Undava King
JF-Expert Member
- Aug 11, 2017
- 3,205
- 5,332
"Matunda ya kila mti wa bustani unaweza kula mpaka ushibe. Lakini kuhusu matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula,utakufa hakika" (mwanzo 2:16,17)
Lakini je kuna sehemu fulani ya mwanadamu inayoendelea kuishi baada ya mtu kufa?
Biblia inasema "Mungu hawezi kamwe kusema uongo" (waebrania 6:18) ukweli ni kwamba shetani ndiye alisema uongo alipomwambia Hawa hivi "Hakika hamtakufa" mwanzo 3:4.
Hivyo basi swali ni; ikiwa fundisho la kutokufa kwa nafsi ni uongo ni nini hutokea mtu anapokufa?
"Yehova Mungu akamfanya mtu kutoka katika mavumbi ya nchi na kupuliza katika mianzi ya pua yake pumzi ya uhai,naye mtu akawa nafsi hai" usemi "nafsi hai" unatokana na neno la kiebrania ne'phesh, likimaanisha kiumbe anayepumua.Mwanzo2:7
Hivyo biblia haielezei kuwa mwanadamu hakuumbwa akiwa na "nafsi isiyoweza kufa" badala yake ni "nafsi hai"
Ni kina nani basi walioleta fundisho la nafsi kutokufa kama siyo Mungu mwenyewe?
Wamisri walikuwa kikundi cha kwanza,wakifuatiwa na wababiloni na wagiriki walioeneza mafundisho hayo kuenea katika himaya nzima ya ugiriki katika mwaka wa utawala wa Aleksanda Mkuu 332W.K,
Baadae madhehebu ya kiyahudi ya waesene na mafarisayo, yalianza kufundisha kutokufa kwa nafsi kwa kupokea mawazo ya Plato" ilikuwa rahisi kuunganisha falsafa ya Plato na ukristo sababu ya nadharia ya Plato kwamba mwanzoni nafsi zetu zilikuwa mahali pazuri na sasa zinaishi ulimwengu uliopotoka"
Mtume Paulo analiongeleaje,"...vipindi vya nyakati za mwisho wengine wataanguka kutoka kwenye imani, wakisikiliza maneno yaliyoongozwa kwa roho yenye kupotosha na mafundisho ya roho waovu"(1Timotheo 4:1) Hivyo basi biblia haiungi mkono fundisho hilo na chanzo chake ni falsafa na dini za kale za kipagani.
Yesu anasema" Nanyi mtaijua kweli, nayo kweli itawaweka ninyi huru" (Yohana 8:32)
Yesu kristo alisali hivi kwa Mungu; "uzima wa milele ndio huu, waendelee kupata ujuzi juu yako wewe, Mungu wa pekee wa kweli na juu ya yule uliyemtuma,yesu kristo"
Je wafu wako wapi? Wafu wako kaburini wakingojea ufufuo (Yohana) hawateseki au kuhisi maumivu yoyote, kwa sababu "wafu hawajui lolote kamwe" (mhubiri 9:5)-(mhubiri 9:10) hata hivyo, kupitia ufufuo, Mungu atakishinda kifo milele. 1 Wakorintho 15:24,55;ufunuo 21:4
Kauli tata; ijapokuwa mwili hurudi udongoni, roho humrudia Mungu.(Mh.12:7)
Utatuzi wake; kufuatana na sulemani, katika kifo, hakuna tofauti ya roho za wanyama na za wanadamu, wote huenda pamoja (mh.3:19-21). Anachomaanisha kuwa kinamrudia Mungu ni ile cheche ya uhai (mwa.2:7)
Imani ya kuongea na wafu(spiritualism) ikiwa wafu hawana ufahamu, je wanaongea huwa na akina nani?
Imani ya kuongea na wafu imeanzia kwenye uongo wa awali wa shetani kwa Hawa."Hakika hamtakufa"(mwa.3:4) Maneno hayo yalikuwa hubiri la kwanza (linaloendelea hivi sasa) juu ya kutokufa kwa roho(nafsi)
Roho itendayo dhambi itakufa(Eze.18:20)imebadilishwa kimtizamo kuwa "roho hata ikitenda dhambi itaendelea kuishi milele"
Hivyo utamaduni wa mafundisho haya umejenga imani yenye dhana yakubatilisha ukweli nakutimiliza matakwa ya shetani. Na kila haaminiye nakutimiliza matendo yakiimani katika njia hii ujinasibu mwishoni kuwa yu mungu au mwenye nguvu juu yake mwenyewe zakuumba nakuponya kujua kabla na baada ya,kutoa na kutwaa nakujitukuza mwenyewe sawa na ahadi ya babaye shetani "mtakuwa kama miungu"(Mwa.3:5)