ZLATAN
Senior Member
- Oct 5, 2010
- 150
- 18
Nakumbuka nyumba ya jirani kulikua na watoto watatu baba yao alikua na uwezo kifedha wilayani kwetu lakini pia alikua mkoloni sana. Kwao hawa watoto kukutwa na pesa lilikua ni kosa la jinai linaloadhibiwa kwa bakora lukuki.
Siku moja hawa jamaa zangu wakawa wameiba pesa ndani kwao hivo wakawa wamejaa pesa mfukoni. Jioni ilipofika wakaenda kununua samaki waliokaangwa kwa mama mmoja aliyeitwa mama khalidi. Huyu mama alikua ni jirani yao. Bahati mbaya huyu mama hawakumkuta kwani alikuwa amekwisha ondoka kuwapeleka samaki eneo la biashara ambapo ni mbali kidogo na nyumbani kwake.
Basi jamaa zangu kwa kuhofia kuchelewa nyumbani na kufika kabla ya baba yao hajawasili kutoka kazini wakarejea nyumbani mikono mitupu bila samaki. Mida ya saa mbili usiku baba yao akawa amekwisharejea nyumbani. Huku nyuma mama muuza samaki nae akawa amerejea kwake na akawa amebakiza samaki nadhani biashara haikuwa nzuri. Wanae wakamwambia kina flani walikuja nunua samaki hawakukukuta. Mama wa watu akajua dili hili siliachii. Si akabeba sinia la samaki hadi kwao na jamaa zangu. Kufika akabisha hodi, mmoja wa jamaa zangu akaenda kufungua mlango. Kugundua aliyepo mlangoni ni mama wa samaki akafunga mlango haraka haraka akijua mama kawaletea noma. Baba yake akauliza kwa nini kafunga mlango ilihali aliyebisha hodi hajaonana na wakubwa (yaani baba ama mama yao jamaa zangu). Akamuliwa afungue mlango mgeni aingie. Mlango ukafunguliwa mama wa samaki na sinia lake kaingia ndani.
Mama wa samaki akaeleza shida yake kuwa kapata taarifa samaki walihitajika wakati yeye akiwa biasharani. baba wa jamaa zangu akaitikia kinafiki ati ni kweli na akawahimiza wanae wanunue wale samaki kwa bashasha na unafiki mkubwa.
Baada ya biashara mama wa samaki huyooo akaondoka zake. Huku nyuma baba wa jamaa zangu akaenda kukata bakora akawahimiza wanae wawatafune wale samaki huku akitaka maelezo pesa ya kununua samaki ilitoka wapi. Jamaa zangu wakawa wazito kula wale samaki. Basi mzee akaanza kuwatembezea bakora kwanza za kuwahimiza kula wale samaki. Jamaa zangu wakawa wanakula wale samaki huku wakilia na wakati huo huo yule baba yao akiwa nje anaanda mzigo wa bakora huku akifoka "leo mtanitambua si nilishawakataza kuwa na pesa leo mtanitambua".
Jamaa zangu huku wakilia wakatafuna wale samaki lakini wakati huo huo mvua za bakora zikiwanyeshea kuwahimiza waongeze kasi ya kula wale samaki.
Aisee baada ya zoezi la kula wale samaki lilipokwisha baba yao aliwashushia bakora za kutosha sana kama adhabu ya kukiuka amri yake ya kutokukutwa na pesa mfukoni.
Ni kituko kilichofanywa na jamaa zangu lakini hunichekesha sana kila nikikikumbuka ama tukumbushanapo pindi nionanapo na mmoja wa hawa jamaa zangu.
Hahahaaaaaaa kwa kweli mkuu hapa nimecheka mpaka kunyanzi zimejaa usoni.. Madingi wakoloni ni noma. Hahahaaaaaaaaaaaaaaaaa kwikwikwiiiiiiiii uuuuhhhhhhiiiiiiii....