Uchaguzi 2020 Hivi inakuwaje kuanza kwa kampeni kwa CCM kuwa ruksa na kwa wapinzani kuwe haramu?

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,360
2,000
Jeshi la Polisi nchini linatekeleza majukumu yake kwa "double standards"

Lile linaloonekana haramu, likitendwa na CCM linaonekana halali kwao na likitendwa na vyama vya upinzani linaonekana haramu na linachukuliwa hatua Mara moja!

Mfano halisi ni hivi majuzi tu wakati kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, alipofanya kikao, tena cha ndani, huko Mtwara, akakamatwa na kulazwa kituo cha Polisi, akidaiwa kufanya kikao haramu cha kukusanyika kinyume cha sheria!

Lakini waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amefanya mkutano wa hadhara na tena amepiga simu kwa Rais Magufuli, na simu hiyo ikawekwa "loud speaker" ili kila mtu aliyekuwepo pale mkutanoni amsikie, tena akiwa anafanya kampeni kabla ya muda, kwa kuwaahidi wananchi wa huko kuwa atawajengea barabara ya lami, lakini kitendo hicho hakikuhesabika kuwa ni kuanza kampeni kabla na ni kitendo cha kutaka kuwahonga wakazi wa huko!

Hata hao Polisi walipigwa "ganzi" na kujifanya hawakuliiona "kosa" hilo la wazi kabisa na kutochukuliwa hatua yoyote, kwa Waziri Mkuu, kwa kufanya kosa hilo la kuanza kampeni kabla ya muda!

Ndipo hapo ninapojiuliza, hivi hawa Polisi wetu wameshakuwa jumuiya mojawapo ya Chama cha Mapinduzi?

Hii "double Standards" mnayoiendesha Jeshi letu la Polisi nchini, itafika mahali wananchi tutasema "enough is enough"
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,360
2,000
Kamwe mtoto hawezi kumpiga baba kibao cha uso
Lakini lazima watekeleze majukumu yao kwa mujibu wa viapo vyao.

Viapo vyao vinawataka wao wasijuhusishe na mambo ya siasa na jukumu lao kubwa liwe kulinda usalama wa raia na Mali zao na wawe "fair" katika utekelezaji wa majukumu yao.

Wajiulize hao Polisi wetu, hivi ni kweli wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa viapo vyao au wamejitumbukiza kwenye ulingo wa kisiasa, wakijiegemeza kwa upande wa CCM?
 
stickvibration

JF-Expert Member
Feb 7, 2017
3,213

Kipi bora kiapo au tumbo
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
29,785
2,000
Acha wivu, ya majaliwa ilikua ni shughuli ya kusaini ujenzi w barabara. Sio ahadi.
muulize mmawia na erythrocyte, Mbona wanaposti posti picha za chadema wakiwa mikutanoni?
 
barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
29,785
2,000
Lakini lazima watekeleze majukumu yao kwa mujibu wa viapo vyao.

Viapo vyao vinawataka wao wasijuhusishe na mambo ya siasa na jukumu lao kubwa liwe kulinda usalama wa raia na Mali zao na wawe "fair" katika utekelezaji wa majukumu yao.

Wajiulize hao Polisi wetu, hivi ni kweli wanatekeleza majukumu yao kwa mujibu wa viapo vyao au wamejitumbukiza kwenye ulingo wa kisiasa, wakijiegemeza kwa upande wa CCM?
Umekurupuka, hujui ya majaliwa ilikua ni nini ila umekuja mbio kama kawaida yenu.
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,360
2,000
Umekurupuka, hujui ya majaliwa ilikua ni nini ila umekuja mbio kama kawaida yenu.
Wewe hujui kuwa Bajeti inapangwa na Bunge letu na haipangwi na Rais Magufuli?

Ilikuwaje awaahidi wakazi wa Luangwa barabara ya lami, wakati si jukumu lake?
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
51,118
2,000
CCM bila polisi ni wepesi kama pamba.
tapatalk_1583005154747.jpeg
 
Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
14,360
2,000
CCM bila polisi ni wepesi kama pamba. View attachment 1490709
Daudi Mchambuzi
Hao CCM wanaojitapa kuwa wamewafanyia mambo mengi sana mazuri wananchi, kwa hiyo hawaogopi wapinzani katika uchaguzi mkuu ujao.........

Hivi kama mna uhakika wa kupata ushindi mkubwa kiasi hiko, mna haja gani ya kufanya figisu figisu hizi zote, zinazoongozwa na Jeshi letu la Polisi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom