Hivi huyu kamzidi huyu kimadaraka...........?

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,524
863
Jamani naomba mwenye kufahamu anifahamishe. DC WA WILAYA YA HANDENI BW. MUHUNGO amepewa maagizo na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kapteni HONESTI ERNEST MWANOSSA kufuatilia na kuwafikisha mahakamani wale wote waliohusika na ujenzi duni wa zahanati ya kijiji cha KWEINGOMA, sijajua hapa nani mwenye mamlaka zaidi ya mwingine.
 
Hapo suala si mamlaka, bali ni nani anayefahamika sana kwa JK. Ulikuwa hujui kama JK anakufahamu na mnauswahiba sana unaweza mpa amri hata Waziri wa JMT na akaitekeleza?

Utawala wako umepimwa nao umeonekana umepungua....
 
Jamani naomba mwenye kufahamu anifahamishe. DC WA WILAYA YA HANDENI BW. MUHUNGO amepewa maagizo na kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kapteni HONESTI ERNEST MWANOSSA kufuatilia na kuwafikisha mahakamani wale wote waliohusika na ujenzi duni wa zahanati ya kijiji cha KWEINGOMA, sijajua hapa nani mwenye mamlaka zaidi ya mwingine.

Yaani hata mimi nilishangaa sana wakati naangalia hiyo habari.
Ni kama mtu anayesema, nitakusemea kwa baba! shauri yako!
 
Yaani hata mimi nilishangaa sana wakati naangalia hiyo habari.
Ni kama mtu anayesema, nitakusemea kwa baba! shauri yako!

Kama kusemewa kwa baba kunaharibu mipango yako basi tekereza unachoambiwa bila kuchali nani anakueleza
 
Mkuu hapo kiongozi wa mbio za mwenge ndo mkubwa kwa wakati huo anakimbiza mwenge, anakuwa ni kiongozi wa kitaifa na ndo maana anapewa heshima kukata kufungua au kuweka jiwe la msingi kwenye miradi kibao nchini kote lakini mwambie huyo mkuu wa wilaya kama ataweza kufungua mradi wowote nje ya wilaya yake.

katika uhai wote wa mbio za mwenge kila wanapoenda ni ugeni wa kitaifa na ndo maana wanapokelewa na wanene wote wa mkoa/wilaya husika utafikiri ni Liwalo na liwe au mheshimiwa Dhaifu au yule mzee wa scissors.
 
hicho cheo cha kiongozi wa mbio za mwenge kipo ktk katiba ya jamhuri?au ni cheo ndani ya ccm?
 
hicho cheo cha kiongozi wa mbio za mwenge kipo ktk katiba ya jamhuri?au ni cheo ndani ya ccm?
Mimi sijui kama hicho cheo kipo kwenye katiba lakini kumbuka mwenge wa uhuru ni alama mojawapo ya taifa letu na alama za taifa mara nyingi huheshimiwa sasa kwa nini kiongozi anayetembeza hiyo alama asiheshimiwe?
 
Ni udhaifu katika serikali ya tanzania tu, duniani kote. kwa sabababu kiongozi wa mbio za mwenge hakupewa mamlaka ya kuwajibisha bali kufungua miradi atakayoikuta maeneo husika bila kujali ubora ikiwa ni pamoja na kuwafikishia wananchi ujumbe wa Mbio za mwenge. Sasa swali la kujiuliza yeye(mbio za mwenge) ni mtaalamu wa kila kitu au kapewa wataalamu wa kuzunguka nao? Nitashangaa kuona huyo mkuu wa wilaya akiweweseka kwa kauli ya huyo Dogo mkimbiza mwenge. Dogo mkimbiza mwenge ameenda nje ya mada/lengo.
 
unashangaa swala mwenye njaa akimfukuza simba porini?
ndipo tulipofika kama taifa na uzuri vyeo vyote hutaviona baada ya katiba nusumpya.
 
Kama kusemewa kwa baba kunaharibu mipango yako basi tekereza unachoambiwa bila kuchali nani anakueleza

Huko ni kutoongozwa na taratibu na kanuni bali na watu. Tunahitaji uongozi kama taasisi na sio watu. Yaani chain of command should be clear!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom