Hivi karibuni naongeza idadi ya single mothers mtaani

Hivi karibuni naongeza idadi ya single mothers mtaani

Hana adabu tu hakuna cha kusumbuliwa na mimba.

Umejitahidi uvumilivu....kwasababu u mvumilivu na waswahili husema mvumilivu hula mbivu vumilia mzee.
Mimi mwenyewe nimeona tu kwamba hana adabu mkuu. Nimemvumilia sana
 
Mkuu vumilia mbna me nakula mke wa mtu mtarajiwa kila siku an, ile mimba inanipenda balaa hta sa10 usku akimiss anakuja freshy.
Angalia wakikukamata watakuumiza
 
Changamoto ndogo sana hizo wakati wa ujauzito.
Usimwache.
 
Whatever, kama kosa ulishalifanya tangu day one unaanzisha mahusiano na huyo binti. If so, jaribu kukubaliana na matokeo ya ulichokifanya....

Usimshit huyo binti, remember ana mimba yako. Cha kufanya we jifanye mjinga tu, ungalie ni vipi utaweza kurescue hali yake.
Sawa boss ngoja nione namna
 
Huyo binti ni mimba ndio inamfanya awe hivyo kwa kiasi kikubwa. Vitu kama hasira malumbano ni kitu ambacho wanakuwa nacho baadhi ya Wanawake wakiwa na mimba.So hulka yake ukiongeza na hiyo hali unakuta anakuwa hivyo. Mvumilie itaisha, Kwani kabla ya mimba alikuwa hivyo?Think twice
 
Basi ndio maana.....bado mdogo hata kiakili ukichanganya na mimba ya kwanza ndio anakua hivyo. Mvumilie tuu maana ana mtoto wako, na ulishasema kuwa ulikua na mpango wa kumuoa.

Ndoa ndio ziko hivyo na hapo ndio uanze kupata somo mapema. I hope akijifungua atatulia akili and she will be matured enough for the sake of you and your baby.

Pole sana kwa changamoto unazokutana, ukisikia ukubwa dawa ndio hivi sasa. Na hongereni sana pia kwa future baby.
 
Utakua mpumbavu zaidi ya huyo dem wako kama utaruhusu mtoto wako akalelewe na single mother au kidume kingine akulelee mtoto wako

Pia inabidi uelewe kwamba wanawake wakiwa kwenye kipindi cha ujauzito huwa wanabadilika sana kitabia. Kwenye kila kitu yy anakua anatafuta kosa tu kama unavyosema kwamba usipopokea simu anadhan uko na machangudoa.

Lastly, fatilia kama kweli hio mimba ni yako au anakuhadaa tu coz hawa madem wanaweza kuwa wanajua mhusika wa mimba lkn bado wakakufanya uhisi kama mimbavni yako kumbe anataka mahitaji kutoka sehemu zote mbili. Coz dem mwenye akili hawezi kumkataa mwenye mimba bila sababu unless huyo dem awe chizi
Ukijishusha Mateso yanazidi...... Ifike mahali wanaume tuache kufa mapema kwa misongo ya mawazo yasio kuwa na maana




Ushauri wangu kwa mwana kama mbwai na iwe mbwai..... Fanya maamuzi magumu kwa Usalama wa nafsi na akili zako
 
We bado hujakomaa mwenzio ana ujauzito tena wa kwanza una mdrive crazy na wewe unaenda nae hivyo hivyo hatimae unataka kuachana nae.Kwanza tambua huyo anakupenda kweli na ndiyo maana ana wivu mkali sana na wewe na anajua umemtundika li mimba ili um dump amejawa na hofu ambayo kwa sasa ndiyo inayozaa mawivu yenye mifarakano ya kitoto.
SO USHAURI WANGU MPE SUPPORT KWA SABABU YUPO KWENYE HALI YA UJAUZITO ILI UMCHECK BAADA YA KUJIFUNGUA.
Endelea kusema ujauzito hauja komaaa kumbe mwenzio hajui ujauzito ni wa nani na ampe nani....... Mwangu fanya kama ulivyo amua
 
Oya fanya kama ulivyo amua.... Unaweza ukijifanya umejishusha yaishe kumbe mwenzio hajui nani babe wa mtoto........ Hawa wanawake malofa sana.... Hata mimi ninapitia story kama yako na ni mwana chuo hivo hivo......

Usiliamini chozi la mwanamke. Uamuzi ulio uchukua ni wa kiume.

#ukijishusha Mateso ndio yatazidi
Nilimrudia sababu ya mimba mkuu sikuona kama ana msaada mwingine
 
Wakuu salam

Ni hivi, huyu binti nimekuwa nae kwenye mahusiano nilipokuwa chuoni, yeye pia akiwa chuo, makubaliano yetu ilikuwa ni kuja kufanya maisha pamoja, nikimaanisha kuoana, hivyo basi nililenga angalau kuwepo na utangulizi wa mimba tu ndio mengine yaendelee, maana siko tayari kuishi na mtu ambaye sitaweza kutengeneza nae familia,kunipatia watoto, kwa maana madada wengi siku hizi wanachezea vizazi wanatoa mimba sana sipendi nimuoe halafu ndio nigundue kwamba hawezi nipatia watoto na nimeshamuoa.

Nikazungumza nae tukapanga kuwa mwezi wa tisa baada ya chuo utaratibu wa mimba ufanyike, baada ya hapo nimtambulishe nyumbani kama mchumba na taratibu nyingine ziendelee, ila katika kufanya mapenzi mimba ikashika mwezi wa 5 akaniomba tuitoe ili mwezi wa tisa ubaki palepale, nikakatalia kabisa, alilazimisha sana, ikabidi nimtafutie watu wa kumshauri asitoe, basi ikawa usumbufu hivyo tukitofautiana kidogo anasema tuachane, siku moja alipiga simu akakuta iko busy akasema ninamsaliti japo nilimueleza kuwa si kweli nilikuwa naongea na mzazi, hakutaka anisikilize alisema mahusiano yaishe nisimtafute wala kumsumbua na wala mimba nisiiulizie, na wala nisishiriki chochote ataamua atakalo, ilikuwa kipindi cha mitihani nikatuliza akili yangu nikafanya mitihani yangu muda kama wa wiki tatu, akanitangulia kumaliza mitihani, akaenda nyumbani kwao, hapo mimba ikiwa na miezi minne, akaenda nyumbani, nilipomaliza mtihani nikamtafuta akasema amepata mtu wa kuilea mimba hivyo nisimsumbue, mimi hawezi kunitambulisha kama baba wa mtoto maana hatuendani, akaniblock kote sms, calls,whatsapp nikawa simpati!

Baada ya week mbili kupita, nikaona kanitoa block kote akanisms anaumwa sana na maji yanamtoka ukeni hajui ni ya nini, basi ikabidi nimchukue tu nimpeleke hospital kwanza atibiwe na kucheck afya ya mtoto kwenye ultrasound, mtoto alikuwa salama yeye alikuwa anasumbuliwa na homa, alipopona akaniambia kuwa anaomba kuwa nimsaidie pesa ya mahitaji ale anachojisikia, maana vyakula havipandi vya nyumbani, anashinda njaa muda mrefu, nimnunulie na nguo pana za kulelea ujauzito, nikamuuliza lakini si ulisema una mtu anayekulea na ujauzito, yuko wapi hadi ukose vyote hivyo, akasema ilikuwa si kweli yale maneno, nikapotezea hilo jambo nikamtimizia alilohitaji, hapo mimba ina miezi mitano na nyumbani kwao hawafahamu...nikamwambia asijali nitafanya utaratibu kuongea na wazee ili tuje pale nyumbani nifahamike kwanza, ndio awaambie ana mimba yangu ili asigombezwe na kulaumiwa sana...akasema kama sitafanikiwa kwenda mimi kwao ili nyumbani aruhusiwe kuja kujifungulia nyumbani kwetu, ataondoka aende mbali, akajifungulie mbali mkoa mwingine ambapo rafiki yake amepanga getto huko, nikamwambia haitashindikana atakuja aje kujifungulia nyumbani, huko sitaki aende ni mbali ya uangalizi wangu kwa mtoto.

Nikawaambia wazazi kuwa nina mchumba nahitaji tuanze taratibu za kwenda kutoa kishika uchumba, ili aweze kuruhusiwa kutoka kule aje kujifungua huku, maana yeye alisema kujifungulia nyumbani ni aibu hawezi, wazazi wakakubali tukapanga tarehe (Mwisho wa Mwezi huu wa 10). Mimi na yeye mahusiano yakaendelea kama kawaida hivyo namjali nampa anachohitaji, clinic nampeleka, ikafikia mahali akasema anahitaji nimsaidie mtaji afanye biashara ndogo ndogo, nikampa, nikamnunulia simu mpya..yaani kwa kifupi nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kutimiza mahitaji yake.

Jumamosi iliyopita nilikuwa kwenye ibada mida ya jioni, akapiga simu sikupokea, nikamsms kwamba nipo kwenye ibada siwezi ongea, akatuma sms kwamba si kweli, nafanya drama, nilivyomaliza nikamcheck nikaongea nae ila hakuwa anajibu vzuri siku nzima ya jumapili haikuwa nzuri, Jumatatu ya juzi ilipaswa tuamkie kwenda clinic, akakataa kwenda, nilikasirika nikamwambia "Una Maamuzi Ya Kipumbavu" akajibu Kama unataka kwenda, Kusanya vichangudoa vyako uende navyo" basi akaanza kusema kuwa namdharau na kumtukana, simthamini na hiyo mimba anataka aitoe tu maana ananiona ni mtu nisiyemjali na kumuheshimu, kwahiyo tuachane na wala nisiulizie chochote kuhusu mimba maana ameshasema tuachane, na hata mtoto nisiulizie, kwetu pia hawezi kuja aje aishie kuwa housegirl,kama kulea anaweza kulea mwenyewe bila kunishirikisha mimi lolote, na hata nikitaka pesa zangu zote nilizompa arudishe yupo tayari, nikamwambia kaa nazo...kuhusu suala la mimba sijajua atafanya nini akiamue kuzaa na azae, akiamua kutoa na atoe, nimefika uwezo maximum wa kumhandle, potelea mbali, mimba ina miezi mitano sasa.

I do not care anymore.

Ndio nimeamua hivyo wakuu, au mnasemaje.
Bro
Hizo ni athari za mimba. Fikiri upya na endelea naye. Pindi akishusha injini, kila kitu kitakuwa kipya. Hata hivyo hiyo ni probability ya 90% tu. Kuna hiyo 10% iliyobaki inaweza leta balaa

Bazazi
 
Hayo tu!!! Wewe anza kujiandaa kupokei kiumbe hicho .
 
Kumbe 22 yrs unakuja kulia lia hapa, mvumilie ajifungue halafu pima upya tabia yake lakini mi naona ni changamoto za ujauzito tu.
 
Bro
Hizo ni athari za mimba. Fikiri upya na endelea naye. Pindi akishusha injini, kila kitu kitakuwa kipya. Hata hivyo hiyo ni probability ya 90% tu. Kuna hiyo 10% iliyobaki inaweza leta balaa

Bazazi
Ngoja tuone maana anatishia kutoa
 
Bazazi ameshaleta mrejesho wa ongezeko la SINGOMAZA, na wewe unaongeza tena!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom