Hivi kuna mtu alishawahi kuwa na uhusiano na kiumbe jini

The Eric

JF-Expert Member
Feb 23, 2019
5,053
8,140
Salaam wote!

Nimeaona sio vibaya nikawashirikisha hili wakuu daah, maisha ya duniani kama huyajui unaweza dhania unayajua kumbe kuna vingi vitu huvijui.

hata ule chumvi nyingi lakini vipo bado vingi hutakuwa huvifahamu.

Hawa viumbe tunawasikia wanaitwa majini wapo lakini mara nyingi hawaonekani na huwa wapo kwenye mazingira yetu. Ikumbukwe jini huweza kuwavaa hata binadamu bila yeye kujua.

Binafsi nilikuwa mazingira fulani ya shamba ambapo kuna ukimya na hakuna movement wala mimea mingi, basi nikanotisi harafu ya marashi makali sana ya kike hii ilitokea siku mbili zilizopita nyuma na jana tena yametokea.

Hivi Swali langu wakuu kwa nini Jini linapenda kufuata binadamu, kuna jamaa mmoja alisema ukiwa msafi sana jini huwa linatabia hizo, na pia ukiwa na mahusiano yanayosumbua afu jini likaamua kukupenda kuliko anayekusumbua pia hukufuata. (Ikumbukwe Kuna majini wazuri na wabaya).

Majini wengine wanabana au kuziba hadi riziki na wengine pia huwa na neema sema watakupa masharti.

Mawazo yenu wakuu hii hali inatokea sana.
 
Salaam wote!!....

Nimeaona sio vibaya nikawashirikisha hili wakuu daah, maisha ya duniani kama huyajui unaweza dhania unayajua kumbe kuna vingi vitu huvijui.

hata ule chumvi nyingi lakini vipo bado vingi hutakuwa huvifahamu.

Hawa viumbe tunawasikia wanaitwa majini wapo lakini mara nyingi hawaonekani na huwa wapo kwenye mazingira yetu....ikumbukwe jini huweza kuwavaa hata binadamu bila yeye kujua.

Binafsi nilikuwa mazingira fulani ya shamba ambapo kuna ukimya na hakuna movement wala mimea mingi, basi nikanotisi harafu ya marashi makali sana ya kike hii ilitokea siku mbili zilizopita nyuma na jana tena yametokea.

Hivi Swali langu wakuu kwa nini Jini linapenda kufuata binadamu, kuna jamaa mmoja alisema ukiwa msafi sana jini huwa linatabia hizo, na pia ukiwa na mahusiano yanayosumbua afu jini likaamua kukupenda kuliko anayekusumbua pia hukufuata. (Ikumbukwe Kuna majini wazuri na wabaya).

Majini wengine wanabana au kuziba hadi riziki na wengine pia huwa na neema sema watakupa masharti.

Mawazo yenu wakuu hii hali inatokea sana.
Wa hiyo wewe unatamani ukutane na jini?
 
Majini ni malaika waasi kwa Mungu. Ni roho, kwa mujibu wa Biblia majini ni wawakilishi wa shetani, shetani hana lolote jema kwa mwanadamu, shetani akikupa kitu na mkono wa kulia anachukua kitu ndani yako kwa mkono wake wa kushoto.

Anaweza kukupa pesa na vitu vingine unavyo tamani lakini hawezi kukupa amani, amani ni kila kitu kwa mwanadamu, Bora ukose vyote lkn uwe na amani kwakua hata pesa tunazitafuta ili tuwe na amani. Mwisho wa uhusiano wowote na majini ni mauti na moto wa milele jehanamu. Mpokee Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yako, naye atakupumzisha mizigo yako
 
Kwa imani yabgu hakuna majini wazuri. Majini wana nia ya kuaharibu siju zote. Unaweza dhan anajupenda pindi akupapo vitu flan ila vyote akupavyo utarudisha zaidi ulivyo polea. Shetan hajawahi kumwazia mtu mazuri hata siku moja

Epuka kujiunganisha na mashetani/majini kwa namna yoyote
 
Hakuna cha majini wala nini,,huko porini kina miti yenye maua,,wanyama,,wadudu,,majani ya aina mbalimbali na wana harufu tofauti tofauti kuanzia hiyo mimea hadi wadudu na wanyama,,,unaweza kuta hayo ni marashi ya mmea/maua kwa kuwa umshekalilishwa ukisikia harufu porini ni majini basi na wewe akili ikakupuleka huko!!!
 
Mtoa mada wewe mwenyewe ni jini au wakala wa majini?

Mbona kama unawapigia promo majini?

Hakuna jini mwema, na kama yupo -kwa mujibu wa imani yako- basi hawezi kuwa na mahusiano na mwanadamu, yeye mwenyewe atakua na issue zake na familia yake kama za kwako, hawezi kukufuatilia wewe.
 
Waulize wale wanaosali nao pamoja yaani dini Moja. Waulize wale wanaongea na kutandika lugha Moja ya kuanzia nyuma, waulize wale ambao kwao hawakubaliani na Mungu kuwa majini yote yalikuwa ni kati ya uzao malaika walio hadi na kulaaniwa kuwa mashetani
 
Majini ni malaika waasi kwa Mungu. Ni roho, kwa mujibu wa Biblia majini ni wawakilishi wa shetani, shetani hana lolote jema kwa mwanadamu, shetani akikupa kitu na mkono wa kulia anachukua kitu ndani yako kwa mkono wake wa kushoto. Anaweza kukupa pesa na vitu vingine unavyo tamani lakini hawezi kukupa amani, amani ni kila kitu kwa mwanadamu, Bora ukose vyote lkn uwe na amani kwakua hata pesa tunazitafuta ili tuwe na amani. Mwisho wa uhusiano wowote na majini ni mauti na moto wa milele jehanamu. Mpokee Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yako, naye atakupumzisha mizigo yako
Malaika Hana sifa ya kumuasi mungu,
Jini na Malaika ni viumbe viwili tofauti
 
Nasubiri wataalamu wa majini na wale wa tiba za kisuna na wasoma visomo waje hapa watupe darasa kidogo.
Maana wengi hapa walokole afu sipati chemistry yoyote.
 
Kwa imani yangu, majini ndiyo wa kwanza kuumbwa kabla binadamu na wameishi duniani miaka mingi kabla ya mtu. Uwepo wa wema ndiyo wapo na wala hawana muda na wewe na kujitokeza mbele yake, wao wana maisha na kufuata ya kwao. Ukiona jini anakuja kwenye maisha yao na kukwambia kitu fulani mara fanya hiki na kile, jua huyo si mwema hata kidogo ni miongoni mwa waovu.

Majini wapo sehemu mbalimbali hadi ya nyumba zetu tunazoishi, ndiyo maana kwenye dini yetu inaamriwa mabinti waache tabia ya kujiweka uchi ndani na kwenda kujiangalia kwenye kioo. Nao wanatamani kama wengine, na ndiyo mwanzo wa kuanza kuingiliwa na jini. Majini wa ndani ya nyumba huitwa Amirul bayt, na wengi wao wanakuja kuwa majini mahaba kutokana na tabia za dada zetu vyumbani.

Elewa jini mwema hana muda na wewe na hata kujitokeza kwenye maisha yako, wana mambo yao na familia zao
 
Majini ni malaika waasi kwa Mungu. Ni roho, kwa mujibu wa Biblia majini ni wawakilishi wa shetani, shetani hana lolote jema kwa mwanadamu, shetani akikupa kitu na mkono wa kulia anachukua kitu ndani yako kwa mkono wake wa kushoto. Anaweza kukupa pesa na vitu vingine unavyo tamani lakini hawezi kukupa amani, amani ni kila kitu kwa mwanadamu, Bora ukose vyote lkn uwe na amani kwakua hata pesa tunazitafuta ili tuwe na amani. Mwisho wa uhusiano wowote na majini ni mauti na moto wa milele jehanamu. Mpokee Yesu awe Bwana na mwokozi wa maisha yako, naye atakupumzisha mizigo yako
Una uhakika mkuu kuwa shetani si lolote au unaongea tu.

Kwa taarifa yako ulimwengu wetu huu ni mali ya shetani wakiwemo na viumbe wote waishio ndani yake kwa sababu shetani alitupwa huku duniani akapewa milk ya ulimwe gu huu.

Na hata yesu wakati akijalibiwa mlimani shetani alimwambia tazama milki hii nitakupa ukinisujudia.
Hivo kwa akili ya haraka tu wanaomwabudu shetani wana mafanikio makubwa s ana kuliko wanaomwabudu mungu
 
Malaika Hana sifa ya kumuasi mungu,
Jini na Malaika ni viumbe viwili tofauti
Mungu hakumuumba shetani, alimuumba lusifa lakini alipokuwa muasi akaitwa shetani
Shetani mwenyewe alikuwa malaika muasi lakini alikuwa na cheo kikubwa, majini na mapepo na miungu ya jamii fulani ni malaika wadogo×2 ambao walitupwa pamoja na lusifa wakati walipoasi... That's what I know according to the Bible, unaweza kuwa sahihi pengine according to the source of your understanding
 
Una uhakika mkuu kuwa shetani si lolote au unaongea tu.
Kwa taarifa yako ulimwengu wetu huu ni mali ya shetani wakiwemo na viumbe wote waishio ndani yake kwa sababu shetani alitupwa huku duniani akapewa milk ya ulimwe gu huu.
Na hata yesu wakati akijalibiwa mlimani shetani alimwambia tazama milki hii nitakupa ukinisujudia.
Hivo kwa akili ya haraka tu wanaomwabudu shetani wana mafanikio makubwa s ana kuliko wanaomwabudu mungu
Unasema wanao abudu shetani wanamafanikuo kuliko wanao mwabudu Mungu... Wengi wanapotoshwa na vitu vya kuonekana pesa, magari, majumba n.k lakini huo unaweza kuwa mtazamo kuhusu maana ya mafanikio. Mafanikio makubwa duniani nikuwa na amani, unaumwa lakini una amani, una maumivu lakini amani haiondoki. Kama unafikiri shetani anawafanikisha watu kwanini kilasiku wanamkimbia na kujutia kujiunga nae? Kuna mtu mwenye akili anaweza kukimbia mafanikio?
Yesu aliwahi kuuliza "...unafaidika nini ukiupata ulimwengu mzima lakini ukaipoteza roho yako?" Au huku duniani utaishi milele?
 
Mungu hakumuumba shetani, alimuumba lusifa lakini alipokuwa muasi akaitwa shetani
Shetani mwenyewe alikuwa malaika muasi lakini alikuwa na cheo kikubwa, majini na mapepo na miungu ya jamii fulani ni malaika wadogo×2 ambao walitupwa pamoja na lusifa wakati walipoasi... That's what I know according to the Bible, unaweza kuwa sahihi pengine according to the source of your understanding
"Shetani ni jini ila si kila jini ni shetani"

Majini kuna wachavu na waovu ambao wanafanya mabaya mengi sana na hata kushawishi wanadamu waingie kwenye maasi, hawa wanaitwa mashetani. Ni kosa kubwa kumwita shetani jini ambaye hana sifa hizo, yupo zake kwenye makazi yao akiendelea na maisha ya kila siku pasipo kufanya machafu.

Unayemwita Lusifa ni jini kama majini wengine ambaye ameamua kuasi na kufanya yasiyompendeza Mungu ndiyo maana wanamwita Shetani.
 
Back
Top Bottom