Hivi Kabwe Zuberi Zitto wa kumtisha Dr.Wilbrod P. Slaa!? Haiwezekani!

Status
Not open for further replies.

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,192
25,493
Kumekuwa na mfananisho kwa namna ya kuwapambanisha ili kumpata mbabe kati ya Ndugu Kabwe Zuberi Zitto Zitto Kabwe) na @Dr.W.P.Slaa. Kwamba eti Zitto kupitia kwa wanaomuunga mkono, wanaweza 'kumtisha'/'kumtingisha' @Dr.W.P.Slaa. Si kitu rahisi. Kisiasa, Zitto ni mchanga sana kwa Dr.W.P.Slaa. Nasema hivi nikiwa na maana yangu.Nina sababu za kukazia maelezo yangu na imani yangu juu ya jambo hilo nilisemalo.

Kwanza, uzoefu wa uongozi. Nizungumzie Ubunge tu. Dr.Slaa amekuwa Mbunge wa Karatu kuanzia mwaka 1995 hadi 2010 alipogombea Urais kupitia CHADEMA. Amekuwa Mbunge wa Jimbo kwa miaka 15. Yaani, ni mara tatu ameaminiwa na chama chake na amechaguliwa na wananchi wake. Zitto amekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini tangu mwaka 2005 hadi sasa. Hadi mwaka 2015, atatimiza miaka 10 ya Ubunge wake.Ameaminiwa na chama chake na kuchaguliwa na wananchi wake mara mbili. Kwa hapo, Dr. Slaa anaongoza.

Pili, umachachari Bungeni kama Mbunge wa Upinzani. Wote hapa wana alama zinazokaribiana. Wakati Zitto akiibua kashfa ya Buzwagi, Dr. Slaa aliripua jambo jipya kila alipokuwa akichangia au kuuliza swali. Nafasi ilikuwa ikifika kwa Dr.Slaa, Mawaziri,Wabunge na wanachi walikaa mkao wa kula. Walijua kuna la maana linafuata. Hata Zitto naye. Kwa hili, niseme nguvu ni sawa.

Tatu, umachachari nje ya Bunge. Hapa Zitto simpi alama nyingi.Ingawa amekuwa akihutubu mikutano na makongamano tofauti, lakini nje ya Bunge hakuwa muibuaji wa mambo mazito ya kinchi.Lakini, Dr.Slaa ndiye aliyeibua 'issue' ya External Payments Account (EPA) na kuisimamia.Pia,Dr.Slaa ndiye liyesimama Mwembeyanga-Temeke na kutaja Orodha ya Watanzania 11 aliowaita 'Mafisadi'. Mmoja baada ya mwingine anajidhihirisha.

Nne, ukaribu na wana-CCM. Kuna habari kuwa Zitto ana ukaribu sana na viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali yake.Inasemwa pia kuwa Zitto ni swahiba wa Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa. Urafiki huu unaonekana kama uliozidi na kuvuka mipaka ya kiupinzani. Kuhusu urafiki wa namna hii,Dr. Slaa ndiye nguli katika hili.Yeye kuanzia mwaka 1974 alikuwa karibu na Uongozi wa juu wa TANU ppale ambapo alikuwa Katibu wa TANU-youth League pale Seminarini Kipalapala-Tabora(sijui hapa wadini watasemaje).

Kama hiyo haitoshi, Dr.Slaa alikuwa Katibu wa CCM kwenye Tawi la Rome-Italia. Kwa kufanya hivi, Dr.Slaa alikuwa karibu na vigogo wa TANU na baadaye CCM akiwemo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa Mwenyekiti wa TANU na baadaye CCM kwa wakati huo. Dr.Slaa aliendelea kuwa mwanachama mtiifu wa CCM hadi alipojiondoa huko na kujiunga na CHADEMA hapo 1995.

Katika kigezo hiki cha urafiki na ukaribu Dr.Slaa natia fora.Lakini, sasa yeye ni mpinzani kama alivyo Zitto ambaye hakuwahi kuwa katika chama tawala tangu kuzaliwa kwake. Sasa, kwanini Zitto atiliwe shaka na Dr. Slaa aachwe? Kila mmoja wetu na ajijibu.

Ninachotaka kusema hapa ni kuwa ingawa wote: Dr.Slaa na Zitto ni wanasiasa lakini hawa ni wa ngazi tofauti. Mmoja yuko juu ya mwingine. Dr.Slaa anamzidi Zitto kwa vitu vingi vikiwemo hivyo nilivyojaribu kuviainisha hapo juu. Sasa, ulinganifu na uchonganishi wa wawili hawa hauna nafasi. Ni kwakuwa hawafanani. Mmoja ni mfano wa mwingine.Ni Mwalimu.

Hakuna haja ya kuonesha kuwa Zitto na wafuasi wake ndani na nje ya CHADEMA wanamtisha Dr.Slaa. Nadhani imeonekana. Dr.Slaa,pamoja na propaganda na vitisho vyote, ameendelea na ziara yake mkoani Kigoma ikiwa pamoja na Jimbo la Uchaguzi la Zitto(nyumbani kabisa)-Jimbo la Kigoma Kaskazini. Kwa uzoefu wa kisiasa alionao Dr.Slaa, si Zitto wala awaye yeyote nayeweza kumtisha kisiasa Dr.Slaa. Waswahili wana msemo kuwa: 'Nyani Mzee amekwepa mishale mingi'. Zitto anayo nafasi ya kuendelea na siasa na kukomaa kama Dr.Slaa. Yawezekana!
 
Last edited by a moderator:
Umenena vema sana mkuu..

Sie watu wa Musoma tunasema "ukiona mshindani wako kakufuata mpaka kwenu, basi jua pambano limekushinda"
 
sijamaliza kusoma maelezo marefu mno au kuna mtu unamwandikia barua bahati mbaya ndo umeposti hapa?
 
Zitto anapaswa kupambanisha na mimi ambaye sijashika hata uenyekiti wa familia wa CHAMA, ila namshinda kwa kila kitu. Kuanzia akili, hekima, nk. Zitto kanishind moja tu UNAFIKI na UBINAFSI.
 
Toka lini sikio likazidi kichwa? toka lini govi likawa na thamani dhidi ya mshoroboko wenyewe?kutahiri kunafaida kubwa kwa afya ya akili na mwili...si vema kumfananisha mchumia tumbo dhidi ya mzalendo mwanamapinduzi wa kweli...
 
Na ukiangalia umri wao wakati ZzK ana umri huo Katibu katika umri kama huu alikuwa ame achieve nini mkuu????!!!!!!!

Maana kashaishi miaka mingi sana hili nalo liangaliwe
 
Kumekuwa na mfananisho kwa namna ya kuwapambanisha ili kumpata mbabe kati ya Ndugu Kabwe Zuberi Zitto Zitto Kabwe) na @Dr.W.P.Slaa. Kwamba eti Zitto kupitia kwa wanaomuunga mkono, wanaweza 'kumtisha'/'kumtingisha' @Dr.W.P.Slaa. Si kitu rahisi. Kisiasa, Zitto ni mchanga sana kwa Dr.W.P.Slaa. Nasema hivi nikiwa na maana yangu.Nina sababu za kukazia maelezo yangu na imani yangu juu ya jambo hilo nilisemalo.

Kwanza, uzoefu wa uongozi. Nizungumzie Ubunge tu. Dr.Slaa amekuwa Mbunge wa Karatu kuanzia mwaka 1995 hadi 2010 alipogombea Urais kupitia CHADEMA. Amekuwa Mbunge wa Jimbo kwa miaka 15. Yaani, ni mara tatu ameaminiwa na chama chake na amechaguliwa na wananchi wake. Zitto amekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini tangu mwaka 2005 hadi sasa. Hadi mwaka 2015, atatimiza miaka 10 ya Ubunge wake.Ameaminiwa na chama chake na kuchaguliwa na wananchi wake mara mbili. Kwa hapo, Dr. Slaa anaongoza.

Pili, umachachari Bungeni kama Mbunge wa Upinzani. Wote hapa wana alama zinazokaribiana. Wakati Zitto akiibua kashfa ya Buzwagi, Dr. Slaa aliripua jambo jipya kila alipokuwa akichangia au kuuliza swali. Nafasi ilikuwa ikifika kwa Dr.Slaa, Mawaziri,Wabunge na wanachi walikaa mkao wa kula. Walijua kuna la maana linafuata. Hata Zitto naye. Kwa hili, niseme nguvu ni sawa.

Tatu, umachachari nje ya Bunge. Hapa Zitto simpi alama nyingi.Ingawa amekuwa akihutubu mikutano na makongamano tofauti, lakini nje ya Bunge hakuwa muibuaji wa mambo mazito ya kinchi.Lakini, Dr.Slaa ndiye aliyeibua 'issue' ya External Payments Account (EPA) na kuisimamia.Pia,Dr.Slaa ndiye liyesimama Mwembeyanga-Temeke na kutaja Orodha ya Watanzania 11 aliowaita 'Mafisadi'. Mmoja baada ya mwingine anajidhihirisha.

Nne, ukaribu na wana-CCM. Kuna habari kuwa Zitto ana ukaribu sana na viongozi mbalimbali wa CCM na Serikali yake.Inasemwa pia kuwa Zitto ni swahiba wa Rais Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa. Urafiki huu unaonekana kama uliozidi na kuvuka mipaka ya kiupinzani. Kuhusu urafiki wa namna hii,Dr. Slaa ndiye nguli katika hili.Yeye kuanzia mwaka 1974 alikuwa karibu na Uongozi wa juu wa TANU ppale ambapo alikuwa Katibu wa TANU-youth League pale Seminarini Kipalapala-Tabora(sijui hapa wadini watasemaje).

Kama hiyo haitoshi, Dr.Slaa alikuwa Katibu wa CCM kwenye Tawi la Rome-Italia. Kwa kufanya hivi, Dr.Slaa alikuwa karibu na vigogo wa TANU na baadaye CCM akiwemo Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa Mwenyekiti wa TANU na baadaye CCM kwa wakati huo. Dr.Slaa aliendelea kuwa mwanachama mtiifu wa CCM hadi alipojiondoa huko na kujiunga na CHADEMA hapo 1995.

Katika kigezo hiki cha urafiki na ukaribu Dr.Slaa natia fora.Lakini, sasa yeye ni mpinzani kama alivyo Zitto ambaye hakuwahi kuwa katika chama tawala tangu kuzaliwa kwake. Sasa, kwanini Zitto atiliwe shaka na Dr. Slaa aachwe? Kila mmoja wetu na ajijibu.

Ninachotaka kusema hapa ni kuwa ingawa wote: Dr.Slaa na Zitto ni wanasiasa lakini hawa ni wa ngazi tofauti. Mmoja yuko juu ya mwingine. Dr.Slaa anamzidi Zitto kwa vitu vingi vikiwemo hivyo nilivyojaribu kuviainisha hapo juu. Sasa, ulinganifu na uchonganishi wa wawili hawa hauna nafasi. Ni kwakuwa hawafanani. Mmoja ni mfano wa mwingine.Ni Mwalimu.

Hakuna haja ya kuonesha kuwa Zitto na wafuasi wake ndani na nje ya CHADEMA wanamtisha Dr.Slaa. Nadhani imeonekana. Dr.Slaa,pamoja na propaganda na vitisho vyote, ameendelea na ziara yake mkoani Kigoma ikiwa pamoja na Jimbo la Uchaguzi la Zitto(nyumbani kabisa)-Jimbo la Kigoma Kaskazini. Kwa uzoefu wa kisiasa alionao Dr.Slaa, si Zitto wala awaye yeyote nayeweza kumtisha kisiasa Dr.Slaa. Waswahili wana msemo kuwa: 'Nyani Mzee amekwepa mishale mingi'. Zitto anayo nafasi ya kuendelea na siasa na kukomaa kama Dr.Slaa. Yawezekana!

Si rahisi kutishwa na kinyago ulichokichonga mwenyewe!
 
Huyu Slaa ana miaka 65 Zitto ana miaka 35. Zitto ana miaka mingine 35 ya kufanya siasa actively. Huyu Slaa akiwa na bahati mwishoni wake 2015 pale Mbowe atakapompiku kugombea urais. Post 2015 elections Slaa hayupo katika siasa za Tanzania. Unalinganisha kinyesi na mkojo!
 
Inasemakana mmoja wao ana kadi hai ya uanachama wa chama kingine,,ulilifanyia utafiti hilo?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Zitto atakomaa ila kwasasa bado hajakomaa.

Dr Slaa anajua kila hatua za kisiasa nchi imepitia na kwa kushiriki kila upande wa chama tawala na upinzani.

Zitto atafikia kama atabadilika na kuacha kutafuta madaraka kwa nguvu bali madaraka yamtafute.

Hakuna nafasi ambayo Dr Slaa alitumia mbinu mbinu kuipata kuanzia ubunge,ukatibu mkuu na hata ugombea urais.Kote aliombwa kutumikia hizo nafasi tena akiwa na mipango tofauti.
 
muulize mukama na nape zile 90 za RA, EL na mzee wa vijisent zimekwisha lini!
 
zito amuwezi slaa ata iweje. Kupola mke wa mtu na mwenye mke kakimbilia mahakamani bado ameshindwa na mke kamkosa. Mtu wa hivyo sio wa kuwa nae karibu. Zito kuwa mpole tu slaa umuwezi
 
Huu ujinga tunaupinga sana!!!!!
Mbona huvai pad nawe si binadamu kama wanawake???!!!!!
Ukiambiwa A sema ya A sio ooonh mbona B haina ncha juu...shaiza!!!!!
 
Zitto atakomaa ila kwasasa bado hajakomaa.

Dr Slaa anajua kila hatua za kisiasa nchi imepitia na kwa kushiriki kila upande wa chama tawala na upinzani.

Zitto atafikia kama atabadilika na kuacha kutafuta madaraka kwa nguvu bali madaraka yamtafute.

Hakuna nafasi ambayo Dr Slaa alitumia mbinu mbinu kuipata kuanzia ubunge,ukatibu mkuu na hata ugombea urais.Kote aliombwa kutumikia hizo nafasi tena akiwa na mipango tofauti.

kumbe mademu ndo waliomshawishi aachane na upandri huyu afahi kuwa kiongozi maana ni laisi kushawishika
 
Huyu Slaa ana miaka 65 Zitto ana miaka 35. Zitto ana miaka mingine 35 ya kufanya siasa actively. Huyu Slaa akiwa na bahati mwishoni wake 2015 pale Mbowe atakapompiku kugombea urais. Post 2015 elections Slaa hayupo katika siasa za Tanzania. Unalinganisha kinyesi na mkojo!
Bahati mbaya nyie vijana wa Kanumba academy hamzijui kanuni za vita ( jeshini). Ni hivi, kamanda au askari wa kawaida mwenye umri wa miaka 35 lakini akatawaliwa na tamaa na usaliti dhidi ya wenzake hawezi kudumu miaka mingine 5 kabla hajapotea katika medani hiyo. Nakuambia kama huyo Zitto amefanya huo usaliti unaosemwa wallah hana nafasi tena kwenye siasa. Kama wewe au yeye mnabisha tusubiri tuone.
 
Last edited by a moderator:
zito amuwezi slaa ata iweje. Kupola mke wa mtu na mwenye mke kakimbilia mahakamani bado ameshindwa na mke kamkosa. Mtu wa hivyo sio wa kuwa nae karibu. Zito kuwa mpole tu slaa umuwezi
Hizo Bold ni kukuonyesha kuwa wewe ni ngumbaru. Unaingia kwenye mijadala isiyo saizi yako. Soma kijana acha kutumika.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom