Hivi kinachoitwa MFUMO ni kitu gani?

Hivi kinachoitwa MFUMO ni kitu gani?

Ukweli utaniweka huru, Mfumo wa kifisadi unahama ccm na sasa unaingia cdm, wanaotengeneza mfumo ni watu tena hasa viongozi, na watu hao sasa wanaingia chadema na wanafuta uongozi, na hivyo mfumo wa kifisafi unahama kutoka ccm, unahamia cdm. Sina tatizo Lowasa kuhamia cdm ila atakapoteuliwa kuwa mgombea NAIKATA CDM. kwanini ang'ang'ania kwa nguvu nafasi hiyo. TUMEVURUGWA.
 
TUMEVURUGWA, kama lengo moja tu lililopo mbele kuiondoa ccm! TUMEVURUGWA. 'jumbemmoja alitoka nje kupigasimu, alipoingia akaniambia mkataa hauna shida na mamlaka ya juu wamesema upitishe' Kiongozi asiye namsimamo.
 
Hivi Tanzania hapa hapa kuna watu wanajua kutumia computer ama smart phone lakini hawajui mfumo ni nini? duh hakyanani nchi ina mapimbi hii ..halafu wanajidai wanajua kila kitu dah
 
Mkuu ngoja CHADEMA wataupeleka mahakamani mfumo halafu twende tukauangalie.......
 
Mfumo ni Mkusanyiko au Muunganiko wa vitu au sehemu ndogo zinazounda kitu kigumu au kitu kimoja.

Kwa tafsiri hii Mfumo unaoongelewa hapa ni Mfumo wa kifisadi ambao umo ndani ya CCM na Serikali yake ambao ni muunganiko wa Watu (Viongozi) na Tasisi mbalimbali za Serikali chini ya Usimamizi wa CCM (Chama Tawala) zinashirikiana kuwezesha Fisadi mbalimbali zinazotokea Nchini.

Kutokana na ukweli huu Mfumo unajumuisha watu wengi na wakati mwigine Taasisi zaidi ya moja. Hivyo katika Mfumo huu wa Kifisadi hata ukimtoa Mtu moja bado haibadilishi kitu, japo Mtu huyu mmoja mkimtoa anweza kubadilika. Kuvunja Mfumo ni Kuondoa Msimamizi wa hawa Watu (viongozi) na Taasisi za Serikali ambae ni CCM

Good job "JB"Kwa ulivyo jitahidi kiufafanuzi hakuna atakaye thani kua uliishia std 7.
 
Nakuhakikishia Chenge, Rostam wanaweza kuhamia chama kingine chochote na huko wakawa viongozi wazuri kulingana na utamaduni watakaoukuta huko. Kwa lugha nyepesi, kinachoitwa 'mfumo' hapa ni utamaduni uliojengeka chini ya uongozi wa ccm ambapo wakosaji na wezi wa mali ya umma wenye nyadhifa serikalini hawawajibishwi kwa makosa wanayotenda. Badala yake wanalindwa. Wanasiasa hao wakihamia chama kingine ambacho hakina huo utamaduni wa hovyo, hawana jinsi bali kubadilika.

Acha kujifariji haohao walounda huo mfumo mmbovu ndo wanahamia chadema na kupewa madaraka ya juu kama raisi unategemea huo mfumo utabadilika zaidi ya kutoka ccm na kuhamia chadema hao kina rostam,karamagi,chenge wako nyuma ya lowasa akipata uraisi nani wakuwazuia kufanya yao maana mtu wao ndo top na mbowe wala slaa hawezi wazuia maana watakua hawana sauti tena
 
Na mimi leo hii nilikuwa nauliza watu kuhusu hiki kitu kinaitwa mfumo kama wanakifahamu ama wanashabikia tu kwakweli mkuu umeweka moja ya discussion ambazo ni za hekima kuliko zote nimewahi kusoma humu maana nilikuwa nimeanza kuzichoka post za humu
 
Yap wanayarudia yale yale wao wenyewe hawana huo mfumo thabiti wakiambiwa mkaguzi anakuja utasikia hesabu zao aziko tayari na walipata hati chafu sujui yenye mashaka kutoka kwa CAG from their accounting books.

Lakini aliondoi tatizo la jumla kwanza CAG anapofika akutakiwi kuwa na hadithi hatupo tayari or else inaondoa the meaning of random checks, ndio maana wewe unaajiri accoutants wako kwa sababu ya vitu kama hivi.

Mbali na CDM au vyama vya siasa hata kwenye taasisi za serikari ni hivi hivi NHC mwaka wa pili wanamaliza awajatoa financial statement publicly na taasisi nyingi za serikari azifanyi hivyo. Ni mwanzo tu kwakweli mfumo wa usimamizi ni tatizo including ndani ya hao hao CDM wenyewe not only with their expenditures but also having a vision on what they want to do with Tanzania.

This is a national problem
. wee huelewi maana ya mifumo ya nchi. hivi hapa unavoviongelea ni vitawi tu vya miti mikubwa ya mifumo ya nchi. huyo CAG anachaguliwa kupitia mifumo gani? ipo sahihi? nani anamteua CAG na anamteua kwa sheria ipi? hiyo sheria imeundwa chini ya sheria mama(Katiba) ya aina gani? katiba ya nchi ndo baba na mama wa matawi mengine yote ya mifumo ya nchi. Je Katiba ya sasa inayotetewa na ccm ipo kwa maslah mapana ya nchi au kikundi kidogo cha ccm?

hiyo NHC unaongelea ipo kwa sheria ipi na sheria hiyo inatokana na katiba ya aina gani?

Mfumo wa ccm unamfanya Rais, badala ya katiba ya nchi, kuwa Mungu mtu wa kuteua kila mtu, kuunda na kuvunja kila Taasisi ya Umma nk nk. Mfumo ni dhaifu kuanzia juu, ni mfumo wa kulindana na hata wizi, na ufisadi, wa ccm si wa mtu mmoja mmoja bali ni wa kimfumo na ndo maana wao wenyewe kwa wenywe hawakamatani. Mwizi hawezi kumkamata mwizi mwenziye. wanalindana na ikibidi mwizi anamua mwizi mwenziwe ili kupoteza ushahidi..rejea ya stakishari jamaa wa pikipiki ilivokataa kuwaka wezi wenziwe walimfanyaje?

wewe na mimi hatujui hata alikozikwa Balali ni wapi, au wewe unajua?
 
Acha kujifariji haohao walounda huo mfumo mmbovu ndo wanahamia chadema na kupewa madaraka ya juu kama raisi unategemea huo mfumo utabadilika zaidi ya kutoka ccm na kuhamia chadema hao kina rostam,karamagi,chenge wako nyuma ya lowasa akipata uraisi nani wakuwazuia kufanya yao maana mtu wao ndo top na mbowe wala slaa hawezi wazuia maana watakua hawana sauti tena
yaan nyie akili zenu nyembamba sana hazijajua methali.

ni hivi, ukiyamimina maji kwenye sufuria yatakaa katika umbo flani ndani ya sufuria. maji hayo hayo ukiyamimina ndani ya chupa ya dasani umbo litakalochukuliwa na maji hayo litakuwa tofauti sana na lile la kwenye ile sufurIA. Maji ni yale yale(wana ccm) lakini yanalazimika kujiumba tofauti(kubadilika kutoka kwenye tabia za kifisadi) kutokana na aina ya chombo (chama cha siasa na aina ya mifumo kilichojitengenezea) yalipomiminwa maji hayo.

Katika ccm ufisadi haiwezi kwisha kwa sababu, mifumo iliyojitengenezea, ya ndani ya chama na katika serikali yake, ni ile inayolinda na kurutubisha ufisadi na si kuupiga vita. ndo maana utaskia leo waziri mmoja wa ccm kafukuzwa kwa ufisadi, kesho unaskia tena mwingine, hujakaa sawa tena na mwingine, na mwingine na mwingine lakini ufisadi upo pale pale ccm. hauwezi kwisha kwa kumfukuza waziri mmoja bila kuharibu huo mfumo kwanza. utafukuza hata serikali nzima lakini wizi ni pale pale.

na kiukweli, katika mfumo wa kifisadi kama wa ccm, wale wasio fisadi (kama kina warioba, Butiku nk) mfumo unakuwa repellant kwao na unawa suck out of the system na mwisho wanaishia katika aibu na kudharauliwa.

kama lowassa, alipokuwa ccm alifisadi chochote (which so far is not the case until evidently proved otherwise) ni kwa sababu ndo mfumo wenyewe ulivomtaka afanye la sivyo ungem repel out. Kwani m-ccm Lowassa asiibe kwa nini wakati wa-ccm wenziwe wote wanaiba?
 
Mfumo ni muunganiko wa sheria, kanuni, taratibu, mtindo wa kuongoza, regulator, na washiriki (participants). Kimoja wapo kikiwa kibovu basi mfumo mzima utakuwa ni mbovu. Hivyo mfumo wa ccm umeoza. Participants wanaweza kuwa wapo vizuri lakini components nyingine zikawa mbovu hivyo lazima mfumo utafeli. Ni sawa na mfumo wa umeng'enyaji wa chakula mwilini (digestive system) ambao umeundwa kwa mdomo, meno, ulimimi, mate, koromeo, enzymes (vimeng'enya), utumbo mpana, utumbo mwembamba, ini, appendix, etc. appendix ikikorofisha mfumo mzima utashindwa kufanya kazi. Hata kama unameno mazima ini likikorofisha tuu basi mfumo mzima wa kumeng'enya chakula utashindwa kufanya kazi. Hivyo mfumo wa ccm umefeli kulitoa taifa kwenye dimbwi la umaskini kwavile ini la ccm limeoza hata kama wana meno mazima. Nadhani mtoa mada utakuwa umeelewa maana ya mfumo na kwanini watu wanasema mfumo wa ccm ni mbovu na endapo wana ccm wote wakiamua kuhama ccm na kwenda kwenye system zenye mfumo mzuri tutapata mafanikio.
 
Ukweli utaniweka huru, Mfumo wa kifisadi unahama ccm na sasa unaingia cdm, wanaotengeneza mfumo ni watu tena hasa viongozi, na watu hao sasa wanaingia chadema na wanafuta uongozi, na hivyo mfumo wa kifisafi unahama kutoka ccm, unahamia cdm. Sina tatizo Lowasa kuhamia cdm ila atakapoteuliwa kuwa mgombea NAIKATA CDM. kwanini ang'ang'ania kwa nguvu nafasi hiyo. TUMEVURUGWA.

Ili kuyajua haya unahitaji kuwa na fikra pana kwa kuuweka ushabiki pembeni...
 
Wewe unaonekana unahitaji kweli kuelewa [Maana kwa kuuliza hili swali inaonesha umepata maana ya mfumo kutoka kwa wachangiaji waliopita]. Lakini ulivyosema "hao watu wote" hujawa wazi, wote una maana wana-CCM wote wa Tz au ulimaanisha wana-CCM wanaonyooshewa vidole kwa kashfa? Na ulivyosema "chama kikabaki ivoivo" umemaanisha chama gani (CCM au CHADEMA)?
Nisamaraizi tu ninavyoelewa: Mfumo wa CCM unaozungumziwa ni kile kitendo cha kundi kubwa la Wanachama wake kujitengenezea mitandao ambayo inasababisha ugumu wa kuwajibishana pale ambapo kuna viashiria vyote vya watu kutakiwa kuwajibishwa. Hili limefanya uwepo huo wa mitandao (ambao ndiyo kiina cha kinachoitwa mfumo) kuwapa viburi watendaji wengi wa CCM. Wengi wanashindwa kabisa kuwa serious katika maslahi ya umma huku kukikosekana kabisa ubavu wa kuwajibishana. Kipindi kifupi cha hivi karibuni wameonekana kushtuka kuwa Watz wanaanza kuwaelewa, sasa wanalitumia Bunge kufanya hiki kinachoitwa kuwajibishana (lakini ni kwa kuwahadaa watu). Nasema kuwahadaa, ukitaka kunielewa jaribu kuchunguza wote waliowahi kuwajibishwa wana maisha gani baada ya hapo. Ukweli ni kuwa mfumo wao (wa kimtandao) hauwaruhusu kutiana adabu ya ukweliukweli. Wamekaa muda mrefu wakajitengenezea huo mfumo kwa watu kuweka mitandao. Ipo ya kifamilia, kindugu, kikabila, kikanda, kidini, nyumba ndogo, nk. Kiburi kimetokana na huo mfumo. Ndiyo maana kuna watu wanaamini hata CCM ikipambanishwa na jiwe wako radhi kulichagua jiwe. Hii ikiwa na maana ya kuwapa muda nje ya uongozi huku hilo jiwe likiuponda ule mfumo wa zamani ili hata kikirudi tena kiwe na adabu.
Sasa kama kuna watu watahama CCM na kuhamia chama pinzani (kama CHADEMA), swali linabaki ni wote wale wenye mitandao iliyotengeneza huo mfumo? Sasa kama wote wa mitandao (ambapo ni ngumu) watahama CCM na kuhamia CHADEMA na CCM ikabaki na wasafi (wapo wanaopenda mabadiriko ila hawana nguvu, wanaishia kudaka tu tonge na hawana ujasiri wa kukimbia chama) mfumo hovyo CCM unaweza kufa na CCM mpya kuzaliwa. Wakati huo nako huwezi sema moja kwa moja kjwa CHADEMA itakuwa imeingia katika ule mfumo mfu uliokuwa CCM (itategemea na nguvu yao kuwatia adabu wahamiaji).
Cheers


Swali Je hao watu wote wa CCM wakiamia Chadema na chama kikabaki ivoivo huo mfumo umekufa au la???????
 
Safi sana mkuu jibu lako limetosheleze... Na kule kuna magege ya wez toka awamu ya kwaza kila mstafu genge lilindwe!
 
. wee huelewi maana ya mifumo ya nchi. hivi hapa unavoviongelea ni vitawi tu vya miti mikubwa ya mifumo ya nchi. huyo CAG anachaguliwa kupitia mifumo gani? ipo sahihi? nani anamteua CAG na anamteua kwa sheria ipi? hiyo sheria imeundwa chini ya sheria mama(Katiba) ya aina gani? katiba ya nchi ndo baba na mama wa matawi mengine yote ya mifumo ya nchi. Je Katiba ya sasa inayotetewa na ccm ipo kwa maslah mapana ya nchi au kikundi kidogo cha ccm?

hiyo NHC unaongelea ipo kwa sheria ipi na sheria hiyo inatokana na katiba ya aina gani?

Mfumo wa ccm unamfanya Rais, badala ya katiba ya nchi, kuwa Mungu mtu wa kuteua kila mtu, kuunda na kuvunja kila Taasisi ya Umma nk nk. Mfumo ni dhaifu kuanzia juu, ni mfumo wa kulindana na hata wizi, na ufisadi, wa ccm si wa mtu mmoja mmoja bali ni wa kimfumo na ndo maana wao wenyewe kwa wenywe hawakamatani. Mwizi hawezi kumkamata mwizi mwenziye. wanalindana na ikibidi mwizi anamua mwizi mwenziwe ili kupoteza ushahidi..rejea ya stakishari jamaa wa pikipiki ilivokataa kuwaka wezi wenziwe walimfanyaje?

wewe na mimi hatujui hata alikozikwa Balali ni wapi, au wewe unajua?

Nadhani unachanganya mambo Katiba sio mfumo bali ni mkataba wa mamlaka ya serikari na wananchi unaoelezea mipaka ya serikari na jinsi nchi itavyo endeshwa ikifafanua limitations za powers za serikari, uhusiano wa mamlaka za serikari katika kutekeleza azima ya uongozi na kusimamia, mgawanyo wa majukumu na haki za wananchi katika nchi husika.

Namna gani chama tawala inasimamia hizo administration za serikari katika kufikia malengo ya kisera, bunge linavyosimamia serikari na mahakama pamoja na taasisi zake zingine za kisheria zinavyolinda sheria za nchi na kuakikisha kila kitu kinafanyika ndani ya mipaka ya katiba na sheria za bunge ndio mfumo.

Kwa hivyo mfumo umegawanyika katika sehemu tatu kuu serikari kuu (taasisi ya raisi na baraza lake la mawaziri pamoja na vyombo vinavyosadia kusimamia uendeshawaji wa shuhuli za serikari kwa na namna ya watchdogs kama ewura, CAG, TBS, etc pamoja na idara za serikari zilizoko chini ya mamlaka ya wizara), pili bunge linalo isimamia serikari pamoja na kuleta hoja za wananchi bungeni kuhusu mahitaji yao, kutunga sheria za nchi na kusimamia maslahi ya wananchi na accountability ya serikari i.e mawaziri, watchdogs and idara za serikari azifanyi mambo kiholela, tatu judiciary ie mahakama na vyombo vya sheria kama polisi, takukuru etc, ambavyo vipo kuakikisha vitu vinafanywa kisheria na sheria zenyewe azipo kinyume na mkataba wa wananchi na serikari (katiba) to ensure checks. Hayo ni kwa ufupi lakini kuna mambo mengi sana katika kila mhimili unaovyanya kazi zake kuakikisha efficiency zinapatikana ikiwemo maadili ya watumishi, sheria za sehemu na upeo wa wasimamizi wenyewe.

Kwa hivyo mfumo mmbovu unatokana na mambo mengi sana na unaweza kosolewa na chombo chochote cha usimamizi CAG katika shughuli zake anaweza kosoa udhaifu wa usimamizi wa mapato na akatoa sababu zake, bunge linaweza kosoa mfumo wa wizara fulani kwenye mechanism za kutekeleza sera na kuonyesha upotefu wa mapato, hiyo sera isivyo wafikia kundi fulani au kupitia kamati zake inaweza kuona mfumo wa tender unaoleta ufisadi, conflict of interest, mahakama zinavyochelewa kutoa haki au adhabu kwa wakosaji etc.

Mahakama nayo inaweza ona sheria fulani za nchi sio sahihi kikatiba, sehemu zake zingine zinaweza kuwa poorly funded kama polisi walivyo katika kuhakikisha wezi wanapelekwa sehemu husika na usimamizi imara wa sheria za nchi, wezi serikarini awalindwi etc.

Mwenye jukumu la mengi ya yote hayo ni chama tawala kwa sababu wao ndio wasimamizi wakuu na wenye mamlaka ya kuakikisha kila kitu kipo katikaa ubora wake na kila taasisi ina deliver accordingly as stated by their function, sasa kama CAG kutokana na mamlaka yake akisema sehemu fulani nimekutana na hiki na bado hakuna maamuzi the bulk stop with the responsible authorities to change things inaweza kuwa kubadilisha sheria, waziri, mkurugenzi wa shirika, namna bora ya usimamizi or even more investment depending on the nature of the highlighted problem.
 
Back
Top Bottom