Hivi inakuwaje mtu kasoma business administration degree halafu hawezi fungua hata genge la kuuza nyanya. A business administrate?

Hivi inakuwaje mtu kasoma business administration degree halafu hawezi fungua hata genge la kuuza nyanya a business administrate?

Genge la kuuza nyanya mtaji elfu 20

Hizo skili zake za business administration anataka akazionyeshee wapi?
Unachanganya business administration na sales management.

Lakini pia ni sawa na kuuliza unawezaje kuwa aircraft engineer huwezi hata kurusha Twin Otter, ndege ya abiria sita.
 
Unachanganya business administration na sales management.
Ukifungua genge unachofanya ni business administration sababu hufanyi sales tu

unapanga mipango ya genge,unanunua,unasimamia transport logistics ,una stock ,unauza ,unapokea na kutunza pesa za mauzo na mahesabu yake na kufanya mnaamuzi ya bei ,marketing nk
 
Hiyo inapendeza kufundishwa kuanzia ngazi ya digrii ya pili au iwe kama postgraduate ya mwaka mmoja. Tuhangaike sana na kozi za ujasiriamali, ufundi, uvuvi, kilimo, ufugaji

Sasa kijana kamaliza form 6 unampeleka miaka 3 akasomee digrii ya business administration. Akimaliza mwajiri anamuajiri kama business administrator! Ndo maana kazi zinaharibika
 
Ukifungua genge unachofanya ni business administration sababu hufanyi sales tu

unapanga mipango ya genge,unanunua,unasimamia transport logistics ,una stock ,unauza ,unapokea na kutunza pesa za mauzo na mahesabu yake na kufanya mnaamuzi ya bei ,marketing nk
Hilo ni genge la nyanya na vitunguu?
 
Wewe ni mjinga sana, Na kwa akili yako unadhani ukiwa msomi unapaswa kuanza na biashara ya kuuza Magari.

Genge la nyanya ni biashara kikubwa ni unaendesha vipi hilo genge? Bakhresa anauza maandazi ila kama angekuwa ni Graduate kaanza kuuza mandazi maneno yangekuwa mengi sana, hizi ndo akili zatu
Biashara haipo kama unavyofikiria mkuu. Kuwaza biashara na kufanya biashara ni vitu viwili tofauti kabisa.
 
Shida ndo inakuja hapo, yaani wewe umesima unataka kufanya genge sawa na ambaye hajaenda shule?

Nina mtu ana genge lake ila yeye anasambaza mahitaji kwa watu, na kwa sasa pia kwenye genge lake kaanzisha kwenda kuchukua ndizi na vitu vingine na kuwasambazia wenye magenge kwa sasa kanunua Guta,

Biashara ni Technique sana sasa ukifanya tu ilimradi lazima ile kwako,
Lazima kuwe na tofauti ya Genge la Graduate na Genge la mtu ambaye hata shule hajaenda
Asa hiyo utaifanya kwa mtaji wa 20000 mkuu?
 
Ujue watu wanazania ukiwa msomi basi kuna aina ya biashara hupaswi kufanya na hii ndo sababu Graduate wamejaa mtaani.

Utofauti huja kwenye Model of oparation, Genge mtu anaweza kuja kumiliki Supermarket ila hayo yote ni malengo.

Sasa humu watu wanazania msomi unatakiwa kuanzia juu uwe na supermarket, kwa akili hizi lazima Graduate wawe wengi mtaani
Wewe ni motivation speaker ambae umetawaliwa na illusion (Vitu vya kufikirika)
 
Inashangaza kwakweli ila usishangae sana, alisoma ili aje kuajiriwa na benki au kampuni flani, na akiajiriwa hapo basi ndoto yake imetimia na atakomesha watu mtaani hasa wasio na ajira.

Ndivyo elimu na mazingira halisi ya kibongo yalivyo.

Pia utashangaa zaidi huyuhuyo ukimkuta anawasifia sana entrepreneurs wa nchi zingine hasa Marekani kuwa yule jamaa alianza chini sana leo ni bilionea mkubwa anamiliki kampuni flani.
Mfumo wa elimu tangu awali uliwawaeka watu kuwa na mentality ya kuajiriwa zaidi. Pia background, mazingira kiukuaji/social interactions na exposure vinaweza pia kuchangia. Hivyo mageuzi kiakili/kifikra/kimtazamo yanahitaji kufanywa mapema ili kuwajenga watu kuwa na muelekeo huo kifikra na kimtazamo.
 
Hii ni sawa na kusema Engineer wa magari anashindwaje kutengeneza koroboi au baiskeli
 
Hivi inakuwaje mtu kasoma business administration degree halafu hawezi fungua hata genge la kuuza nyanya a business administrate?

Genge la kuuza nyanya mtaji elfu 20

Hizo skili zake za business administration anataka akazionyeshee wapi?
Business administration haijikiti zaidi kwenye kuajiri, kufukuza, sheria za kazi, mafao, makato n.k.?
Sidhani kama wanafundishwa jinsi ya kutafuta mtaji na kyzungurusha pesa ili kutengeneza faida, wachilia uwekaji mzuri wa taarifa za kifedha.
 
Back
Top Bottom