Hivi kinachoitwa MFUMO ni kitu gani?

Hivi kinachoitwa MFUMO ni kitu gani?

Ndugu mtoa mada nakwambia kuna maajabu mengi duniani ila inabidi liongezwe ajabu jibya ambalo ni watanzania.

Yaani wanaibiwa mchana kweupe kabisa alafu hawashtuki kama misukule. Mie ngoja niendelee kusubiri Rostam, Chenge na Karamagi kukaribishwa na ukawa alafu mzee mbowe kama kawaida anakupa siasa ni dynamics tunabadirisha gia angani.

Kweli hela mwanaharamu, imenunua hadi Malaika tuliowaamini.

Mkuu..mwizi hawezi iba akiwa ndani ya jera..ili maxingira ya wizi yawepo ni kombineshen ya vitu vingi sana
 
Yap wanayarudia yale yale wao wenyewe hawana huo mfumo thabiti wakiambiwa mkaguzi anakuja utasikia hesabu zao aziko tayari na walipata hati chafu sujui yenye mashaka kutoka kwa CAG from their accounting books.

Lakini aliondoi tatizo la jumla kwanza CAG anapofika akutakiwi kuwa na hadithi hatupo tayari or else inaondoa the meaning of random checks, ndio maana wewe unaajiri accoutants wako kwa sababu ya vitu kama hivi.

Mbali na CDM au vyama vya siasa hata kwenye taasisi za serikari ni hivi hivi NHC mwaka wa pili wanamaliza awajatoa financial statement publicly na taasisi nyingi za serikari azifanyi hivyo. Ni mwanzo tu kwakweli mfumo wa usimamizi ni tatizo including ndani ya hao hao CDM wenyewe not only with their expenditures but also having a vision on what they want to do with Tanzania.

This is a national problem

Mkuu eriq..asante sana umeongea bila ushabiki na kupepesa macho?
 
Hawa jamaa wa lumumba wasituongezee notes ati, mfumo wanaujua vizuri tu, hpo wanataka watafte pakutokea..
Cha msingi tuwajibu hvi..

Mfumo tunaouita ni adui yetu ni SERIKALI ya CCM, just as simple as that, kwakua hyo ndo imebeba mauchafu yote, haina haja kuumizana vidole kuwaandikia watu wenye akili zao ila wasiotaka kuelewa, kikwetu tunasema hivi "Kosamba na tondo oka uilhepvo", yaani ukinawa pamoja na mpumbavu huwezi kutakata hata mara/siku moja.
#Nawasilisha
 
Mfumo wa ovyo unaozungumziwa nadhani ni jinsi chama tawala kinavyo isimamia serikari kuakikisha matumizi na sera azichakachuliwi ovyo, nidhamu ya wafanyakazi wa serikari na wanachama wa vyama pia wanavyo behave.

Kikawaida kila mfanyakazi anawekewa code of conduct kutokana na malengo ya taasisi na utaukumiwa kwa kuvunja hivyo iwe usimamizi legelege wa kitengo unacho ongoza, hasara uliyoitia taifa, mwenendo wa ovyo wa kiongozi kimaadili, ubora wa taasisi na wafanyakazi wake katika kueshimu code of conduct, etc.

Kwa hivyo nadhani wanaposema mfumo huko ovyo serikarini kwa kweli kuna hoja leo hakuna jitihada zozote za serikari despite CAG kuanzia kwa Utoh na huyu wa sasa wote kusema kuna kupwaya sana kwenye management levels za serikari and lack of creativity on running most organization inayosababishia ufisadi na inefficiency on quality of the services.

Kipi kimebadilika kutatua hilo hakuna, kwa maana hiyo chama tawala bado kinalea mfumo usio efficiency kwenye kutatua tatizo la ufisadi hakuna imposition of strict adherence of code of conduct in public sector nor thorough organization function audit to rectify repeating offences and slack supervision sanasana watapewa seminar tu.

Tanzania mtu anaweza jiamkia tu asubuhi na kubuni kodi bila ya kujali or introduce fees na kuchakachuwa hili taasisi yake ipate hela za kufanya tafrija na pengine kufisadi to name a few.

Mfumo ni tatizo hila CDM awana majibu vinginevyo wakependekeza hila yap hoja yao ya ufisadi ni product ya utawala mmbovu na supervision mechanism iliyozaa watu kama akina Lowassa, Chenge, Karamagi et al na bado kuwepo mtaani inasimama kialali.

thesunfrontpage--(None)_MED.jpg

This is him in private

sewel_3387803b.jpg


The same man in public utadhani mtu wa maana.

Jana kwenye nchi za wenzetu kiongozi na mwakilishi imebidi aachie ngazi kwaku pigwa picha anatumia mihadharati, yuko na prostitute and his somewhat perplexing pose; hakuna alichovunja kisheria bali under the code of conduct ya kiongozi wa taifa this is unacceptable.

Sasa tena kwa yale anayoleta CAG wetu ambapo kuna serious issues of flaws on mfumo which could save the nation billions of money if not a trillion by only implementing a better system of supervision na bado hakuna maamuzi sahihi we have a problem.
Unakosea sana pale unapomlaumu CAG,katiba tuliyonayo ambayo ndio inamuweka CAG in power via the president,haimpi mandate ya kuwajibisha culprits, that's why utaskia wanasem CAG anafanya kazi nzuri but hana meno. Chamsingi kubadili mfumo tulionao ambao hautaki kumpatia meno CAG via katiba mpya, then tuone effect us CAG moja kwa moja.. Kwakua katiba iliyopo sec 45.inamtaka CAG akishafanya uchunguzi wake aripoti kwa aliyemteua (Rais),hapo unategemea nini?
Tuutoe mfumo ndo tuurekebishe then tuurudishe kazini
 
Ulisoma Biology o-level?

Cells⏩tissue⏩organ⏩system.
 
Jamaa angebaki ccm mgempa sifa kibao wakati nae thief mkubwa siasa jaman acha tu
 
Kinachoipa nguvu chadema ni kuwa na wanachama na washabiki mfano wa wanyamapori Nyumbu!
 
magode

Hili swali ni kubwa sana kwa wana chadema. Ogopa sana ushabiki! Kule ccm kuna wanaoitwa "wakereketwa". Wale wakereketwa walioko ccm ni sawasawa na hawa "nyumbu" waliopo chadema. Leo hii lowasa akitoka cdm, hawa hawa wanageuka na kusema "bora alivyoondoka"!
 
Last edited by a moderator:
Wewe unaonekana unahitaji kweli kuelewa [Maana kwa kuuliza hili swali inaonesha umepata maana ya mfumo kutoka kwa wachangiaji waliopita]. Lakini ulivyosema "hao watu wote" hujawa wazi, wote una maana wana-CCM wote wa Tz au ulimaanisha wana-CCM wanaonyooshewa vidole kwa kashfa? Na ulivyosema "chama kikabaki ivoivo" umemaanisha chama gani (CCM au CHADEMA)?
Nisamaraizi tu ninavyoelewa: Mfumo wa CCM unaozungumziwa ni kile kitendo cha kundi kubwa la Wanachama wake kujitengenezea mitandao ambayo inasababisha ugumu wa kuwajibishana pale ambapo kuna viashiria vyote vya watu kutakiwa kuwajibishwa. Hili limefanya uwepo huo wa mitandao (ambao ndiyo kiina cha kinachoitwa mfumo) kuwapa viburi watendaji wengi wa CCM. Wengi wanashindwa kabisa kuwa serious katika maslahi ya umma huku kukikosekana kabisa ubavu wa kuwajibishana. Kipindi kifupi cha hivi karibuni wameonekana kushtuka kuwa Watz wanaanza kuwaelewa, sasa wanalitumia Bunge kufanya hiki kinachoitwa kuwajibishana (lakini ni kwa kuwahadaa watu). Nasema kuwahadaa, ukitaka kunielewa jaribu kuchunguza wote waliowahi kuwajibishwa wana maisha gani baada ya hapo. Ukweli ni kuwa mfumo wao (wa kimtandao) hauwaruhusu kutiana adabu ya ukweliukweli. Wamekaa muda mrefu wakajitengenezea huo mfumo kwa watu kuweka mitandao. Ipo ya kifamilia, kindugu, kikabila, kikanda, kidini, nyumba ndogo, nk. Kiburi kimetokana na huo mfumo. Ndiyo maana kuna watu wanaamini hata CCM ikipambanishwa na jiwe wako radhi kulichagua jiwe. Hii ikiwa na maana ya kuwapa muda nje ya uongozi huku hilo jiwe likiuponda ule mfumo wa zamani ili hata kikirudi tena kiwe na adabu.
Sasa kama kuna watu watahama CCM na kuhamia chama pinzani (kama CHADEMA), swali linabaki ni wote wale wenye mitandao iliyotengeneza huo mfumo? Sasa kama wote wa mitandao (ambapo ni ngumu) watahama CCM na kuhamia CHADEMA na CCM ikabaki na wasafi (wapo wanaopenda mabadiriko ila hawana nguvu, wanaishia kudaka tu tonge na hawana ujasiri wa kukimbia chama) mfumo hovyo CCM unaweza kufa na CCM mpya kuzaliwa. Wakati huo nako huwezi sema moja kwa moja kjwa CHADEMA itakuwa imeingia katika ule mfumo mfu uliokuwa CCM (itategemea na nguvu yao kuwatia adabu wahamiaji).
Cheers
Mkuu Guus nafurahi kwamba kwa kiasi fulani umenielewa. Wachangiaji wengi wamejikita kunipa maana ya mfumo ambayo kimsingi siyo hoja yangu. Hoja yangu hapa ni kwamba,huo mfumo ni kitu gani!?? Lowassa alikuwa mtendaji mkuu wa serikali na msimamizi mkuu wa shughuli za serikali bungeni. Alifanya nn kuonyesha kwamba alikuwa anakerwa na huo mfumo!!? Kibaya zaidi nae ni mtuhumiwa wa ufisadi,ukiacha richmond,alishatiliwa mashaka kitambo juu ya utajiri wake.

Tukirudi kwenye hoja yangu,km huyu ambae alikuwa ktk huo mfumo,amepokelewa huku ambako watu walikuwa wameanza kupata matumaini ya kubadili maisha ya watanzania. Anakuja huku anasemwa hana tatizo na anapewa nafasi kubwa kabisa ya kuwa mgombea urais. Nini kitakachomfanya asiendelee kuukumbatia huo mfumo-ccm!!?? Hatuwezi kusema tatizo ni mfumo eti tatizo siyo watu! Wakati mfumo si kitu kinachojiendesha na kujisimamia chenyewe. Mfumo unasimamiwa na watu ni lazima tuwakatae hao ili kuweka nidhamu.

Kule uchina kiongozi akituhumiwa,anaachia ngazi,then anachunguzwa,akithibitishwa kashiriki kwenye ufisadi ananyongwa! Km tunachukulia umaarufu wake ili kupata serikali,kwa nini tusiseme hawa nao ni wale wale!!??
 
Last edited by a moderator:
wee ni darasa la ngapi? maana tukijua LEVEL YA darsa tutajua tukupe dozi ya kiwango gani na KWA stahili ipi tusije tukakuzidishia dozi.

hulaumiwi sana kwa sababu katika afrika, na Tanzania kipekee, si ajabu kukuta mtu anachaguliwa si kwa sababu ana sera nzuri za kuusaidia umma ila kwa sababu tu ni mwigizaji mzuri, ni mwanakaya mzuri, anajua "kukandia" wapinzani vizur jukwaan nk nk. Ukimuuliza mtu kwa nini unamuunga huyu mkono wakati hata sera hana anakwaambia "sera ndo nini bhana, sisi tunachotaka ni mtu anayewapasha vizur wapinzani wakapashika"......???!!!

ni tatizo la elimu ndogo na kutokujifahamu.

Kifupi tu nikwaambie nchi ni mifumo+Taaasisi. nchi si mtu.

Tanzania ya zama za mfumo wa kijamaa ni tofauti sana na Tanzania ya leo ya mfumo wa Ubepari uchwara. mifumo ni pamoja na Katiba, sera, sheria nk nk.

Achilia mbali nchi hata familia tu zinatofautiana kutokana na mifumo. Aina ya mifumo utakayoijenga ndani ya ndoa yako itaamua aina ya ndoa mnayoishi na aina ya watoto mtakaowakuza kupitia mifumo hiyo ya ndoa yenu. kama moja ya mfumo wako ni kurudi nyumbani saa tisa usiku ukiwa umelewa, umejikojolea na kujinyea basi huo ndo mfumo utakaoridhiwa na wanao na ndo watakavokuwa na wao. kama baba wa familia, haijalishi kama u msomi au la, tajiri au la bali kinachojalisha ni aina ya mfumo ulioujenga katika ndoa yako.

Rais Lowassa kupitia Mfumo safi wa CDM na UKAWA ni lazima atakuwa mtu tofauti kabisa na Rais Lowassa kupitia mfumo wa kifisadi wa CCM
Kwa hiyo kwa mfano uliotoa,baba akihama nyumba na watoto wake akahamia sehemu nyingine ndo mfumo huo utakuwa umeisha!?? Wenye akili za kuvukia barabara,huu uzi piteni kando si size yenu. Eti unaandika nchi siyo watu,kwa hiyo nchi ni mfumo..!!? Huo mfumo ni kitu gani ambacho kinauwezo wa kujiendesha na kujisimamia hakiendeshwi na watu!!? Km kinaendeshwa na watu,watu wale wale wakihamia sehemu nyingine na nyadhifa zilezile,nini kitakachowazuia kuishi mfumo waliouzoea!!??
 
Mfumo ni neno tu la CHADEMA NA UKAWA kuhalalisha tamaa yao ya madaraka.Huo wanaouita Mfumo ambao unamfanaya kila mtu CCM awe fisadi umewekewa madawa gani ambayo Kiongozi wa CCM au mwanachama ashindwe kutafakari anachofanya ni sahihi ama sio sahihi? Nitatoa mfano: Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar alipinga pendekezo la Rasimu ya pili katiba bila kujali mfumo wa CCM kupinga rasimu ya jaji warioba. Kwanini Magufuli, Lowasa na wengineo hawana ujasiri wa kupinga mfumo unaolalamikiwa na CHADEMA NA UKAWA ndani ya ccm? Mfumo mbaya uliopo CCM haumuondoi AKILI kiongozi kushindwa kutafakari anachoambiwa kama kina masilahi kwa nchi ama la. Lowasa anasema kila alichokifanya JK alikijua, alilazimishwa kusaini, Hivi EL aliondokwa na akili asifahamu kwamba anachokifanya kitakwenda kuligharimu Taifa? Hivi JK akisema nilifanya vile kumpima EL kama ana akili au hana akili EL atajibu nini? Maana JK anasema akili za kuambiwa changanya na zako.Hii kitu imenilet down sana nimeishiwa nguvu kabisa na ninapata shida kwa Tundulisu na Dr.Slaa niliowaamini kwamba wao ni zaidi ya wanasiasa, ni wanaharakati na wazalendo wa kweli kwa nchi hii. Nadhani mwisho wangu wa kuwaamini na kushabikia wanasiasa nauzika rasmi mwaka huu na hata kupiga kura sitakwenda kama EL atapewa nafasi ya kugombea Uraisi kupitia CHADEMA/UKAWA
Ndugu zangu watanzania tuwe wa kweli tusiyumbishwe na wanasiasa.
 
Mfumo ni neno tu la CHADEMA NA UKAWA kuhalalisha tamaa yao ya madaraka.Huo wanaouita Mfumo ambao unamfanaya kila mtu CCM awe fisadi umewekewa madawa gani ambayo Kiongozi wa CCM au mwanachama ashindwe kutafakari anachofanya ni sahihi ama sio sahihi? Nitatoa mfano: Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar alipinga pendekezo la Rasimu ya pili katiba bila kujali mfumo wa CCM kupinga rasimu ya jaji warioba. Kwanini Magufuli, Lowasa na wengineo hawana ujasiri wa kupinga mfumo unaolalamikiwa na CHADEMA NA UKAWA ndani ya ccm? Mfumo mbaya uliopo CCM haumuondoi AKILI kiongozi kushindwa kutafakari anachoambiwa kama kina masilahi kwa nchi ama la. Lowasa anasema kila alichokifanya JK alikijua, alilazimishwa kusaini, Hivi EL aliondokwa na akili asifahamu kwamba anachokifanya kitakwenda kuligharimu Taifa? Hivi JK akisema nilifanya vile kumpima EL kama ana akili au hana akili EL atajibu nini? Maana JK anasema akili za kuambiwa changanya na zako.Hii kitu imenilet down sana nimeishiwa nguvu kabisa na ninapata shida kwa Tundulisu na Dr.Slaa niliowaamini kwamba wao ni zaidi ya wanasiasa, ni wanaharakati na wazalendo wa kweli kwa nchi hii. Nadhani mwisho wangu wa kuwaamini na kushabikia wanasiasa nauzika rasmi mwaka huu na hata kupiga kura sitakwenda kama EL atapewa nafasi ya kugombea Uraisi kupitia CHADEMA/UKAWA
Ndugu zangu watanzania tuwe wa kweli tusiyumbishwe na wanasiasa.
Huu ndo utani tunaosema hatuutaki kwenye ikulu ya nchi hii. kwa hiyo hiko ndo ambacho huwa anafanya huyo jk? na kwa nini sasa hamumwuulizi huyo aliyetuma badala yake mnamsakama aliyetumwa? leo ccm mnasema jk hakumtuma EL, kesho na keshokutwa JK atakapohamia CDM ndo nyie nyie mtakaosema jk alimtuma EL.

NI HERI KUKUBALI TU MLIKOSEA kisha mjisahihishe kuliko kushupaa mishipa ya shingo wakati kila kitu kipo wazi na siku hadi siku mnazidi kuumbuka.
 
Tanzania na Watanzania tunapitia katika kipindi kigumu nafikiri kuwai kutokea katika taifa letu. Ni kipindi ambacho tunajiuliza kuwa tumwamini nani? Mbona wale tuliojua kuwa ni watu wa kuwaamini nao wamebebwa na nguvu ya fedha??? Tunapitia kipindi ambacho sio kwamba sie ni wa kwanza kukipitia la hasha hata wenzetu wa Italy na Thailand walishawai kukipitia ila tofauti ni kuwa hizi nchi ni za tofauti sana na Tanzania kuanzia kiuchumi hata kisiasa.

Kwanini nasema hivi?
Kutokana na hali halisi kuwa Tanzania ni nchi ambayo kimaendeleo tunaweza kusema kuwa ni kama ndege iliyo kwenye njia yake kuelekea kuruka, yaani ni nchi ambayo inafunguka zaidi kifursa kiasi ambacho kwa watu wakubwa wa ndani na wa nje imegeuka kuwa sehemu wanayoiangalia sana. Hii imetokana na fursa za maliasili, madini ambayo inasemwa hadi leo yaliyochimbwa ni asilimia 10 tu na mafuta na gesi.

Kwa matajiri na watu wenye nguvu ya kifedha ambao wanataka waendelee kumaintain status quo yao au wanataka waendelee kukua zaidi na zaidi wanajua kuwa wakiweza kuikamata Tanzania leo basi watakamata hizi fursa zote na siku ya mwisho Forbes itawatambua.

Matajili ni watu wenye akili sana na wanajuaga sana mahali popote pale, ukitaka kula mema ya nchi basi kikubwa ni kwa gharama yeyote ile muwekeni mtu wenu kwenye top post ya hiyo nchi. kwa nchi zingine top post kiserikali ni waziri mkuu kama italy na Thailand ila kwa Tanzania ni RAIS. Ukishamuweka tu malengo yako yote ya kibiashara yatatimia.

Kama nilivosema hapo juu kuwa yanayotokea leo Tanzania sio yameanzia hapa la hasha yameanzia huko mbele na mfano mzuri ni italy ambapo kulikuwa na Bilionea ambaye sasa yuko jela anajulikana kama Silvio Berlusconi na Thailand kulikuwa na bilionea anayejulikana kama Taksin Shinawatra. Kwa msio wafahamu hawa watu hawa ni matajili wakubwa sana na walitumia sana nguvu yao ya pesa kutengeneza ushawishi wa kisiasa kwenye nchi zao, kwa Thailand ilibidi jeshi(system) iingilie kati kumuondoa Shinawatra ila kwa italy ilibidi wapate msaada wa nje ili kuweza kuiharibu syndicate ya bwana Silvio Berlusconi na hata leo hii wanashukuru ni bora ameondoka na yuko jela.

Hali ilivokuwa Tanzania sasa:
Kwa hapa Tanzania kuna syndicate ilishajipanga tangu mda kuwa lazima mwaka 2015 tuweke mtu wetu. N i kundi kubwa lenye nguvu ya pesa tena sio kawaida ni sana ambalo lilijipanga kisawa sawa kuwa lazima tuikamate CCM na tuiforce imuweke mtu wetu. Walijipanga vizuri sana kuanzia makanisani, misikitini, bodaboda hadi vyuo vikuu. KWA KIFUPI walimpa mtu wao fedha nyingi sana ili ajenge ushawishi kwa sababu walijua weakeness kubwa ya watanzania/waafrika(na binadamu kwa ujumla) ni fedha. Zilitolewa hela zisizo za kawaida makanisani, misikitini na hata meeneo mengi kama bodaboda na vyouni, walitafutwa wahariri wa vyombo vya habari wakaongwa fedha nyingi sana na kwa kifupi hawa watu waliweza kununua asilimia 90 ya vyombo vya habari.

Walivofika dodoma walikuwa na uhakika kuwa iwe isiwe lazima nguvu ya fedha itatamalaki kiasi ambacho mtu wao atapita ambaye ni EL. ila hamadi kilichotokea dodoma kila mtu anakijua kwa sababu CCM walishtuka kuwa tunakoelekea tutakuja kulaaaniwa na vizazi vyote vijavyo vya watanzania kwa sababu hawa watu sio watu wazuri na hawana nia njema na mama Tanzania ikabidi kutokana na hali ilivokuwa waseme inatosha na lazima kweli ya haki ishinde dhidi ya fedha chafu.

Wakamkata na wakaamua kumchukua mtu aliyekuwa hana makundi, hajawekwa na wenye fedha na hana wa kumlipa fadhila wakati atakapokuwa anaendesha nchi yaani John Pombe Magufuli mambo yakatulia.;

Kwa upande wa hawa watu kibaya zaidi hawakuwa na plan b kwa upande wa CCM, walitawanyika ila kiongozi wao na mtu wao kwa sababu yeye nia yake kuu ni kuingia magogoni tu wakasema lets go the other side. Walijua wanayo pesa na wanayo pesa na kiukweli kwa upande huo hamna anayeweza kushindana nao, wakaenda kuwashawishi viongozi wa upinzani. Kuna taarifa zinasema kuwa walikubaliana kugharamia kampeni yote kuanzia uraisi hadi ubunge ya upande wa pili, walikubaliana kuwawezesha upande huo kifedha na viongozi wa upande huo waliwekwa sawa kifedha.

Ukiliangalia hili suala juu juu unaweza kufikiri ni jambo la kawaida sana ila hapana. Kuna kitu hapa ambacho watanzania lazima waamke na wakione nacho ni hadi hawa wameweza kuingiliwa na fedha???????

Katika dunia ya leo mwanasiasa anatakiwa awe mtu predictable na asiwe mnafiki kiasi ambacho mtu aliyempa kura anatakiwa awe na uhakika nae kuwa nilimpa kura huyu mtu kwa sababu anaamini katika A, B, C na hizo ndo zilizonishawishi mie kumuamini na kumpa nafasi kwenye akili yangu.

Mwaka 2007/8 Chama kilichojijengea sifa kubwa nchini Tanzania Chadema kilitoa kile kilichoitwa The list of Shame ambapo walitoa majina ya watu 11 wao waliowataja kuwa ni mafisadi, wanaolitafuna taifa na kuliangamiza taifa. Walisema kuwa wana ushahidi kamili usio na shaka juu ya hawa watu na kama hawa watu wanabisha waende mahakamani. Walisema hawa watu hawastahili kuwa mitaani sehemu wanayostahili kuwa ni jela. Na hiki ni kitu kilichowapa public trust ya kiwango cha juu kabisa, hiki ni kipindi ambacho chadema ndo ilianza kujijenga mioyoni mwa watanzania kuwa ni wakombozi wa kweli, watu wanaongea ukweli, sio waongo na yote wanayosema ni kweli tupu kwa hiyo ndo watu wanaostahili kupewa nchi.

Chadema hawakuishia hapo walizunguka nchi nzima kwenye mikutano na kampeni mbalimbali wakiendelea kuitaja iyo THE LIST OF SHAME, ambayo no 9 alikuwapo Edward Lowassa.

Sio huyo tu washirika wa Lowassa yaani mzee wa vijisenti na the Kings Maker Rostam Azizi washawai kutajwa na Chadema kuwa ni watu mafisadi na wasiofaa.

Kichwa cha mada kinasema ni ulaghai, unafiki na uzandiki kwa sababu pamoja na hiki chama kumtaja huyu mtu ila viongozi wao wamekula matapishi yao wenyewe na leo wamempokea huyu Lowassa na wanamnadi kuwa ni mtu safi, mwenye weredi na anayefaa.

Kuna kitu kimekuwa kikiendelea kwa hawa viongozi kutoa majibu mepesi eti siasa ni dynamics na sio static eti mtu unaweza kubadirisha gia angani wakifikiri watanzania ni mambumbumbu sana kiasi ambacho hawawezi kuhoji na hawafuatilii mambo yanayofanyika duniani huko.

Napenda kuwaambia viongozi wa Chadema kuwa katika siasa za 21st century mwanasiasa akisema jambo alafu ikitokea otherwise au ikitokea tofauti na alivosema au kuuaminisha umma uwa anajiuzuru. Mfano wa haya ni kama ilivotokea juzi Scotland pale waziri mkuu na kiongozi wa chama cha Scotish National Party alipojiuzuru nafasi zake zote baada ya kile kitu alichokuwa akiwaaminisha wascotland kuwa nchi yao inafaa kujitenga kufeli kwenye referundum. Sio huko tu hata England Ed Milband nae baada ya chama chake kushindwa kwenye kushawishi kitokana na sera zake alibidi ajiuzuru. Huu ndo ustaarabu mpya kwenye siasa kwa kifupi siasa za dunia ya leo ni kuwa endapo mwanasiasa ukisema jambo fulani lile jambo likija tokea tofauti na ulivouaminisha umma au chama chako inabidi ujiuzuru.

Sasa kwa Chadema na ukawa what thet were supposed to do ni kuwa kabla Lowassa hajatambulishwa rasmi au soon after kutambulishwa wale viongozi wote waliokuwa wanauaminisha umma na kudai wana ushahidi juu yake kuwa ni fisadi walitakiwa kula matapishi yao kwa wao kujiuzuru nyadhifa zao zote ndani ya chama chao na kuomba msamaha kwa jamii ya Tanzania kwa upotoshaji mkubwa walioufanya.

Ila kwa majibu mepesi wanayoyatoa kama aliyatoa jana Mchungaji Msigwa kwenye kipindi cha Madamoto, kama aliyoyatoa Lema au kama aliyoyatoa Lissu na ziadi na zaidi kama aliyoyatoa mwenyekiti wao Freeman Aikael Mbowe wakati anamkaribisha Lowassa basi its obvious kuwa HUU NI ULAGHAI, UNAFIKI NA UZANDIKI ULIOTUKUKA.

Nakataaa kudharauliwa na viongozi wa ukawa kuniona mie siwezi kufikiri ila wao ndo wanaweza kufikiri kwa niaba yangu.....

Tukutane Oktoba.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATANZANIA.
 
Mkuu Guus nafurahi kwamba kwa kiasi fulani umenielewa. Wachangiaji wengi wamejikita kunipa maana ya mfumo ambayo kimsingi siyo hoja yangu. Hoja yangu hapa ni kwamba,huo mfumo ni kitu gani!?? Lowassa alikuwa mtendaji mkuu wa serikali na msimamizi mkuu wa shughuli za serikali bungeni. Alifanya nn kuonyesha kwamba alikuwa anakerwa na huo mfumo!!? Kibaya zaidi nae ni mtuhumiwa wa ufisadi,ukiacha richmond,alishatiliwa mashaka kitambo juu ya utajiri wake.

Tukirudi kwenye hoja yangu,km huyu ambae alikuwa ktk huo mfumo,amepokelewa huku ambako watu walikuwa wameanza kupata matumaini ya kubadili maisha ya watanzania. Anakuja huku anasemwa hana tatizo na anapewa nafasi kubwa kabisa ya kuwa mgombea urais. Nini kitakachomfanya asiendelee kuukumbatia huo mfumo-ccm!!?? Hatuwezi kusema tatizo ni mfumo eti tatizo siyo watu! Wakati mfumo si kitu kinachojiendesha na kujisimamia chenyewe. Mfumo unasimamiwa na watu ni lazima tuwakatae hao ili kuweka nidhamu.

Kule uchina kiongozi akituhumiwa,anaachia ngazi,then anachunguzwa,akithibitishwa kashiriki kwenye ufisadi ananyongwa! Km tunachukulia umaarufu wake ili kupata serikali,kwa nini tusiseme hawa nao ni wale wale!!??
jaribu kufikiria ni mifumo mingapi ingebadilika kama ccm wangeikubali rasimu ya katiba ya wananchi? katiba hiyo ingelazimisha kubadilisha mifumo mingi ovu ya ccm, lakini ccm, kwa kujua kwamba uovu wa mifumo yake, na wa serikali yake, ndo unaoitegemeza, wasingekubali katu katu katiba hiyo ipite.

Kitendo kimoja tu cha lowassa, kwa kushirikiana na cdm/ukawa, kukubali kuwa, mara baada tu ya kukamata dola, wataipitisha katiba ya wananchi, kitendo hicho chenyewe tu kitabadilisha kabisa aina ya mifumo inayoongoza na kutawala nchi yetu.
 
akili yako wewe ndo ya kukaangia kashata.

wanaohama ni watu hauhami mfumo. tatizo lako huelewi. wanaohama wanahama na katiba, sera, kanuni na taasisi za ccm? katiba mbovu ya sasa ya nchi, ambayo ndo baba na mama anayezaa mifumo ovu yote ya ccm, ndo itakayotumika chini ya uongozi wa cdm na ukawa?

tutashirikiana na lowassa kubomoa mfumo ovu wa ccm na kuweka mfumo safi. tutaanza na KATIBA YA NCHI.
Hapa ndo najua hii nchi kwa nn ipo hivi hadi leo. Mkuu Lowassa akishinda anakuwa Rais wa nchi,akina mbowe watakuwa chini yake,yaani unachosema hapa lowassa akishinda waanze kumuomba abadili mfumo uliopo si ndicho unachomaanisha!!?? Akikataa mawazo yao itakuwaje na anauwezo hata kuwaacha kwenye baraza lake la mawaziri. Watafanya nini akina mbowe na wenzie wa ukawa?? Watarudi kwetu tena kutuambia huyu jamaa hafai?? Mimi ningewaelewa km lowassa angekuja chadema kuongeza nguvu tu lkn asigombee urais. Huo unaouita mfumo haujisimamii wenyewe,unasimamiwa na watu. Hao watu ndo hao hao wanatumia kila aina ya ujanja waendelee kuukumbatia. Amini usiamini lowassa akija kuwageuka chadema,chadema ndo itakuwa imezikwa haitaaminika tena!
 
Nadhani unachanganya mambo Katiba sio mfumo bali ni mkataba wa mamlaka ya serikari na wananchi unaoelezea mipaka ya serikari na jinsi nchi itavyo endeshwa ikifafanua limitations za powers za serikari, uhusiano wa mamlaka za serikari katika kutekeleza azima ya uongozi na kusimamia, mgawanyo wa majukumu na haki za wananchi katika nchi husika.

Namna gani chama tawala inasimamia hizo administration za serikari katika kufikia malengo ya kisera, bunge linavyosimamia serikari na mahakama pamoja na taasisi zake zingine za kisheria zinavyolinda sheria za nchi na kuakikisha kila kitu kinafanyika ndani ya mipaka ya katiba na sheria za bunge ndio mfumo.

Kwa hivyo mfumo umegawanyika katika sehemu tatu kuu serikari kuu (taasisi ya raisi na baraza lake la mawaziri pamoja na vyombo vinavyosadia kusimamia uendeshawaji wa shuhuli za serikari kwa na namna ya watchdogs kama ewura, CAG, TBS, etc pamoja na idara za serikari zilizoko chini ya mamlaka ya wizara), pili bunge linalo isimamia serikari pamoja na kuleta hoja za wananchi bungeni kuhusu mahitaji yao, kutunga sheria za nchi na kusimamia maslahi ya wananchi na accountability ya serikari i.e mawaziri, watchdogs and idara za serikari azifanyi mambo kiholela, tatu judiciary ie mahakama na vyombo vya sheria kama polisi, takukuru etc, ambavyo vipo kuakikisha vitu vinafanywa kisheria na sheria zenyewe azipo kinyume na mkataba wa wananchi na serikari (katiba) to ensure checks. Hayo ni kwa ufupi lakini kuna mambo mengi sana katika kila mhimili unaovyanya kazi zake kuakikisha efficiency zinapatikana ikiwemo maadili ya watumishi, sheria za sehemu na upeo wa wasimamizi wenyewe.

Kwa hivyo mfumo mmbovu unatokana na mambo mengi sana na unaweza kosolewa na chombo chochote cha usimamizi CAG katika shughuli zake anaweza kosoa udhaifu wa usimamizi wa mapato na akatoa sababu zake, bunge linaweza kosoa mfumo wa wizara fulani kwenye mechanism za kutekeleza sera na kuonyesha upotefu wa mapato, hiyo sera isivyo wafikia kundi fulani au kupitia kamati zake inaweza kuona mfumo wa tender unaoleta ufisadi, conflict of interest, mahakama zinavyochelewa kutoa haki au adhabu kwa wakosaji etc.

Mahakama nayo inaweza ona sheria fulani za nchi sio sahihi kikatiba, sehemu zake zingine zinaweza kuwa poorly funded kama polisi walivyo katika kuhakikisha wezi wanapelekwa sehemu husika na usimamizi imara wa sheria za nchi, wezi serikarini awalindwi etc.

Mwenye jukumu la mengi ya yote hayo ni chama tawala kwa sababu wao ndio wasimamizi wakuu na wenye mamlaka ya kuakikisha kila kitu kipo katikaa ubora wake na kila taasisi ina deliver accordingly as stated by their function, sasa kama CAG kutokana na mamlaka yake akisema sehemu fulani nimekutana na hiki na bado hakuna maamuzi the bulk stop with the responsible authorities to change things inaweza kuwa kubadilisha sheria, waziri, mkurugenzi wa shirika, namna bora ya usimamizi or even more investment depending on the nature of the highlighted problem.
japo umejichangachanganya lakini kimsingi umeeleza vizuri sana maana ya mfumo.

kifupi hapo kwenye red huo ndo mfumo lakini ni mfumo daraja la pili kwa maana ya kuwa zao la mfumo daraja la kwanza, mfumo mama, ambao ni KATIBA ya nchi.

mfumo huo kwenye red unawekwe/ unaundwa/ unatengenezwa na mfumo mkuu ambao ni katiba. Katiba ndo inayotakiwa iseme serikali(executive) iweje, ifanye kazi zipi kwa namna gani, kwa mamlaka yepi, iwajibishwe vipi nk nk, vivyo hivyo kwa Bunge(legislature) na Mahakama (Judiciary). Ukiwa na Katiba mbovu, Mfano katiba ambayo inaipa serikali(executive/Rais) nguvu za kupitiliza mfano Rais kuwa na uwezo wa kuteua na ku fire the executive almost yote, tena wakati mwingine at will tu bila kufuata sheria, Rais kuteua Judiciary, Rais kuteua sehemu ya Legislature na yeye mwenyewe kuwa sehemu ya legilsature ndo haya unayoyaona ya watu kuiba (kosa la jinai) badala ya kushtakiwa wanaambiwa tu warudishe walichoiba na mambo yanaisha.

Katiba YA nchi ndo ama itasema, au itaweka msingi wa kutengeneza subdelegation itakoyoelekeza huyo CAG ateuliwe vip, afanye kazi zake kivip aripot kwa nan nk. Kama CAG kazi yake ni kufuatilia utendaji wa serikal utategemea vip atende vema ikiwa serikali hiyo anayoikagua ndo hiyo hiyo inayomteua, inamlipa na ndo ina mamlaka ya kumfukuza kwa kadri itakavoona inafaa?! Tungetegemea mfumo mama (Katiba) mathalan uielekeze kwamba CAG ateuliwe na executive(Rais) lakini uteuzi wake uwe approved na legislature na ikibidi kumfukuza au kumbadilisha au kubadilisha maslahi yake kwa namna yoyote ile basi isifanyike bila idhini ya bunge, na aripoti kwa bunge na si kwa rais ambaye naye anaweza kuwa mtuhumiwa

tunataka mfumo ambao wananchi ndo wenye mamlaka ya mwisho na si mtu mmoja tu kama Rais(executive) ndo analundikiwa mammlaka yote ya nchi. Katika hali kama hii ya sasa siku tukipata Rais mwendawazimu tutapona kweli??!!
 
Back
Top Bottom