Hivi baada ya mtu kufa na kuzikwa anaenda wapi?

Kule Kwetu

JF-Expert Member
Jan 10, 2016
3,157
1,893
Habarini Wadau,

Kuna wakati natafakari mengi,mojawapo ni hili la wapi anapokwenda marehemu baada ya kufukiwa na kuachwa kaburini?

Hizi dini tulizoletewa zinasisitiza kuwa kuna Maisha ya milele Mbinguni/Peponi kwa watakaokufa katika kutenda mema. Na pia kuna moto wa Jehanum usiozima utakaowachoma milele wafao katika hali ya kuwa na madhambi. Haya ni ya kweli? Mbona naona kama walioleta dini wengi hawana hofu hiyo?

Kabla ya wao kuja Afrika,tulikuwa tunaamini tukifa tunaelekea wapi?

Confusing....
 
Hili ni swala la kiimani Bw.Kule kwetu! Hapa inabidi watueleze Wanatheolojia na pia wale Wazee wa mila kabla ya hizi dini za magharibi kuingia Afrika, baada ya maelezo ya pande zote mbili chagua upande mmoja ambao utaona una imani nao kulingana na maelezo yaliyotolewa!!
 
Wanaoza tho kiroho tunabaki nao ndo maana unakuta mtu unamuota mko wote mnapiga story. Na kama huyo mtu mulikuwa marafiki ndo kabisa kila ndoto unamuona akiwa katika hali ya mtu hai

Halafu eti tukiwaota tunaambiwa tuvunje hizo roho...yaani inaaminika sio vizuri kuwaota.
 
Habarini Wadau,

Kuna wakati natafakari mengi,mojawapo ni hili la wapi anapokwenda marehemu baada ya kufukiwa na kuachwa kaburini?

Hizi dini tulizoletewa zinasisitiza kuwa kuna Maisha ya milele Mbinguni/Peponi kwa watakaokufa katika kutenda mema. Na pia kuna moto wa Jehanum usiozima utakaowachoma milele wafao katika hali ya kuwa na madhambi. Haya ni ya kweli? Mbona naona kama walioleta dini wengi hawana hofu hiyo?

Kabla ya wao kuja Afrika,tulikuwa tunaamini tukifa tunaelekea wapi?

Confussing....
HAhahaaaaaaa eti CONFUSSING.,,,,,,SIO HIVO WEYE NI CONFUSING.
 
Back
Top Bottom