Hapa ndo najua hii nchi kwa nn ipo hivi hadi leo. Mkuu Lowassa akishinda anakuwa Rais wa nchi,akina mbowe watakuwa chini yake,yaani unachosema hapa lowassa akishinda waanze kumuomba abadili mfumo uliopo si ndicho unachomaanisha!!?? Akikataa mawazo yao itakuwaje na anauwezo hata kuwaacha kwenye baraza lake la mawaziri. Watafanya nini akina mbowe na wenzie wa ukawa?? Watarudi kwetu tena kutuambia huyu jamaa hafai?? Mimi ningewaelewa km lowassa angekuja chadema kuongeza nguvu tu lkn asigombee urais. Huo unaouita mfumo haujisimamii wenyewe,unasimamiwa na watu. Hao watu ndo hao hao wanatumia kila aina ya ujanja waendelee kuukumbatia. Amini usiamini lowassa akija kuwageuka chadema,chadema ndo itakuwa imezikwa haitaaminika tena!
Tatizo lako ni lile lile la Watanzania wengi tumeaminishwa kumwabudu mtu(RAIS) badala ya kuabudu sheria. Rais ni mtu tu kama wewe na huyupo juu ya sheria.
cdm/ukawa tutatengeneza sheria/katiba (na ndo mfumo wenyewe huo) ambao hata Rais atapaswa kuufuata na kuwa chini yake. Rais kupitia CDM hatokuwa mwenyekiti wa Chama nk nk. Tunataka mifumo iwekwe imuongoze rais jinsi ya kuenenda na si Rais arundikiwe madaraka ya kuamua tu kutenda kadri anavopenda. Unless utuambie ni wapi na lini Lowassa kasema akiwa Rais kupitia CDM hatobadilisha mifumo ya sasa ikiwemo Katiba ya Nchi?
na zaid sana ujue Rais si mtu, Rais ni taasisi, rais hatawali peke yake bali anatawala na wenzake.
acha uzuzu uliaminishwa kuwa Rais ni Mungu. Rais ni mtu muhimu katika nchi lakini Rais si kila kitu. Katiba ya nchi ndiyo (ndiyo inayopaswa kuwa) kila kitu, sheria za nchi ndo kila kitu. Tunatakiwa tuabudu KATIBA YA NCHI si Rais, Rais anakuja na kupita na anaweza kutoka udp, tlp, cuf, cdm, nccr nk nk lakini katiba ya nchi inasimama, na ukitaka kuibadilisha ni mbinde.