Bill
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 8,285
- 8,501
Kila association ina caucus yake....wengi pengine mlikuwa wadogo au hamkuwa mjini wakati Mzee Mtei alipoanzisha chama hiki mwaka 1992 na akina Makani(Msukuma),Kimesera(Mmasai),Ngwilulupi(Mnyakyusa),Kabourou (Muha)Franco Kabigi na baadaye dada yake Maria(Wanyakyusa) na wengine wengi...Mchagga alikuwa Mtei tu pale Kisutu Street...na huyu mzee alikuwa anazunguka na gari yake huku na huko kutafuta wanachama na hakuna aliyemsikiliza...naturally familia yake na za hao wenzake zilijiunga na kumuunga mkono...sasa leo watu wanapodai ni chama cha Mtei na familia yake, udini,ukabila,ukanda kwa kweli siwaelewi kabisa...mnasahau kabisa kuwa awali watu hawakukichukulia seriously hiki chama....Mtei akaona imetosha akang'atuka akamwachia Makani....nae akaona imetosha akamwachia Mbowe...naye wakati wake ukifika atamwachia mwingine
Hakika umenena mkuu, kwa wasiojua historia ya Chadema wanaweza kupotoshwa na propaganda za watu, Ila ukweli ndio huo. Kuna kipindi Mwalimu JK. Nyerere (RIP) alishawahi kusifia sera za Chadema. Lakini Chama hakikuwa na umaarufu hata wa kusimamisha mgombea urais. Kwa kweli Mtei, Bob Makani among others walifanya kazi kubwa sana, lakini pia mchango wa Mbowe na Sasa Dr. (PhD) Slaa umekuwa mkubwa na wamejitolea sana kukiimarisha chama.
Ili kuondoa wingu na propaganda juu ya Chadema nawaomba viongozi wa Chadema watubandikie historia ya chama japo kwa ufupi tu. Wengi tutafurahi