Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Nimeona Rais akisema Serikali kutafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar es Salaam ili kuleta ufanisi na kuongeza mapato.

Ni kweli tunahitaji mbia wa kuiendesha bandari ya Dar? Sisi wenyewe imeshindikana kabisa?

Tumewahi kufanya hivi kwenye reli, shirika la ndege lakini tunajua kilichotukuta.

Hii haiwezi kuja kuiua hii bandari kwa maana tunajuana vizuri sisi hasa linapokuja suala la maslahi.

--
Rais Samia Suluhu amesema maboresho yanafanyika kwenye Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kupata mbia wa kuiendesha, kubadili uongozi na miundombinu ili kuongeza ufanisi.

Amesema robo tatu ya bajeti ya nchi inaweza kutegemea bandari endapo zitafanya kazi inavyotakiwa.

Bandari.jpg


======

KUHUSU MKATABA WA BANDARI YA DAR ES SALAAM NA DUBAI PORT (DP WORLD)

Kumekuwa na mjadala unaoendelea nchini Tanzania tangu 2022 na ukapamba moto 2023 kufuatia hatua ya Serikali kuingia makubaliano na ukodishaji wa bandari ya Dar es Salaam na kampuni moja ya kimataifa ifahamikayo DP World ya Dubai.

Mjadala huo unahoji mazingira ya mkataba huo pamoja na vipengele vilivyomo huku baadhi wakionya kuhusu hali hiyo.

Mjadala huo umeyavutia makundi ya aina mbalimbali kuanzia ndani ya watendaji wa serikali, Wabunge pamoja na wale wapembeni wanaoonyesha ukosoaji wa waziwazi.

Habari zinaonyesha kuwa serikali ya Tanzania kupitia mamlaka ya usimamizi wa bandari nchini TPA, imeanzisha majadiliano na kampuni ya usafirishaji mizigo ya Dubai Port ( DP World) inayomilikiwa na serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu kwa ajili ya kuendesha bandari zote zilizoko nchini.

Licha ya mamlaka ya bandari nchini kufafanua kuwa hakuna mkataba wowote uliosainiwa baina ya pande hizo mbili, hata hivyo wale wanaohoji wanasema kitendo cha serikali kuwahisha kupeleka bungeni azimio la kuanzisha majadiliano hayo linazidisha wasiwasi kuhusu yale yanayoweza kufikiwa kwenye mkataba huo.

Tangu Mwanzoni Mwaka 2022, Habari zilianza kuenea Mitandaoni hasa JamiiForums kwamba Bandari ya Dar Es Salaam imeuzwa kwa Muwekezaji kutoka Dubai(Bandari ya Dar imeuzwa kwa Mwarabu), japo Mara ya kwanza zilianzwa kukanushwa hadi Mkataba ulipo vuja.

Hapa Chini nimeambatanisha baadhi ya Mijadala iliyojadiliwa ndani ya JamiiFrums kuhusu Mjadala wa bandari ya Dar ES Salaam na DP World.
  1. Rais Samia: Serikali kutafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi
  2. Bandari ya Dar es Salaam kashapewa mwarabu kuiendesha. RIP Magufuli, Watanzania tukakukumbuka daima
  3. Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Hakuna kipengele kinachozungumzia uuzwaji wa Bandari, na hakuna mkataba wowote ulioingiwa
  4. Uchambuzi wa mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi Bandari Tanzania na DP WORLD
Wau Mbalimbali Mitandaoni wakaanza kuupinga kwamba ni Mkataba wa Kinyonyaji.
  1. Mkataba wa Bandari: Diaspora Waandamana kupinga Mkataba wa Bandari leo Agosti 18, 2023 London
  2. Wakili Dkt. Rugemeleza Nshala(PhD) aitwa Polisi kutokana na maoni yake kuhusu bandari
  3. Maandamano makubwa ya Amani kupinga DP World kufanyika Julai 22
  4. Askofu Bagonza: Wanasheria wetu Ujanja wao unaishia Kisutu, na Wachumi wetu Ujanja wao unaishia Kariakoo, Mkataba wa Bandari hawauelewi
  5. BANDARI DAY: Mkutano wa Hadhara wa CHADEMA Viwanja vya Bulyaga, Temeke
  6. Vijana kufanya Maandamano kupinga Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na kampuni ya DP World ya Dubai
  7. Wakili Mwabukusi: Rais Samia atusikie, Mkataba wa Bandari haulindi uhai wa Nchi yetu
Vyombo vya dola vikaanza kuwakamata na kuwatia misukosuko watu Walioonekana kupinga Mkataba huo hata waliojaribu kuandamana Walikamatwa
  1. Dkt. Slaa akamatwa na watu waliojitambulisha kama Polisi
  2. Serikali yatumia nguvu kubwa ya Polisi kutaka kuzuia kongamano la wananchi la kupinga mkataba wa bandari
  3. Tulikamatwa kinyume na sheria kwa sababu za kisiasa na tukaachiwa kisiasa
  4. Rais Samia amvua hadhi ya Ubalozi Dkt. Slaa | JamiiForums
  5. Dkt. Slaa: Nitaendelea kusema ninachoamini, asema hajutii kuondolewa hadhi ya balozi
  6. Waliondamana Dar es Salaam kupinga mkataba wa bandari wakamatwa na polisi. Mratibu wa maandamano na wenzake 10 wanahojiwa na Polisi
  7. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataka kumfutia Leseni ya Uwakili Wakili Mwabukusi aliyefungua kesi kupinga mkataba wa DP World
  8. Hatma ya Dkt. Slaa, Wakili Mwabukusi na Mdude bado Giza Totoro
Taasisi mbalimbali, Watu wa binafsi, dini na vyama vya siasa, vikatoa matamko ya kutaka Mkataba huo usisainiwe au urekebiswe kwa Manufaa ya Umma. Huku wengine wakiunga Mkono Mkataba huo.
  1. Baraza la Maaskofu Katoliki (TEC): Hatuungi mkono Mkataba wa Bandari. Sauti ya Watu ni sauti ya Mungu
  2. Freeman Mbowe: Tunazindua "Operation +255 Katiba Mpya Okoa Bandari Zetu" kuwaambia watanzania ubaya wa Mkataba wa DP World
  3. Arusha: Rais Samia ashiriki Maadhimisho ya Miaka 60 ya KKKT - Agosti 21, 2023
  4. Askofu: JamiiForums pekee ndio wameripoti Waraka wa TEC kwa Weledi
  5. CCM yatoa Baraka zote kwa DP World kufanya uwekezaji wa Bandari
  6. Uchambuzi wa TLS kuhusu Mkataba wa Bandari, ipatikane nakala ya Kiswahili
  7. Tundu Lissu: Rais Samia na Mbarawa wameiuza Tanganyika yetu kwa Waarabu
  8. Anna Tibaijuka: Dubai ni Mshindani Wetu kwenye kuendeleza Transhipment potential, tukimkabidhi Bandari zote ni sawa na Kujinyonga!
  9. Kardinali Pengo: Ni kweli Watanzania hatuwezi kuendesha bandari yetu?
  10. Mbowe: We are surrendering our Sovereignty to Dubai
  11. Wanazuoni watoa tamko: Bandari ni mali za Watanzania wote hatuna wanahisa na hatuhitaji wanahisa
  12. Rais TLS: Huwezi kutuita ghafla kutoa maoni kuhusu Bandari, sisi sio Waganga wa Kienyeji
  13. Bandari na DP World: Dkt. Slaa asema ni uuzaji wa Nchi. Adai Serikali iliyopo ina uhalali wa wasiwasi
  14. Viongozi wa Dini wanazungumza na Serikali kuhusu Mkataba wa Bandari kati ya Tanzania na Dubai
  15. Mpina: Nchi yetu imefilisika hadi inapangisha Bandari? Tusikubali hili
  16. Musukuma aisifia DP world ya Dubai sakata la bandari. Adai Taifa linacheleweshwa na wajinga wanaotaka kushirikishwa kila kitu
Hata pale DP WORLD ilipofanya kazi za kujitolea Nchini, ilizua maneno kwamba Wanahonga ili wakubalike
  1. Askofu Mwamakula: DP World kujenga msikiti wa Masjid al jumaa wa Mbeya na kuendelea kusaidia dini ya kiislam nchini Tanzania!
  2. Baada ya kulitafakari sakata la DP World, nimegundua kuwa waislam walikuwa sahihi
Bunge likaitisha Mkataba huo na kuusoma hatimaye kuupitisha baada ya kuitaka Serikali irekebisha baadhi ya vifungu.
  1. Bunge lakaribisha maoni, kuhusu mapendekezo ya kuridhia makubaliano mkataba kati ya Tanzania na kampuni ya Saudia kuendesha bandari Dar es Salaam
  2. Maoni ya Kamati Kuhusu Azimio la Bunge Kuridhia Makubaliano Kati ya Tanzania na Dubai Kuhusu Ushirikiano wa Uendelezaji na Uboreshaji Bandari Tanzania
  3. Waziri Mkuu: Bandari imepewa DP-World kwa kuwa utendaji wa TICTS ni mdogo
  4. DP WORLD: Mkataba wa Bandari kwa Kiswahili (tafsiri isiyo rasmi)
  5. Uchambuzi wa mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi na kijamii kwa ajili ya uendelezaji na uboreshaji wa utendaji kazi Bandari Tanzania na DP WORLD
  6. Hamza Johari: Timu ya Uchunguzi wa Mkataba wa DP World iliteuliwa na Hayati Magufuli, Rais Samia anaendeleza mchakato
  7. Mkazi wa Songea amuandikia barua Spika wa Bunge kupinga bandari kuuzwa
  8. Dodoma: Bunge lapitisha azimio la kuunga mkono mkataba wa Tanzania na DP World
Kesi ilifunguliwa Mahakamani kushinikiza DP WORLD Wasichukue bandari ya Dar. Makubaliano yote yasitishwe.
  1. Sakata la Bandari: Tunafungua Shauri Mahakama Kuu kwa Hati ya Dharura
  2. Sakata Mkataba wa Bandari: Wakili Mwabukusi asema asiyetaka kukosolewa aondoke kwenye ofisi za Umma
  3. Mbeya: Hukumu ya kesi ya kupinga Mkataba wa Bandari yaahirishwa, sasa kusomwa Alhamis 10/8/2023
  4. Mbeya: Mahakama Kuu yatoa baraka Uwekezaji wa DP WORLD Dubai Bandarini. Walalamikaji wajipanga kukata Rufaa ya Hukumu
Hatimaye Serikali ya Tanzania ikasaini Mkata rasmi na DP WORLD na Kuanza kutumika.
  1. Tanzania inatarajiwa kuingia mkataba na Kampuni ya DP World ya Dubai kuendeleza bandari ya Dar es Salaam
  2. Utiaji saini Mkataba wa Tanzania na DP World: Mkataba utakuwa wa miaka 30 na utendaji kazi wake utapimwa kila baada ya miaka 5 na sio miaka 100
  3. Prof Mbarawa: Kwa sasa Bandari inachangia 37% ya Bajeti ya Nchi lakini DP World atatufikisha kwenye 67% hivyo ondoeni Wasiwasi!
  4. Waziri Mbarawa ataja sababu za kubinafsisha bandari zetu kwa wageni
DP WORLD Wanaanza kazi Dar kwa Kuwataka Wafanyakazi wa Bandari kuchagua kubaki TPA au Kujiunga na DP WORD
  1. Mamlaka ya Bandari (TPA) yatoa ufafanuzi kuhusu hali ya ajira za Watumishi wa Bandari ya Dar es Salaam
 
Aiseee! Kuna siku tutatafuta mbia wa kuiendesha serikali maana tumeshashindwa kuiendesha bandari.

Ili bandari ifanye vizuri zaidi inatupasa kuachana na siasa kwenye uendeshaji wake Menejimenti ya Bandari iwekewe malengo na wasiingiliwe na serikali.

Kuwe na mkataba baina ya serikali na menejimentj ya TPA, iwapo watashindwa kufikia malengo yaliyowekwa kwa kila robo mwaka basi kibarua kinaota nyasi na iwapo kuna jinai sheria ichukue mkondo wake.

Nadhani tuanzie hapo.

Vv
 
Huu ufunguaji wa Nchi inabidi tuufanyie due diligence ya kupata Pro and Cons.

Naona tunatafuta short term gains for long term pains.

Na wale tuliotegemea wasimamie na kuishauri serikali wamegeuka kuwa rubber stampers.

Hawa wanafanya zile Propaganda za awamu iliyopita zianze kuonekana Maybe..., Just Maybe kulikuwa na Ukweli ndani yake.
 
Kama yeye Rais anamteua Polisi mstaafu kuwa mwenyekiti wa bodi ya Bandari.

Hivi tutarajie miujiza gani hapo?

Au ndio mkakati wa kuididimiza Bandari yetu zaidi?

Ikumbukwe kwamba ukiishaingia mikataba leo haitakuwa rahisi kuja kuwaondoa huko mbeleni.

Hata iwapo wanaendelea na madudu yao.
 
Back
Top Bottom