Hivi CHADEMA siku hizi inasimamia nini?

Hivi CHADEMA siku hizi inasimamia nini?

Anza kwa kueleza were binafsi umesaidia vipi kuhakikisha wananchi hawauawi, kutekwa, kuteswa, kufungwa bila hukumu na maovu mengine mengi yanayofanywa na watu wasiojulikana. Ukianza hivyo mjadala utakuwa wa pande mbili hivyo utanoga, umeanzisha hoja kisha umeifunga.
Hiyo kazi ya polis na vyombovya usalama
 
Wanasimamia agenda ya Kutaka kuchafua amani ya nchi..!!

Bado najiuliza hio demokrasia ndio itapatikana baada ya kuliingiza taifa katika machafuko..??

Waliokaa chini na kuhitimisha njia pekee ya kulikomboa hili taifa ni kuhamasisha uhaini, wanahitaji kupimwa akili..!!
Unazungumzia machafuko gani, haya ya watu kutekwa na kuuawa kisha kufungwa kwenye viroba. Mie naona tayari kuna machafuki, hatujawahi kukutana na mazingira haya kama ya Rwanda.
 
Wanasimamia mlo kama wewe unavyosimamia wa kwako.
Eti wanasimamia nini. Wa kwako anasimamia nini? Killings???
 
Chama kila mtu msemaji wakiamua kuitisha press conference kila mtu na ukumbi na azimio lake.

Chama mfu kabisa. Kwa aina ya siasa zao waache CCM watawale tu.
 
Chadema kwa sasa wanakera sana wanasimamia kauri za Mange Kimambi. Huyu dada amekuwa kama kiongozi wa Chadema akisema neno chadema wanakurupuka kama nyumbu wanamuunga mkono.
 
Chama Kina Ilani yake ..Ukiipitia utajua wanasimamia nini..Ni Kama ilivyo Serikali ya Magu sasa.Wanaongoza Nchi Kwa Ilani ya CCM ..Ila Kila Kiongozi Awamu hii Akiamka asubuhi ana Tamko..Hivi Msemaji wa Serikali ni nani?..Jambo Baya zaidi Kiongozi wa Nchi anasema Wanaweka Katiba kando kwanza Wainyooshe Nchi..Nini kipaumbele kwa Serikali hii Ya Sasa? Maswali yako Mkuu Nyani Ngabu Kwa CDM Majibu yake yako Wazi..Labda kama Ungetolea Mfano CUF.
 
Labda nikueleze tu upinzani ni taa ya serikali kwa watawala wanaojielewa kwa maana kwamba wao wana uwezo wa kuzungumza madhaifu ya serikali bila unafiki sasa kwa mtawala anayejielewa anayachukua kama changamoto anayafanyia kazi ili Tupate Tanzania bora,hata haya Magufuli anayopambana nayo asilimia kubwa yalipigiwa kelele na upinzani kwa muda mrefu japo unaweza kuhoji ufanisi wake wa kuyashughulikia!

Sasa katika zama hizi mtu akionyesha udhaifu wa serikali hatakiwi huyo anapewa chama na ukijitanabaisha kwamba ni mpinzani na unakosoa tu jambo unahatarisha maisha yako kwa maana unaweza kuuliwa...!!!sasa hapo ajenda yako itasimama kweli?jibu ni hapana lazima kwanza upambane kutafuta demokrasia then ukishaipata unyooke kwenye agenda yako
 
Tunasimamia mambo makubwa manne:

1. Matusi. Kama huamini basi subiri uone tutakavyokufanya kwenye huu uzi wako.

2. Ukabila. Kamanda wetu mkuu [HASHTAG]#lissumsaliti[/HASHTAG] alituanzishia chuki dhidi ya wasukuma kwa kuwa Magu ni wa huko, kwa hiyo tunafuata maono ya kiongozi wetu.

3. Kupinga kila kitu. Huo ndo mtazamo wetu km chama - big NO to everything.

4. Kutetea kitu chochote kilicho kinyume na sheria na matakwa ya serikali na uongozi wa nchi. Tunatetea wala rushwa, mafisadi, wauza 'sembe', wakwepa kodi, nk.
Sema jingine.
Tungekuwa tunatetea wala rushwa tungekuwa tunaisupport CCM, maana ndio author wa rushwa, ufisadi, uuaji na umaskini hapa nchini.
 
kuna jamaa huwa anasema kuuliza si ujinga ila hilo jambo halimaanishi watu wawe wanauliza maswali ya kijinga.
 
Uchaguzi wa SIHA?
Hata ule ambao wasimamizi ni makada wa chama, na ambao wanagoma hata kutoa barua za utambulisho wa mawakala wa CHADEMA wakiamini kuwa wana jeshi la polisi nyuma yao.
Very primitive indeed!!
 
Hawa wanaojiita chama kikuu cha upinzani siku hizi wanasimamia nini?

Manake naona wapo wapo tu. Hawaeleweki.

Eti wanampinga Magufuli kwa wanachodai ni 'udikteta' wake halafu wanamuunga mkono Uhuru Kenyatta kisa tu eti Raila Odinga ni rafiki wa Magufuli.

Halafu hapo hapo mambo wanayompingia Magufuli huyo Kenyatta naye anayafanya!

Si ajabu kama Magufuli angekuwa ni rafiki na Kizza Besigye CHADEMA nao wangemuunga mkono Museveni.

Sasa hivi hata haijulikani nani anakiongoza hicho chama. Ni Mange? Mbowe? Mashinji? Sugu? Lema? Lowassa? Sumaye? Nyalandu?

Nyie makamanda, nani kiongozi wenu siku hizi?

Bure kabisa nyinyi.

Tangu tuwasaliti wananchi 2015, kwa sasa tunasimamia MATUKIO na maelekezo ya Mange.
 
Kuna tetesi mke wa nyalandu nae anataka uongozi kwanini mumewe mwenye share nyingi baada ya lowassa asipewe shavu apewe mange asietoa chochote!
Mange ni taasisi kiboko hasa, watu hawalali
 
Back
Top Bottom