Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,197
- 25,516
Kumekuwa na mfananisho kwa namna ya kuwapambanisha ili kumpata mbabe kati ya Ndugu Kabwe Zuberi Zitto Zitto Kabwe) na @Dr.W.P.Slaa. Kwamba eti Zitto kupitia kwa wanaomuunga mkono, wanaweza 'kumtisha'/'kumtingisha' @Dr.W.P.Slaa. Si kitu rahisi. Kisiasa, Zitto ni mchanga sana kwa Dr.W.P.Slaa. Nasema hivi nikiwa na maana yangu.Nina sababu za kukazia maelezo yangu na imani yangu juu ya jambo hilo nilisemalo.
Kwanza, uzoefu wa uongozi. Nizungumzie Ubunge tu. Dr.Slaa amekuwa Mbunge wa Karatu kuanzia mwaka 1995 hadi 2010 alipogombea Urais kupitia CHADEMA. Amekuwa Mbunge wa Jimbo kwa miaka 15. Yaani, ni mara tatu ameaminiwa na chama chake na amechaguliwa na wananchi wake. Zitto amekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini tangu mwaka 2005 hadi sasa. Hadi mwaka 2015, atatimiza miaka 10 ya Ubunge wake.Ameaminiwa na chama chake na kuchaguliwa na wananchi wake mara mbili. Kwa hapo, Dr. Slaa anaongoza.
Pili, umachachari Bungeni kama Mbunge wa Upinzani. Wote hapa wana alama zinazokaribiana. Wakati Zitto akiibua kashfa ya Buzwagi, Dr. Slaa aliripua jambo jipya kila alipokuwa akichangia au kuuliza swali. Nafasi ilikuwa ikifika kwa Dr.Slaa, Mawaziri,Wabunge na wanachi walikaa mkao wa kula. Walijua kuna la maana linafuata. Hata Zitto naye. Kwa hili, niseme nguvu ni sawa.
Tatu, umachachari nje ya Bunge. Hapa Zitto simpi alama nyingi.Ingawa amekuwa akihutubu mikutano na makongamano tofauti, lakini nje ya Bunge hakuwa muibuaji wa mambo mazito ya kinchi.Lakini, Dr.Slaa ndiye aliyeibua 'issue' ya External Payments Account (EPA) na kuisimamia.Pia,Dr.Slaa ndiye liyesimama Mwembeyanga-Temeke na kutaja Orodha ya Watanzania 11 aliowaita 'Mafisadi'. Mmoja baada ya mwingine anajidhihirisha.
Nne, ukaribu na wana-CCM. Kuna habari kuwa Zitto ana ukaribu sana na viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali yake.Inasemwa pia kuwa Zitto ni swahiba wa Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa. Urafiki huu unaonekana kama uliozidi na kuvuka mipaka ya kiupinzani. Kuhusu urafiki wa namna hii,Dr. Slaa ndiye nguli katika hili.Yeye kuanzia mwaka 1974 alikuwa karibu na Uongozi wa juu wa TANU ppale ambapo alikuwa Katibu wa TANU-youth League pale Seminarini Kipalapala-Tabora(sijui hapa wadini watasemaje).
Kama hiyo haitoshi, Dr.Slaa alikuwa Katibu wa CCM kwenye Tawi la Rome-Italia. Kwa kufanya hivi, Dr.Slaa alikuwa karibu na vigogo wa TANU na baadaye CCM akiwemo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa Mwenyekiti wa TANU na baadaye CCM kwa wakati huo. Dr.Slaa aliendelea kuwa mwanachama mtiifu wa CCM hadi alipojiondoa huko na kujiunga na CHADEMA hapo 1995.
Katika kigezo hiki cha urafiki na ukaribu Dr.Slaa natia fora.Lakini, sasa yeye ni mpinzani kama alivyo Zitto ambaye hakuwahi kuwa katika chama tawala tangu kuzaliwa kwake. Sasa, kwanini Zitto atiliwe shaka na Dr. Slaa aachwe? Kila mmoja wetu na ajijibu.
Ninachotaka kusema hapa ni kuwa ingawa wote: Dr.Slaa na Zitto ni wanasiasa lakini hawa ni wa ngazi tofauti. Mmoja yuko juu ya mwingine. Dr.Slaa anamzidi Zitto kwa vitu vingi vikiwemo hivyo nilivyojaribu kuviainisha hapo juu. Sasa, ulinganifu na uchonganishi wa wawili hawa hauna nafasi. Ni kwakuwa hawafanani. Mmoja ni mfano wa mwingine.Ni Mwalimu.
Hakuna haja ya kuonesha kuwa Zitto na wafuasi wake ndani na nje ya CHADEMA wanamtisha Dr.Slaa. Nadhani imeonekana. Dr.Slaa,pamoja na propaganda na vitisho vyote, ameendelea na ziara yake mkoani Kigoma ikiwa pamoja na Jimbo la Uchaguzi la Zitto(nyumbani kabisa)-Jimbo la Kigoma Kaskazini. Kwa uzoefu wa kisiasa alionao Dr.Slaa, si Zitto wala awaye yeyote nayeweza kumtisha kisiasa Dr.Slaa. Waswahili wana msemo kuwa: 'Nyani Mzee amekwepa mishale mingi'. Zitto anayo nafasi ya kuendelea na siasa na kukomaa kama Dr.Slaa. Yawezekana!

Last edited by a moderator: