Hivi kosa langu ni nini katika haya yote?

Hivi kosa langu ni nini katika haya yote?

Ndio unakosa kwa kuchepuka.
Ukizingatia hukuwahi kuthibitisha kuwa mkeo anachepuka.....what if ilibidi "afundishe tuition" nyingi ili kupata fedha zA kuwasaidia? ?????
 
Wanawake kama hawa ndio wanatufanya wanawake wote tuonekane tunapenda hela tu. Jamani kile kiapo cha shida na raha ni shida na raha kweli sio kwenye shida unakwepa...ndio matokeo hayaaa.....
Back to topic

Mariana.......


......nitakuja kuendelea....

Kumbe ndio wewe........jamaa anatangaza ndoa hapa
 
Usimuache kama Muislam muoe huyo mwengine mfanye awaubari watoto wako na usikihe kilimo...
Wakabahau
 
Mpwa hizo nguvu zote hizo unazozitumia kulumbana na kugombana nae huku ukimhudumia Mariana LAITI ungeendelea kuziwekeza kwenye huo mradi wa KILIMO ungekuwa mbali sana zaidi ya hapo ulipo. Leo hii badala ya kupost kitu kama hiki ungepost kuhusu mafanikio yako na jinsi tunavyoweza kujifunza kutoka kwako.

You must grow in mind and healthy sio umri tu, hivyo vita ulivyoviendeleza havina mshindi zaidi ya kujiongezea stress na kupunguza concentration kwenye ujasiliamali wako. Mwanzoni ulifikia 19m kwasababu you invested most of your time kwenye hio agribusiness, sasa hivi umei-cut off hio nguvu kwasababu nusu au pengine robo tatu yake inafikiria jinsi ya kumkomoa huyo Mama.

As you Mom said, msamehe muendelee mbele, basi kama hayasameheki basi suiyakuze yaache yabaki hivyo hivyo, hii ndio busara ya Mpwao Elli

Mwanangu Elli (mtoto wangu mmoja anaitwa Elli...) upo sahihi kabisa.Chukua LIKE ya maandishi.
Hivyo vita si kutokuwa na mshindi tu,bali anatengeneza matatizo mengine mawili ama zaidi katika jamii.
Kwanza hiyo dhambi aliyoilipiza kuna uwezekano mkubwa wa kuja kujirudia tena kwa Mariana kumcheat,na pili ni kwa watoto amabao hawatayapata malezi ya baba na mama kwa pamoja,kitu kitakachopelekea kuharibikiwa kwa watoto kisaikolojia.
Cha kufanya ni kuachana na Mariana,then unakaa chini na mkeo,mnaangalia wapi mlikosea na kuombana msamaha,then mnaendelea kujenga taifa na kujenga familia bora kwa amani na upendo.Kinyume na hapo mkuu,hakuna familia bora wala watoto watakaokuwa bora katika jamii.
 
Last edited by a moderator:
Kwahiyo umempiga "Muosha huowoshwa" ndio anaanza kulia lia
sasa hapo jambo ni moja tu...wewe andaa mazingira mazuri
ya watoto wako kisha fanya maamuzi , kwanini uishi na kidonda ndugu
kila siku ili hali ukijua hakiwezi kupona even by hooks or crooks ...??
 
umeshajiuliza mariana kakupendea nini??? usikute ni bora hata mwalimu kavumilia for some years
 
kumpata mariana sio suluhisho huyo naye umempata kwa kuwa una hela ukipata tena ajali na huyo atakufanyia yaleyale ushauri wangu somesha wanao na kuwatunza sana ila swala la ndoa saivi achana nalo coz huyo mkeo mpya anaweza kuja kukutesea wanao sana
 
Hujui kosa lako ni nini? Kwa hiyo mwenzako akikojoa wewe ndio unakunya kabisa? Wakati unafunga ndoa uliapa nini mbele za Mungu na leo wewe unafanya nini? Hayo unayoyafanya sasa hivi na unayotaka kuyafanya ndio fadhila na shukrani unayotaka kumrudishia Mungu kwa kukujalia kupata shughuli ya kukuingizia kipato?

Majibu ya maswali hayo yatakueleza kosa lako liko wapi.
 
Thank you tuko na mtazamo ulio sawa kabisa, hatuko kwenye enzi za kuendekeza mambo ambayo yanatupa stress tu
Mwanangu Elli (mtoto wangu mmoja anaitwa Elli...) upo sahihi kabisa.Chukua LIKE ya maandishi.
Hivyo vita si kutokuwa na mshindi tu,bali anatengeneza matatizo mengine mawili ama zaidi katika jamii.
Kwanza hiyo dhambi aliyoilipiza kuna uwezekano mkubwa wa kuja kujirudia tena kwa Mariana kumcheat,na pili ni kwa watoto amabao hawatayapata malezi ya baba na mama kwa pamoja,kitu kitakachopelekea kuharibikiwa kwa watoto kisaikolojia.
Cha kufanya ni kuachana na Mariana,then unakaa chini na mkeo,mnaangalia wapi mlikosea na kuombana msamaha,then mnaendelea kujenga taifa na kujenga familia bora kwa amani na upendo.Kinyume na hapo mkuu,hakuna familia bora wala watoto watakaokuwa bora katika jamii.
 
"mwanamke akuzidi kila kitu ila sio kipato"
Wako mtiifu mwanamke
Evelyn Salt
 
Aiseeeee! Namna hii? Mungu atusaidie mabachalor wenye nia na ndoa!
 
Mungu anisaidie nikiwa na kazi siku akifukuzwa au akiumizwa tu na chochote na kushinda kuendelea na kazi nyumba yangu itageuka mbingu.. Nitampenda na kumjaki km my tito boy( yy sintomgombeza maana toto boy lazma nimkanye kwa kafimbo kadogo tabia zake za kupiga wengine,) I Love my husband... Mungu tupe maisha marefu waja wako..
 
Habari zenu
Naomba msipate tabu na neno Dr kwenye ID yangu, ni jina tu

Mwaka 2005 nilipata ajali mbaya ya Gari nikiwa safarini kikazi, nilivunjika sehemu mbali mbali za mwili, nilikaa muhimbili karibu mwaka mzima, shirika nililivunja mkataba na mm walini terminate baada ya kujiridhisha kwa vigezo vyao kuwa siwezi kumudu tena kazi, nikapewa malipo yangu yote, hayakua makubwa sana, maana nilianza kazi 1999, pia nilikua na mkopo nilichukua kujengea nyumba, walitumia mafao yangu kulipia huo mkopo, nilibaki na kiasi kidogo sana cha fedha

Mke ni mwalimu wa sekondari, na tulikua na watoto wawili hadi hapo napoteza ajira, mkubwa miaka 4 na mdogo mwaka mmoja, ilipofika 2008 nilikua nimepona kabisa, watu walionizunguka hawakuamin kabisa muujiza huo, changamoto iliyonikabili baada ya kupona ni kukosa kazi, nilihangaika bila mafanikio nikipanda ghorofa kwa ghorofa na vyeti vyangu

Wife akaanza visa, kwamba nimekuvumilia na kukulisha tangu 2005 ulipopata ajali, sasa umepona siwezi kukulisha tena, kama hupati kazi hilo sio tatizo langu, nenda hata kabebe zege au kasukume toroli ulete matumizi""
Nilishangaa sana kwa Maneno Yale, maana alijua wazi sikua naruhusiwa kubeba vitu vizito,
2010 nilikua bado sijafanikiwa kupata kazi, wife akaanza kurudi usiku mwingi, akiwa kanywa pombe, na akifika hataki kuguswa, tulikua tunakutana pale anapotaka yeye tu, weekend mzima hashindi nyumbani, kwa kifupi dharau zilikua nyingi mno, lakini nilivumilia, nikasema ipo siku mungu ataniinua tena

2011 nilipata msaada kutoka kwa shemeji yangu alieoa Dada yangu tumbo moja, yeye ni mkulima wa kati siku nyingi, analima mchele na mahindi sengerema vijijini, akanipigia simu niende sengerema ana mazungumzo na mm, kumbe mama yangu alishakwenda kumuona mwezi nyuma na kumuomba anisaidie
Alinigawia sehemu kubwa ya kulima kama heka nne hivi, alinipa mtaji wa kilimo milioni 5 yy ndie aliesimamia zoezi la kulima heka hizo, kusia mbegu, na kupanda, na kuwalipa watenda kazi yy mwenyewe, nilikaa huko shambani miezi mitatu, nilimficha wife kuhusu suala hilo

Alikua tu anashangaa mwezi huu nipo, ujao sipo dar, hivyo hivyo hadi nilipovuna na kuuza, awamu ya kwanza nilipata 13m nilizirudisha zote kwenye kilimo msimu uliofuata, na awamu ya pili nikapata 19 milioni, nimeendelea hivyo hadi sasa napata pesa za kuridhisha, hiyo ni kutoka 2011 hadi sasa, 2015, kwa kipindi chote hiki nime pretend kuishi kama vile sina kitu, ila matumizi ndani natoa na nikawa nalipa shuleni kwa watoto ada,

Mwaka huu, nimefanya makubwa zaidi, nimeizungushia nyumba ukuta na Geti, nimetoa nyavu na kuweka aluminium glass, nimenunua Gari ndogo na mengine mengi, nimetafuta msichana mzuri pembeni ( Mariana) mwenye adabu na Upendo, siogopi kutaja jina lake maana sio siri

Wana Jf kwa kawaida Dereva mzuri ni lazima arudi reverse, ataendesha wee lakini kuna pahala atalazimika kurudi reverse, sasa wife, ghafla bin vuu ameanza kuona wivu, kwamba mbona unarudi saa saba usiku unatoka wapi,!! Anaanzisha fujo usiku kucha, kesho yake mm narudi alfajiri kabisa au nalala huko huko kwa mariana , naondoka Friday narudi Sunday namkuta analia kama mtoto mdogo, nawapakia watoto wangu garini nawapeleka beach jioni tunarudi wakiwa wamefurahi

Ametafuta namba ya Mariana kwenye simu yangu hadi akaipata, sasa hivi anamtukana na kwenda kumfanyia fujo kila siku, weekend iliyokwisha nimeitwa kwenye kikao cha usuluhisho, baada ya wife kwenda kushtaki kwa wazee wake, huko nyuma wakati akinisumbua niliwahi kushitaki kwao walikua wakinipuuza, sasa juzi nimewajibu its pay back time, nikaondoka

Nataka kumuondoa kwangu niachane nae kabisa nilete Mariana ndani, watoto nitabaki nao, kama atangangania kugawana Mali nipo tayari kumuachia nyumba na watoto kama atataka, nitaenda kupanga huku nikimalizia nyumba yangu nyingine iliyopo kwenye linta,

Ingawa mama yangu mzazi ameniomba kumsamehe lakini sioni kama hilo linawezekana, amenitendea mambo mabaya sana ikiwemo infidelity ambayo kwa vyovyote ilifanyika kutokana na ushahidi wa kimazingira, sikutaka kumfumania wala kumfuatilia niliogopa kuumia zaidi moyoni, huwa sina kifua hicho

Wana Jf naomba kuwauliza katika yote Haya kosa langu ni nini hasa?
Nina kosa lolote hapo?

Naombeni mnisaidie

Mkuu mimi sijakuona na kosa, hata mimi ningefanya hivyo hivyo ulivyopanga kifanya.
 
Kama ni kweli hayo yote uliyosema basi huna kosa. Msalimie Mariana!!
 
Ndo maana nimeweka uzi kuwa SITAOA humu ndani.Haya mambo ndo tatizo.FUKUZAAAAA oa Mariana
 
Kosa lako ni kwenda kwa Mariana ukifikiri ndo suluhisho...hicho ulichopata kitaishia kwa Mariana yy hatakusaidia hata kidogo.ukiona mwanamke Yuko na ww na anajua ww ni mume wa MTU ujue kafata pesa tu hapo na zikiisha ataenda kwa mwingine mwenye nazo. Msamehe mkeo mlee watoto katika maadili mema.
 
Back
Top Bottom