Hivi kituko gani unakikumbuka ulikifanya wakati mdogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hivi kituko gani unakikumbuka ulikifanya wakati mdogo

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Mshume Kiyate, Apr 9, 2011.

 1. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #1
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mimi nakumbuka wakati mdogo nipo darasa la nne (4) nilienda jikoni nikaiba mandazi matatu nikapanda kitandani ili nile yale mandazi huku nimejilaza kitandani usingizi ukanipitia. asubuhi Mother kuingia chumbani kayakuta mandazi yamesambaa kitandani mimi nimelala. nilichezea bakora sana...endeleza na wewe kituko chako cha utotoni
   
 2. Jaguar

  Jaguar JF-Expert Member

  #2
  Apr 9, 2011
  Joined: Mar 6, 2011
  Messages: 3,409
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Mi nakumbuka enzi zile dingi alikuwa mwalimu mkuu.Basi nilitinga ofisini,dingi sikumkuta,nilipanda kwenye ma shelve ya vitabu na kuvisambaza vyote chini kisha nikaondoka.Alipofika dingi ilikuwa msala kwani aliwaita walimu wote na kuwaweka kitimoto huku aking'aka,'nani aliyekuwa anapekua documents zangu za siri?'.Msala usingeisha kama si mwanafunzi mmoja wa darasa la saba kuja kuelezea ukweli kuhusu ujio wangu ofisini.
   
 3. Capitano

  Capitano JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2011
  Joined: Apr 7, 2011
  Messages: 402
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  Mimi nakumbuka nilipotoka kucheza mchezo wa kibabababa na kimamamama si nikajisahau nikavaa chakatinakati(chu***) ya kabinti nilikokuwa nacheza nako! wakati naoga maza si akanishitukia, wee nilichezea bakora balaa.
   
 4. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,141
  Trophy Points: 280
  mi nilifanya matusi kinguo nguo, niliyefanya naye akaenda kunisemea home,nilichapwa ile mbaya.
   
 5. z

  zayat JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mwalimu wa nidhamu>wewe zayati huwezi kukaa kimya?
  zayati>(mimi) mwalimu nikikaa kimya mdomo unanuka
  nilipigwa bakora assembly
   
 6. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hahahahaa:mimba:
   
 7. L

  Lwikunulo Senior Member

  #7
  Apr 10, 2011
  Joined: Jun 1, 2007
  Messages: 114
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ...nikiwa darasa la pili (mwaka Ninteen Kweusi!), tulikuwa tunatakiwa kwenda shule SAA TANO mchana. Siku hiyo wanafamilia wote walikua wametoka (nilikuwa naishi kwa bibi yangu). Baada ya maandalizi mengine yote sikuweza kuona mafuta ya kupakaa (kupaka?). Ikabidi nipekue ndani ya begi la mama yangu mdogo nikakuta kichupa kidogo cha rangi ya blue/kijani hivi. Nilipofungua nikaona kun amafuta nikapakaa toka kichwani hadi miguuni.

  Punde si punde nikaanza kujisikia joto lilichnaganyika na msisimko wa mwili pamoja na harufu nzito. Kwa kuwa nilikuwa nimeshachelewa shule nikatoka vivyo hivyo mbio kwenda shule (kama kilomita moja hivi toka nyumbani). Nilipofika nilikuwa nimesweat kupita kiasi na bado nikisikia joto/msisimko na harufu nisiyoijua. Nilipoingia darasani mwalimu wa somo alikuwa ameshaanza kufundisha. Alipona hali niliyokuwa nayo akanisimamisha akauliza kulikoni? Mimi nikaishia kuomba msamaha kwa kuchelewa kuingia darasani. Akanichukua kunipeleka kwenye bomba la maji la shule kuninawisha-nikaja kuelewa baada ya kumsikia akiongea na walimu wengine kumbe nilikua nimepakaa VICKS KINGO nikidhani ni mafuta ya kupaka!!!
   
 8. P

  Pokola JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 717
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Mimi nilikuwa mtoto mwenye hila ile mbaya. Tapeli kabisa.

  Nakumbuka nilimhadaa rafiki yangu wa karibu sana nilipokuwa darasa la tatu, jamaa kaenda kumchungulia mwalimu wa kike chooni (Choo cha walimu kilikuwa kimepakana na cha wanafunzi na kutenganishwa na ukuta wenye nafasi kubwa juu). Yule mwalimu alimwona, na siku hiyo ilikuwa kiama kwa rafiki yangu yule.

  Mimi nilikimbia, siku 3 sikukanyaga shule.
   
 9. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #9
  Apr 10, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hahahahaha hapo kwenye blue ndugu yangu mbavu sina:sorry:
   
 10. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #10
  Apr 11, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  nakumbuka nilikuwa darasa la tatu nilienda kumtembelea shangazi yangu wakati wa likizo. jioni moja alipika maandazi na akasema hakuna kula tutanywea chai asubuhi, ilipofika usiku mimi na binamu yangu tukapanga kuiba. ilipofika usiku watu wote walikuwa wameshalala, beseni la maandazi liliwekwa juu ya kabati jikoni sasa tukaanza kubebebana ili tuchukue maandazi, mimi nilichuchumaa binamu yangu akawa ananikanyaga mabegani ili apande juu avute lile beseni achukue maandazi, baada ya kuvuta lile beseni mimi huku nilikuwa nimeshachoka nikatikisika kidogo yeye akayumba na kudodosha lile beseni halafu lilikuwa la bati... basi kishindo cha beseni kilisikika nyumba nzima, shangazi akashituka akauliza mnafanya nini?
  alipoamka akatukuta tunahangaika kukusanya maandazi.. alichosema tutaonana kesho akaenda kulala...
  kilichoendelea asubuhi nyie acheni tu..........
   
 11. s

  sugi JF-Expert Member

  #11
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  nilikuwa nachezea dudu yangu,hapo ilikuwa na fore skin,nikachukua utomvu wa minyaa nikapaka,e bwana asikuambia mtu!dudu ilivimba ikauma vibaya mno,nilikuwa nikikojoa mkojo unakwenda zig zag,acha tu
  siku nyingine nikadokoa nyama jikoni mara sister anatokea c nikaweka mfukoni!natoka nje mara mbwa ananidandia kinoma kanusa harufu ya nyama mfukoni,dah long tym
   
 12. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #12
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kwanza kila aliyepigwa bakora ndiye aliyenifurahisha.
  Mm nipo ktk familia ya kiislam, na ilipokuwa inafika ramadhani watu wanafunga na inapofikia mida ya magharibi WANAFTARI (wanakula/wanafungulia).
  Siku hiyo nikaambiwa njoo UFTARI. Nikaenda, kufika nakutana na watu wanakula muhogo, nikawaambia mm sitaki muhogo nataka FTARI.... Khaaa, mimi nilikuwa najuwa FTARI ni chakula maalum kumbe ina maana ya kula. Siku hiyo hapakutosha kwa kujuwa kuwa wanalificha FTARI lao
   
 13. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #13
  Apr 11, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Ahahaha!! mkuu ilikuwa noma
   
 14. TheChoji

  TheChoji JF-Expert Member

  #14
  Apr 12, 2011
  Joined: Apr 14, 2009
  Messages: 672
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Nilipokua mdogo nilikua nasumbuliwa sana na kifua. Sasa cku moja nikamsikia bro akisema dawa ya kifua ni pombe kali. Nakumbuka cku moja ya xmas kifua kilikua kinakwaruza, mi nikaingia room kwa dingi kulikua na chupa ya whisky nikaanza kuinywa! Muda huo ndugu zangu walikua wako huko nje wanapiga stori. Basi ili nisikamatwe nikafunga mlango wa nje kwa ndani nikaendelea kujimiminia kilaji. Si nikalewa nikaishia usingizini! Unaambiwa cku hiyo watu wote walilala nje! Gonga mlango.. Wapi! Duh..
   
 15. Kaunga

  Kaunga JF-Expert Member

  #15
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 28, 2010
  Messages: 12,591
  Likes Received: 801
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa napenda sana michezo ya utoto, kiasi kwamba kitendo cha kwenda kukojoa naona napoteza muda. So nikaamua, ili kupunguza muda wa kuvua chupi bora niitoboe chupi ili niwe nachuchumaa tu bila kuhangaika kuvua chupi. So nikaunguza chupi moja katikati, ilikuwa ya mpira, ikaanza kuniumiza, ikabidi nitupe chooni!

  That was when I was 4 or 5 yrs old!
   
 16. Tigga Mumba

  Tigga Mumba JF-Expert Member

  #16
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 747
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  mimi nilienda toilet nikakuta hakuna Toilet paper nikatumia majani ya magimbi! Kilichonitokea sitasahau
   
 17. Wa Nyumbani

  Wa Nyumbani JF-Expert Member

  #17
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 432
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Mimi nikiwa darasa la sita nilipendana msichana mmoja lakini hatukuwahi kufanya chochote maana sikujua namna ya kuanza. Siku moja nikiwa na huyo msichana tulikutana na baba yangu ambaye alikuwa hataki watoto tutembee mbali na nyumbani bila sababu. Alinipiga kofi kali sana mbele ya msichana wangu, niliumia, lakini kilichoniliza ni kupigwa mbele ya yule msichana...kesho yake tulipoonana, aliponiona tu alilia sana...du machozi yananilenga...naishia hapa!
   
 18. A

  Aine JF-Expert Member

  #18
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,613
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Yaani leo nimefurahi sana, nimecheka hadi machozi yananitoka jamani utoto una raha yake bwana asikuambie mtu, mimi sikumbuki ni darasa la ngapi, nilikuwa monitor wa darasa sasa kuna mkaka alikuwa mkubwa kuliko wote darasani, alikuwa anapiga kelele sana kwa kujivunia ukubwa wake!nikamuandika kati ya wapiga kelele wa siku hiyo, alipigwa fimbo na mwalimu. Sasa baada ya kutoka darasani, kuna kijana mwingine akawa ananichongea ili yule niliyemuandika anipige, mwenyewe akawa hana mpango wa kunipiga, sasa akazidi kunichokoza sana, alipoona yule kaka hajali, basi tukachorewa msitari atakayevuka ndo aaze kupigana yule kijana akavuka, akaanza kunipiga, nikiwa naogopa sanasana nikamshika, nikampiga vibaya sana sijui nguvu nilitoa wapi baadae nikaanza kulia mwenyewe kwa hasira!!!!!!!!!!!!!!!
   
 19. mama D

  mama D JF-Expert Member

  #19
  Apr 12, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 1,755
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  mimi nakumbuka nilchukuliwa na aunt yangu kwa lengo la kunisomesha maana familia yangu ilkua duni walkua matajiri sana lakini baada ya kuhamia kwake cha moto nilikiona maana nilkua house girl wa familia......... nilkua nawapikia watoto wake japo walkua wakubwa kwangu, nawafulia, nafanya usafi nyumba kubwa ya kifahari ikifika saa ya kuosha vyombo napanda juu ya kiti ili nifkie sink maana nlkua mdogo sana ikifika saa ya kula niko hoi hata kula siwezi nasinzia tuuu.....................................

  jamani sitamani kuwa mtoto hata kidogo
   
 20. wapalepale

  wapalepale JF-Expert Member

  #20
  Apr 12, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 259
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 33
  masikin weee ni bora ungekaa kwenu ucheze zako kombolela.. maisha ya geti wakati mwingine miyeyusho
   
Loading...