Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,480
- 30,152
Jeshi la Polisi nchini linatekeleza majukumu yake kwa "double standards"
Lile linaloonekana haramu, likitendwa na CCM linaonekana halali kwao na likitendwa na vyama vya upinzani linaonekana haramu na linachukuliwa hatua Mara moja!
Mfano halisi ni hivi majuzi tu wakati kiongozi wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, alipofanya kikao, tena cha ndani, huko Mtwara, akakamatwa na kulazwa kituo cha Polisi, akidaiwa kufanya kikao haramu cha kukusanyika kinyume cha sheria!
Lakini waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, amefanya mkutano wa hadhara na tena amepiga simu kwa Rais Magufuli, na simu hiyo ikawekwa "loud speaker" ili kila mtu aliyekuwepo pale mkutanoni amsikie, tena akiwa anafanya kampeni kabla ya muda, kwa kuwaahidi wananchi wa huko kuwa atawajengea barabara ya lami, lakini kitendo hicho hakikuhesabika kuwa ni kuanza kampeni kabla na ni kitendo cha kutaka kuwahonga wakazi wa huko!
Hata hao Polisi walipigwa "ganzi" na kujifanya hawakuliiona "kosa" hilo la wazi kabisa na kutochukuliwa hatua yoyote, kwa Waziri Mkuu, kwa kufanya kosa hilo la kuanza kampeni kabla ya muda!
Ndipo hapo ninapojiuliza, hivi hawa Polisi wetu wameshakuwa jumuiya mojawapo ya Chama cha Mapinduzi?
Hii "double Standards" mnayoiendesha Jeshi letu la Polisi nchini, itafika mahali wananchi tutasema "enough is enough"