Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,620
- 46,260
Kila historia ya uhuru wa Tanganyika inapozungumzwa jina linalokaribia kumeza historia yote ni Julius Kambarage Nyerere(JKN). Ukimuondoa Nelson Mandela wa Afrika kusini hakuna kiongozi mpigania uhuru aliyetandaza kivuli chake kwa nchi yake kama Mwl. Nyerere.
JKN ameacha "legacy" kubwa na ndefu. Ameandikwa katika kila kitabu cha historia nchi hii, madaraja, majengo, viwanja vya ndege, mabwawa ya umeme, barabara, shule, vyuo n.k vimepewa jina lake. JKN amekuwa rejea ya uongozi nchi hii, ukimkosoa JKN unaonekana kama mhaini na wafahidhina wa nchi hii.
Tofauti na Afrika Kusini ya Nelson Mandela ambapo wapigania uhuru wake wengi wameendelea kutajwa mfano wa Oliver Thambo, Steve Biko, Chris Hani, Govan Mbeki n.k Tanganyika na baadaye Tanzania ya Nyerere jina kubwa la harakati za uhuru ni JKN, majina mengine yanasikika kwa mbali sana au yamepotea kabisa.
Sote tunafahamu Nyerere alikuwa na wenzake wengi katika kutafuta uhuru wa nchi hii. Tungependa kuwafahamu na kujua mchango wao kupitia maandishi ya historia rasmi rasmi za serikali. Pia wangetendewa haki kama majina yao yangeanza kupewa masoko, madaraja, barabara, viwanja vya michezo, ofisi za serikali zinazojengwa Dodoma n.k