Hivi kituko gani unakikumbuka ulikifanya wakati mdogo

Nilipokua mdogo nilikua nasumbuliwa sana na kifua. Sasa cku moja nikamsikia bro akisema dawa ya kifua ni pombe kali. Nakumbuka cku moja ya xmas kifua kilikua kinakwaruza, mi nikaingia room kwa dingi kulikua na chupa ya whisky nikaanza kuinywa! Muda huo ndugu zangu walikua wako huko nje wanapiga stori. Basi ili nisikamatwe nikafunga mlango wa nje kwa ndani nikaendelea kujimiminia kilaji. Si nikalewa nikaishia usingizini! Unaambiwa cku hiyo watu wote walilala nje! Gonga mlango.. Wapi! Duh..

Du, huenda dingiyo alikuwa na mahamu na mkewe, kaharibu ladha yote.
 
Mimi nakumbuka wakati mdogo nipo darasa la nne (4) nilienda jikoni nikaiba mandazi matatu nikapanda kitandani ili nile yale mandazi huku nimejilaza kitandani usingizi ukanipitia. asubuhi Mother kuingia chumbani kayakuta mandazi yamesambaa kitandani mimi nimelala. nilichezea bakora sana...endeleza na wewe kituko chako cha utotoni

ChatuDume hii thread uliyoanzisha ....chichemi lakini wanaochangia wamenikenulisha kweli kwa vitukao vyao. Sasa wale majuha wataanza kuchangia ush*** wao!!!
 
Mie nakumbuka, nikiwa darasa la tano, wakati huo kwa kweli nilikuwa najua kuchora sio siri. Basi asubuhi moja wakati ule wa watu kufanya usafi kabla ya kwenda mstarini, nikaenda kwenye chumba cha darasa la sita, nikachukua chaki na kumchora Madenge (yule wa gazeti la Sani) ubaoni. Nilimpatia ile mbaya. Si sikumfuta. Nikaenda zangu. Mwalimu alipoingia kufundisha darasa hilo akaikuta ile picha ubaoni, kuuliza wale wanafunzi nani kachora, kuna waliokuwepo wakati naichora, wakanitaja. Nikaitwa ofisini nikalamba mikwaju ya haja!
 
Nakumbuka darasa la 6 nliokota sh 45000,then wakati naendlea mbele akaja mtu wa makamo akaniuliuza kwa huruma sana kama nimeokota bahasha yenye hela njia ilikuwa hapiti watu wengi sana.nkampa alinipa sh 10000.nakuniaeba kwenye baiskeli hadi home
 
Nakumbuka darasa la 6 nliokota sh 45000,then wakati naendlea mbele akaja mtu wa makamo akaniuliuza kwa huruma sana kama nimeokota bahasha yenye hela njia ilikuwa hapiti watu wengi sana.nkampa alinipa sh 10000.nakuniaeba kwenye baiskeli hadi home
ya kweli hayo!??
 
duh! mimi sjawahi kuwa mtoto lakini story zenu nzuri hata ivyo sana sana ya Viksi
 
Mimi sikumbuki nilikuwa na umri gani wakati huo. Kuna mtoto mwenzangu wa jirani (wa kike na mimi wa kiume) tulikuwa tunacheza naye. Sasa ikafika wakati wote tukaenda kukojoa, yeye akachuchumaa na mimi nikasimama wakati nakojoa. Sasa nikaanza kumshangaa mbona wewe umekaa badala ya kusimama? Ikabidi niende kumchungulia nikaona hana dudu kama yangu, yeye ni kitobo tu, niliingiza hadi kidole kwa kushangaa.

Then nikakimbia nyumbani kwenda kumwelezea mama yangu, nikamkuta nyumbani yuko na wamama wengine wa jirani nikaanza kuelezea "Eti mama nimeona kikojoleo cha fulani ni kitobo tu hana dudu kama yangu, tena nimeingiza kidole ni kishimo tu kipo ,,,,," kabla hata sijamalizia nilechezea kichapo oho!! sijawahi kusahau hadi leo.
 
Enzi hizo tunduma primary school,wavulana tulikuwa na tabia tukiwa parade,tunaweka vioo chini ya wasichana waliosimama mbele yetu,then una check still picture ya private zake..Basi baadaye demu akikuzingua,unampa makavu,'c**pi yako ya kijani,afu umeifunga na pini.Siku moja waliamua kutushtaki kwa walimu,wavulana shule nzima except dara la(1&2) tulichakazwa bakora zisizo na idadi.
 
nakumbuka nilikua kama na miaka sita hivi, tulikua wengi tu home, shangazi ifikapo likizo hua anapita kwa kaka zake wote na kuzoa watoto .. so kwa idadi na watoto wake tukawa kama tisa hivi .. sasa siku moja alitembelewa na wageni wake .. kama sita hivi .. wakawa sebuleni wanaongea .. time ya chakula nakumbuka mama wa kazi (maana ni mfanyakazi lakini mama wa makamu) akatupakulia wali na nyama kila mmoja na sahani yake tukamkatalia tukataka tule wote kwenye sinia moja .. kelele zilivyozidi shangazi akamwambia afayanye tunavyotaka sisi .. .so akatuwekea kwenye sinia ... zile vujo na nini tukaanza kunyanganyana nyama .. kelele za nyama yangu zikawa nyingi .. duh shangazi akapata aibu ya mwaka .. akaja akaondoa ile sinia akatuamrisha kila mmoja wetu apande kitandani alale .. kimya .. tukafanya hivyo .. wageni walivyoondoka .. shangazi
kaondoka akaleta kilo ishirini za steki wakachemsha kimya kimya sisi tumefungiwa chumbani .. walivyoivisha tukaamshwa sote .. shangazi kashika wire wa radio .. tukaamrishwa kuanza kula .. tukafikia wakati tumeshiba tuko hoi .. mpaka tukatamka tumekoma .. baada ya hapo viboko vikafuata mpaka tukavimba miili
 
Nilikua nalazimishwa kula,nikaanza kufikiri labda mamdogo na maza ni aliens wanataka ninenepe wanile. Nikafkiri wanakua aliens kama siwaoni,nikigeuka tu wanakua na sura zao za kawaida.Kila nikijaribu kugeuka fasta nakuta sio aliens.Ilikua kazi!Mamdogo akaita mchungaji niombewe mana alihisi nina tatizo. Lol!
 
mie nakumbuka nikiwa na miaka minne nilimshikia kisu mama yangu wa kambo na kumuambia kuwa leo nakuua umezoea sana kunionea basi alikimbia huyo kwa kuogopa kisu,mdingi alivyorudi kazini nadhani mnajua nini kilitokea
 
mie nakumbuka nikiwa na miaka minne nilimshikia kisu mama yangu wa kambo na kumuambia kuwa leo nakuua umezoea sana kunionea basi alikimbia huyo kwa kuogopa kisu,mdingi alivyorudi kazini nadhani mnajua nini kilitokea

mhhmmm...mkuuu 4 yrs????? we like your story anyway..
 
Nimekumbuka maisha ya utotoni mpaka roho inauma yalivyokuwa mazuri, nakumbuka Father akitoka job anakuja nyumbani na Magazeti, ya Mfanyakazi, Uhuru na Mzalendo basi mimi nilikuwa nakata zile picha za wacheza mpira naenda kubandika chumbani kwetu, yaani ukiingia chumbani picha kibao, nilikuwa na picha ya Kajole, Peter Tino, Omar Husein, Zamoyoni Mogela, Marota Soma, Zuberi Magoa, Athuman Chama, wengi tu, alafu nilikuwa na picha ya kuchora mtu kapanda juu ya mti juu kuna Nyoka nchi kuna Simba balaa hiyo picha nilikuwa naipenda sana
 
Nakumbuka wakati nipo darasa la pili kuna mwanafunzi mwenzangu msichana(yeye alikuwa na mwili mkubwa)tuliyekuwa tukiishi nae mtaa mmoja nilimwazima penseli yangu na hakunirudishia. Ikawa kila ninapowaona wadogo zake wanapita karibu na kwetu niliwazuia njia na kuwadai penseli yangu.kumbe kile kitendo kilimuuma dada yao, na akapanga siku ya kufunga shule wanipige yeye na rafiki yake. Ilipofika siku ya kufunga shule bahati nzuri msamaria mwema alinitonya kuwa amesikia kuwa siku hiyo wamepanga wanipige sawasawa.Niliposikia taarifa ya kupokea kipigo nilitoroka shule saa 5 kabla ya mda wa kufunga saa 7 mchana.Na sikuwabughuza tena wadogo wa Yule msichana
 
nakumbuka nilikuwa darasa la tatu nilienda kumtembelea shangazi yangu wakati wa likizo. jioni moja alipika maandazi na akasema hakuna kula tutanywea chai asubuhi, ilipofika usiku mimi na binamu yangu tukapanga kuiba. ilipofika usiku watu wote walikuwa wameshalala, beseni la maandazi liliwekwa juu ya kabati jikoni sasa tukaanza kubebebana ili tuchukue maandazi, mimi nilichuchumaa binamu yangu akawa ananikanyaga mabegani ili apande juu avute lile beseni achukue maandazi, baada ya kuvuta lile beseni mimi huku nilikuwa nimeshachoka nikatikisika kidogo yeye akayumba na kudodosha lile beseni halafu lilikuwa la bati... basi kishindo cha beseni kilisikika nyumba nzima, shangazi akashituka akauliza mnafanya nini?
alipoamka akatukuta tunahangaika kukusanya maandazi.. alichosema tutaonana kesho akaenda kulala...
kilichoendelea asubuhi nyie acheni tu..........

hii imenichekesha mpaka nikasahau kama nna h/work
 
mimi nakumbuka nilchukuliwa na aunt yangu kwa lengo la kunisomesha maana familia yangu ilkua duni walkua matajiri sana lakini baada ya kuhamia kwake cha moto nilikiona maana nilkua house girl wa familia......... nilkua nawapikia watoto wake japo walkua wakubwa kwangu, nawafulia, nafanya usafi nyumba kubwa ya kifahari ikifika saa ya kuosha vyombo napanda juu ya kiti ili nifkie sink maana nlkua mdogo sana ikifika saa ya kula niko hoi hata kula siwezi nasinzia tuuu.....................................

jamani sitamani kuwa mtoto hata kidogo
Pole sana!
 
...nikiwa darasa la pili (mwaka Ninteen Kweusi!), tulikuwa tunatakiwa kwenda shule SAA TANO mchana. Siku hiyo wanafamilia wote walikua wametoka (nilikuwa naishi kwa bibi yangu). Baada ya maandalizi mengine yote sikuweza kuona mafuta ya kupakaa (kupaka?). Ikabidi nipekue ndani ya begi la mama yangu mdogo nikakuta kichupa kidogo cha rangi ya blue/kijani hivi. Nilipofungua nikaona kun amafuta nikapakaa toka kichwani hadi miguuni.

Punde si punde nikaanza kujisikia joto lilichnaganyika na msisimko wa mwili pamoja na harufu nzito. Kwa kuwa nilikuwa nimeshachelewa shule nikatoka vivyo hivyo mbio kwenda shule (kama kilomita moja hivi toka nyumbani). Nilipofika nilikuwa nimesweat kupita kiasi na bado nikisikia joto/msisimko na harufu nisiyoijua. Nilipoingia darasani mwalimu wa somo alikuwa ameshaanza kufundisha. Alipona hali niliyokuwa nayo akanisimamisha akauliza kulikoni? Mimi nikaishia kuomba msamaha kwa kuchelewa kuingia darasani. Akanichukua kunipeleka kwenye bomba la maji la shule kuninawisha-nikaja kuelewa baada ya kumsikia akiongea na walimu wengine kumbe nilikua nimepakaa VICKS KINGO nikidhani ni mafuta ya kupaka!!!
Hii kali!!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom