Idimi
JF-Expert Member
- Mar 18, 2007
- 14,971
- 10,465
does this mean kama wewe haumo ndani ya system/serikali huwezi kuajiriwa in a senior position hata kama elimu yako inatakiwa uanzie huko juu...watu hawa naona vichwani ni makamasi tuu labda kada anaelewa kwanini?
Yaani pamoja na kutaabika kwangu kote kujisomea ili niitumikie sirikali naona sasa nachinjiwa baharini. Sijauelewa vyema huu uamuzi wa Hawa Ghasia na wenzake wa utumishi wa umma, sijajua mantiki hasa ya kufanya maamuzi haya ambayo kwa maoni yangu naona ni maamuzi ya ajabu kupita maelezo.
HOJA
1. Napinga suala la serikali kujitetea kwamba wanaepuka gharama za "On job training", hizi haziepukiki kabisa. Teknolojia mpya za utendaji kazi huwa zinabadilika kila leo, kwa hiyo mafunzo kazini hayakwepeki. Madhara ya kutowapa elimu mpya hao watumishi wa zamani ni makubwa sana kuliko hizo gharama wanazojifanya wanaziepuka, na hapo ndipo tunapoangamiza kabisa na zile juhudi kidogo tulizozionyesha katika utumishi wa umma. Wanataka turudi kwenye kuhifadhi mafaili "Manually", badala ya kutumia nyenzo? Mfano, mwishoni mwa miaka ya tisini, wengi tulitumia programu za kompyuta za "Windows 9x, yaani 95 na 98. Kuanzia mwaka 2000 kumekuja Windows mpya zikiwa na mambo mengi mapya. Windows hizi ni Millennium Edition (ME), 2000, XP, Media Cente Edition, Server na sasa vista. Sasa kama uliajiri watu wa kutumia windows 95 miaka hiyo, lazima watu hawa wapate elimu ya kutumia programu hizi mpya, ama uamue kubaki na teknolojia ya zamani na kupunguza ufanisi. Mpaka hapa lazima utafute mtu wa kuwapa elimu mpya hawa watumishi. Huu uhafidhina naona umefikia mahali pabaya sana. Huo ni mfano mmoja tu. Najua kwa watawala, mbinu za kiutawala hubadilika kuendana na mazingira na wakati, kwa hiyo kutokubali kubadilika ina manaa tunarudisha maendeleo nyuma.
2.Kasema kuwa wataajiri watendaji pale tu ambapo kutakuwa hakuna kabisa watumishi wa nafasi husika waliopo kazini kwa wakati huo. Sawa! Je hawa hawatapatiwa mafunzo ya utendaji? Sasa hapa unaepuka nini na unakwepa nini?
3. Kuna hizi tuhuma hapa Jf kwamba watoto wa vigogo wamejazana kule kunako pesa za sie walipa kodi. Ina maana kama hakuna mtu wa kuingia kutoka nje ya hao waliopo basi sisi wenye hizo pesa tunakosa imani na waliopo, hili nalo litafanya hata kile kidogo tulichohifadhi kitokomee kabisa. Nina wasiwasi na hili, labda nipatiwe ufafanuzi. Nina hofu na hizi ajira za vimemo.
4. Hoja nyingine ya Mheshimiwa Ghasia ni kwamba wanakwepa kuajiri watu ambao utendaji wao haujulikani. hili nalo mimi nalipinga kabisa. Sirikali haina uwezo wa kumjua kila mtu na utendaji wake, sawa, lakini kuna watu ambao wako nje ya utumishi wa umma na wanafahamika kuwa ni watendaji kazi bora sana. Mfano, kuna Dr Kimei wa CRDB ambaye utendaji wake unaonekana, kwamba benki anayoiongoza inazalisha faida na wanahisa wanapa gawio, tofauti na TOL. Sasa huyu naye watasema utendaji wake haufahamiki? Kuna wahandisi, mameneja, watawala na watafiti kibao sana wanaotumika nje ya utumushi wa umma na wanafahamika kwa utendaji wao, sasa kwa nini watiliwe shaka? Hali kadhalika kuna kipindi cha maangalizi (probation), mtu anapoanza kazi, kama utenaji wake hauridhishi basi anabadilishwa. Napinga kabisa kitendo cha sirikali kuogopa kuajiri watu eti kwa sababu utendaji wao haufahamiki. Huku ni kutokubali changamoto. Ingekuwa ni mtihani kwa Ghasia na wenzake ningewapa alama "G" kabisa, kwa sababu wamepitiliza kiwango cha mwisho cha kufelia ambacho ni daraja "F".
Huo ndio mtazamo wangu
Naomba kuwasilisha!