Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,365
- 23,518
Kwamba hiki kitendo kimefanyika mchana kweupee in broad daylight na mbele ya waandishi wa habari ni kielelezo cha tulipofika kama taifa.
Adolf Hitler alikuwa na henchman anayeitwa Heinrich Himmler, Idi Amin Dada alikuwa na henchman wake anayeitwa Isaac Maliyamungu na historia ya madikteta wote ni kwamba wanakuwa na mtu anayetekeleza mambo kwa niaba yao. Huyo mtu haguswi, ukimgusa ni kama umechezea sharubu za simba.Hitler mara ya mwisho kumuona ilikuwa koromije miaka km 10 iliyopita sema alikuwa kabadili jina silikumbuki vzr
Asante sana kwa kunikumbusha hawa mafia .Adolf Hitler alikuwa na henchman anayeitwa Heinrich Himmler, Idi Amin Dada alikuwa na henchman wake anayeitwa Isaac Maliyamungu na historia ya madikteta wote ni kwamba wanakuwa na mtu anayetekeleza mambo kwa niaba yao. Huyo mtu haguswi, ukimgusa ni kama umechezea sharubu za simba.
Hitler yuko Tanzania KolomijeBaada ya kuwashuhudia vijana wa Bashite wakimshughulikia aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye, nimejawa na wasi wasi mkubwa kuhusu hatma ya kijana Bernard Focus Saanane!
Kwamba hiki kitendo kimefanyika mchana kweupee in broad daylight na mbele ya waandishi wa habari ni kielelezo cha tulipofika kama taifa.
Mmhh Hitler yupi inayemuulizia wewe..??
Unafikiri hatuchangii uzi wako Mag3, tunachangia sana tu ndugu yetu, bali tunachangia kimoyomoyo tunaogopa wenyewe wasitusikie!!
Ahaaaaa....aiseee nimecheka sana hilo jina alilokua akijiita Iddy Amin Dada...SKU zote nilikuwa nikidhani jina la wazabanga Mobutu ssesseseko ndo la ajabu ajabu sana kumbe amini yupo na jina tata namna hii aisee nimecheka Sana.Wakati wake wengi walipotea katika mazingira tatanishi na kosa kubwa ni kusikika ukimsema vibaya bosi wake aliyejulikana kama His Excellency, President for Life, Field Marshal Al Hadji Doctor Idi Amin Dada, VC, DSO, MC, Lord of All the Beasts of the Earth and Fishes of the Seas and Conqueror of the British Empire in Africa in General and Uganda in Particular!
Huyu ndiye alikuwa Kanali Isaac Maliyamungu (sasa marehemu)
Wengi walipotea kwa njia hii.
Nape hapo ashukuru wanahabari tu, hata huyo aliyekuwa mlinzi wake inaonekana alijua issue yote ndio maana hakuchukua hatua yoyote boss wake alipotolewa bastola.
Jamani hebu fikirieni kama tukio hili lingefanyika gizani (usiku) na bila mashuhuda! Yawezekana sasa hizi tungekuwa tunaongea mengine tukijiuliza aliko Nape kama tunavyojiuliza alipo Ben. Sina hakika kama Nape Nnauye mwenyewe anajua alivyo na bahati kuweza kuchomoka kirahisi namna hiyo...
Nakumbuka yaliyompata Mwandishi Daud Mwangosi na msemaji wa polisi kudai Chadema walimtupia kitu na kumlipua...je kama ushahidi wa picha usingekuwepo, wana Chadema wangapi wangebambikiwa kesi ya mauaji?