Dr Akili
JF-Expert Member
- Aug 21, 2011
- 4,953
- 4,326
Rais aliruhusu mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ili vikatangaze sera za vyama vyao kwa wananchi ili kuwavutia kuwaunga mkono kwenye harakati za kushika dola kwenye chaguzi zijazo.
Chama cha siasa ni sera yake na si vinginevyo. Rais aliruhusu ruzuku ya Serikali kwa Chadema iliyokuwa imegomewa ya bilion mbili (inasemekana) kwa mwezi kuanza kutolewa.
Cha ajabu Chadema wamekuwa wanazunguka kila mahali wakipinga serikali kwa kila kitu inachokifanya, wakikashifu, kudhalilisha na hata kuwatutana na kuwatezwa viongozi wakuu wa serikali ikiwamo raisi wa nchi, kuchochea vurugu na uvunjaji wa amani. Wamekuwa wakitishia kwamba watakiwasha hapa ndani na duniani kote kwani waungwa mkono na dunia aka mabeberu wa dunia ie EU, USA etc.
Wamekuwa wakidandia masuala hususani ya maboresho ya katiba ya nhi, mkataba wa bandari zetu na DP World na uboreshaji wa hifadhi ya Ngorongoro na kuyafanya kuwa ndiyo sera yao wakati kuna vyombo halali vinavyo shughulikia mambo haya.
Leo Rais kasema na kutoa maelekezo, sidhani kama hawa chadema wamemuelewa. Watapinga maelekezo haya kama kawaida yao. Ikumbukwe kwa mila zetu, tamaduni zetu na sheria zetu, maelekezo ya mkuu wa nchi ni maagizo na ni amri. Hawa jamaa watayapinga na kumteza aliyeyatoa. Ni utovu wa nidhamu na ukosefu wa adabu.