  Kwenye imani tunakiri "Kusamehe kama tunavyosamehewa" no matter umefanya nini.
  Neno "Msamaha" linamaanisha "Nimejutia nililofanya"

  So kama huwezi kusamehe basi hata Mungu hawezi kukusamehe.
  Na kama unachagua makosa ya kusamehe, basi hata wewe utachaguliwa makosa ya kusamehewa.
   
 12. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #12
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180


  Umezungumzia galfriend hivyo ni kua wewe ni mkaka... Wanawake tukipenda kweli
  hua hamna kitu tunapenda kama huyo tuliempenda atujali 24/7.. Sio kwamba awe hapo...
  ila kwamba wakati wowote unapomhitaji au una shida... yupo... kitendo cha Galfrnd kuchukia
  wewe kumtafuta thru rafiki proves kua kuna kitu anaficha, na ni kwamba anapoka hapatikani
  sio bahati mbaya bali hataki... na kama kafika that stage hakupendi, yupo nawe kwa
  sababu ya vigezo vingine...

  Alikugombeza... ukamgombeza na ukaomba msamaha... ulikua huna sababu ya kuendelea kujishusha
  mno... ilitakiwa umwambie wazi kua kweli umekosea ila hata wewe hujapenda tabia yake na
  atoe sababu kwa nini akwazike kiasi hicho hali ulikua una was juu yake... Pole Saaana.
   
 13. CPU

  CPU JF Gold Member

  #13
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Nimegundua kuna watu wana nature ya KUTOSAMEHE
   
 14. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
   
 15. CPU

  CPU JF Gold Member

  #15
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  Mkuu
  Acha msamaha wa kweli utoke moyoni mwake, kama kumbembeleza na kumuelewesha naona umefanya vya kutosha.
  Ni wazi anaonekana hawezi kukusamehe.
  Na utajiingiza matatizoni ukimlazimisha akusamehe, atatumia mwanya huo kukushika masikio
   
 16. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  kuna baadhi ya watu hasa wanawake
  ukiomba msamaha tu,umeumia....
  anakuona soft hivi au b.w.e.ge hivi...

  ndo maana sometimes kesi ndogo unaziacha zinapita tu
  unatoa space shetani apite kuliko kukimbilia kuomba msamaha...
   
 17. CPU

  CPU JF Gold Member

  #17
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135

  When a woman . . . . .
  Thanx
   
 18. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #18
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  As much as umesema baadhi... ebu Boss wanaume wangapi wanaomba msamaha? wachache mno...
   
 19. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #19
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180

  AshaDii is humbled...
   
 20. CPU

  CPU JF Gold Member

  #20
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Mkuu
  Ashadii kavua gamba hapo juu
  Hebu soma sababu alizozitoa hapo juu wanawake kutosamheme, wakati by nature mwanamke ni alama ya upendo na huruma
   
Loading...