HIV- Nimebugi step?

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
1,195
Baada ya miaka mingi sana, nilibahatika kukutana na ex-girl friend wangu wa enzi za mwalimu na kama zali wote tukajikuta tuko single! Kukawa hakuna kipingamizi cha mimi na yeye kukumbushiana enzi ila this time ilibidi tutumie condom kwa kuwa yeye pamoja na mimi tulitoka na watu wengine wengi baada ya kupotezana. I must say baada ya game ya kwanza, hakuna aliyeridhishwa na matokeo ya mchezo na tuliwekana wazi kuhusu hilo na tuligundua sababu iliyozuia tusienjoy kama enzi zile za mwalimu ni hiyo condom, kipindi kile tulikua tunapiga mchezo kavukavu. Basi tukakubaliana kwamba tukokotane mguu kwa mguu tukapime ili kama wote tuko fresh, ngoma irudiwe kavukavu. Sikuwa na wasiwasi wala yeye hakua na woga na thanks god majibu yetu yakawa poa na tukakumbukia enzi zetu big time...tena si mara moja wala mbili....

Hii story nilimuelezea mshkaji wangu mmoja na alichosema kilinikata stimu to say the least, akasema kwamba kwa anavyojua yeye HIV inachukua at least mwezi kuwa detected kwenye damu ya mtu baada ya maambukizi. Mi nilikua najua ukipima kama uko fresh unajiachia tu. Je hii kitu ni kweli au story za kijiweni? Does it mean am at risk? Kuna kipimo chenye uwezo wa kusoma hivo vidudu baada tu ya masaa machache mtu kuambukizwa?

Happy belated World AIDS day
KKN
 

snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
17,288
2,000
umebuuuugi meeeeen!
kitu kina gross period na chenyewe oh!
ila najaribu kuimagine mlivomaliza kudo round ya kwanza mkaoga mkavaa mkatafuta usafiri mkaenda kituo cha kupima mkapima mkaambiwa NEGATIVE!huo mshangilio wake SI MCHEZO najua!
haoooooo mkarudi kukianzisha tena!HAPO NDO NGOMA ILIPONOGA!
HONGERA,JAPO ULIJALI KIASI FULANI !una moyo best!wengi wetu hapa tutakushambuliaaaaa lakini ukweli uliyofanya ni maamuzi magumu ujue!TATIZO TU,uhakika ndo sio wa kuchukulia mkopo,daaamn!
 

snowhite

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
17,288
2,000
Snowhite, zilipita siku mbili tatu kabla ya kwenda kupima na mchezo kurudiwa....
anhaaaa!bora umenisaidia kuondoa hiyo video niliyotengenza kukichwa!
ila still upo kwenye risk bana until further notice!huwezi jua pengine binti alishiriki tendo na mtu ndani ya wiki hiyo hyo na jamaa alikuwa mwathrika!au wewe mwenyewe pia ukawa umemwambukiza!
ah lakini kwanini ujiumize kwa mawazo banaaa!after all maisha sio magumu hivoooo!subiri miezi mitatu ukapime uwe na amani si ajabu muoane sasa na huyo ex si wote mmekutana bado masingle kuweni double sasa!sawa?
my take!
usifikiri nalichukulia ni jambo jepesi mi najaribu tu kukutake through so as ucalm down ndo mana naongea hivi ninavoongea.najua ni ngumu sana hasa kama anajali afya yako!lakini sasa ndo imeshatokea huna namna zaidi ya kusuburi upate majibu ya uhakika!sawa?
 

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
1,195
Incubation period ya HIV siyo miezi 6 kweli?

Duu!! kaa ni ezi 6 tutakufa wengi! Kuna mtu mwingine aliniambia ni miezi 3, sijui hata ukweli ni upi na hawa jamaa zetu wanao campaign kuhusu AIDS mbona hii kitu ya incubation haiwaigusii? Ujumbe ninaouskia kila siku ni "tumia condom, ukishindwa kapime na mwenzako"
 

Father of All

JF-Expert Member
Feb 26, 2012
4,864
2,000
Kupima bila kuacha uzinzi si jibu. Mnaweza kupima leo mkaonekana negative. Kama kesho mkiendekeza kuchangisha hapa na pale mnakuwa mnafanya ujinga sawa na kuruka mkojo ukakanya manihino. Hivyo kupima kwako si big deal kama wewe na mwenzio hamuachi mchezo wa kuruka ruka na kuchovya chovya hapa na pale. Simpo.
 

The Hunter

JF-Expert Member
Dec 25, 2010
1,049
1,500
Condom Ikitumiwa vizuri INAWEZA, kukukinga na ukimwi....
Hawakusema Itakukinga bali itaweza so hata watengeneza condom hawana uhakika..
Mwana endelea kula bia, ila kumbuka zana kila unapoenda kuzini..aka..kumalayika..!
 

Mbu

JF-Expert Member
Jan 11, 2007
12,749
2,000
Snowhite, zilipita siku mbili tatu kabla ya kwenda kupima na mchezo kurudiwa....

....worry u not bro, unless wewe au a couple of hours prior to your date mliegesha gari siko...

Mmeshapima, mmeonekana hamna 'ngoma' kubali matokeo tu.

Haijalishi kwakuwa wote mpo -ve leo ndio kesho/keshokutwa hamtoweza ambukizwa UKIMWI na 'new' partner.
 

Watu8

Platinum Member
Feb 19, 2010
60,611
2,000
there is no clear answer to your doubt...you might be infected or not....
Also, as much a I know the incubation period for HIV is approx 3 months
 

Kana-Ka-Nsungu

JF-Expert Member
Oct 4, 2007
2,257
1,195
....worry u not bro, unless wewe au a couple of hours prior to your date mliegesha gari siko...

Hapa ndipo mgogoro ulipo mkuu, mimi najiamini lakini huwezi jua yeye alipitiwa na nani siku, wiki au hata miezi michache iliyopita kabla yangu.
 

dandabo

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
303
225
Umejichanganya kichwa bure. Mmekutana baada ya miaka mingi, mkaenda kupima wote mko salama. Hiyo miezi mitatu unataka ujue kama alikua na virusi kabla hamja do sex au kama mliambukizana mlipo do?
Mlipopima vipimo vimeonyesha mko fiti, ridhika nae acha kona kona, na yeye pia ivyo ivyo
 

Kang

JF-Expert Member
Jun 24, 2008
5,288
2,000
Rafiki yako amekwambia kweli, ila usiogope sana rate ya transmission ya HIV ni ndogo sana kwa tendo la ndoa la kawaida hata kama alikuwa anao chance zako za kuupata ni ndogo sana so subiri mwezi nenda kapime.

Actual detection times zinatofautiana kuanzia wiki mbili hadi miezi sita, wastani ni siku 25, hii ni kwa sababu vipimo vingi havipimi HIV yenyewe vinapima antibodies ambazo zinatengenezwa na mwili wako kupigana HIV kitu kinachochukua muda kutengenezwa na mwili wako.

Kuna kipimo kinaitwa RNA hiki kinapima HIV yenyewe sio antibodies na kinaweza kupima ndani ya siku 9-11, so kama kuna sehemu bongo wanatoa jicho kipimo unaweza kwenda.
 

waubani

JF-Expert Member
Nov 21, 2012
542
250
mbona vipimo vya kisasa zaidi vipo, vinatoa majibu kama umeambukizwa 12hrs ago.Hivyo vya kutoa majibu ya uambukizo wa 3 month a go is the old sch
 

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,404
2,000
Duu!! kaa ni ezi 6 tutakufa wengi! Kuna mtu mwingine aliniambia ni miezi 3, sijui hata ukweli ni upi na hawa jamaa zetu wanao campaign kuhusu AIDS mbona hii kitu ya incubation haiwaigusii? Ujumbe ninaouskia kila siku ni "tumia condom, ukishindwa kapime na mwenzako"

Mazee, naona tangu urudi Bongo zali zimekuandama. Mara ukosekoswe na gari katika vivuko, ghafla umegonga bila nanga mahala pa-kukumbushia pasipo survey ya kutosha... daaah, angalia tu Mkuu; tahadhali na kwenda taratibu muhimu Bongo yetu, maana kitakachofatia hapo kwenye mlolongo wa mikasa ni kama vile - kuvunjiwa vioo kwa kuacha laptop au simu kwenye gari. Ikitoka hapo kuuziwa kiwanja feki, uzio wa nyumba kupigwa X kwa kujenga ndani ya hifadhi ya barabara au viwanda. Na mwishowe ku-report mahakamani kwa jaribio la kuwakwepa TRA!!:glasses-nerdy:

Naungana nawe kusema kuwa miezi 6 mingi aisee. Na kama ndiyo hivyo, basi ndiyo maana hili dubwasha linazidi kuangamiza watu na halitakuja isha kamwe... maana takwimu za kitaa zinasema kwa wastani njemba inatumia ndomu mara tatu tu kwa mpezi mmoja kabla ya kuanza kupiga kavukavu!! Sasa kama ndiyo hivyo, basi inabidi mtu katika observation period ugonge mara moja kwa mwezi...lol
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom