Vazi la Taifa; Mfupa uliowashinda Wakongwe na sasa tunaanza kuhangaika nao tena

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mchakato wa kutafuta Vazi la Taifa ulianza mwaka 2004, ambapo kuliundwa Kamati maalumu na aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo wakati huo, Dkt. Emmanuel Nchimbi lakini Mtindo uliopatikana ulionekana haukidhi hadhi ya kuwa Vazi la Taifa.

Mchakato huo ulifufuliwa tena mwaka 2011 ambapo Desemba 22, 2011, kamati maalumu ya kutafuta vazi la Taifa ilizinduliwa rasmi na Dkt. Nchimbi, aliyekuwa Waziri mwenye dhamana wakati huo, tayari kuanza mchakato ambao ulipaswa kukamilika ndani ya siku 75. Kamati hiyo haikutakiwa kuanza upya mchakato, bali kuendeleza walipoishia waliouanza mwaka 2004.

Hata hivyo baada ya kutokea mabadiliko katika baraza la Mawaziri mwaka 2011 ambapo Dkt. Fenella Mukangara alikabidhiwa kusimamia Wizara hiyo, Kamati maalumu iliyoteuliwa kusimamia upatikanaji wa vazi hilo ilikabidhi michoro sita kutoka katika 200 iliyowasilishwa na Wasanii mbalimbali katika Wizara hiyo.

Kamati ilikabidhi Wizarani taarifa na mapendekezo kuwa Vazi la Taifa litokane na aina ya Kitambaa na siyo mshono. Na walipendekeza aina ya Vitambaa kwa Vazi hilo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo alikuwa Joseph Kusaga na Katibu ni Angela Ngowi, huku wajumbe wa kamati hiyo wakiwa ni Habib Gunze, Joyce Mhaville, Mustafa Hassanali, Makwaia Kuhenga, Ndesambuka Merinyo na Absalom Kibanda, ambaye baadaye alitangaza kujiweka kando.

Waziri Mukangara alionesha shauku ya kuona vazi hilo linapatikana haraka na kwamba lingevaliwa katika maadhimisho ya miaka 51 ya Uhuru wa Tanganyika yaliyofanyika Desemba 9, mwaka 2012 lakini wapi, jambo hilo halikufanikiwa.

Serikali kupitia Baraza la Mawaziri iliagiza kwamba jamii iachiwe huru kuchagua aina ya vazi ambalo litatokana na mageuzi ndani ya jamii yenyewe na isiwe uamuzi wa Serikali. Wizara ilitoa taarifa kwa maamuzi yaliyofikiwa na Serikali kwenye vyombo vya habari na tovuti ya Wizara ili wananchi wajadili na waamue wenyewe kuhusu Vazi la Taifa ambalo litapendekezwa.

Desemba, 2018, mchakato ulianza upya ambapo utaratibu wa ukusanyaji wa michoro, picha ya vazi au mavazi halisi kutoka kwa wabunifu kwa kila mkoa uliandaliwa kwa kuwaandikia Makatibu Tawala wa Mikoa yote, kuwapa taarifa kuhusu mchakato wa kupata Vazi la Taifa kwa kushirikiana na Maafisa Utamaduni kuhamasisha wabunifu ili waweze kuandaa, kuwasilisha michoro, picha au mavazi waliyobuni yanayoendana na asili ya mkoa husika.

Hata hivyo, mnamo Machi 2021 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ameliambia Bunge kuwa mpango huo umesitishwa kwa sasa kwa kuwa Serikali iligundua kuwa inafanya mchakato wa kupata vazi la viongozi na siyo kwa Watanzania wote.

Julai 2022, aliyekuwa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mohammed Mchengerwa aliteua Kamati nyingine Mpya kwa ajili ya kushughulikia mchakato wa kupata Vazi la Taifa chini ya uenyekiti wa Profesa Hermas Mwansoko ambaye ni Mkurugenzi mstaafu wa Idara ya Maendeleo ya Utamaduni, huku Katibu akiwa Dk Emmanuel Temu, Mkurugenzi wa Utamaduni kutoka Wizara ya Utamaduni.

Februari 03, 2023 aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi alituhakikishia kulipokea Vazi la Taifa, baada ya mchakato wa muda mrefu sasa na majadiliano ya muda mrefu sana na baada ya kukosekana maamuzi kwa muda mrefu sana. Hata hivyo Vazi hilo halikupokelewa tena.

Februari 7, 2024 na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma amesema Kamati ya Kitaifa ya kuratibu upatikanaji wa Vazi la Taifa inatarajia kuwashindanisha wabunifu wa mavazi kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ili watakaokuwa washindi kwa upande wa wanaume na wanawake mavazi yao yapendekezwe kuwa vazi la Taifa.

Je, suala hili hatimaye litafika mwisho au ndio litaishia hapo hapo kama wengine?

PIA SOMA
- Kamati zinazoundwa kufanya Mchakato wa Vazi la Taifa mbona hazimalizagi Kazi?

- Vazi la Taifa: Nchi yetu imepata fursa nyingine ya matumizi mabaya ya rasilimali
 
Baba wataifa ndo alisababisha

Akitaka kwenda kukopa au kuchonga china anavaa Kaunda suti

Akitaka kwenye kukopa au kusema lolote west (US au ulaya) ,anaulamba suti zenye kola


Changamoto

Lisu anakuambia mpaka wimbo wa taifa tuliukopa siku wakidai gharama tujipange
 
Naamini tunakosa majibu juu ya vazi la Taifa tatizo lipo vichwani kwetu,kubwa zaidi wengi hufikiria vazi la Taifa ni kuvaa rangi ya bendera ya Taifa kama lugola vile au shati nzima iwe bendera ndipo tuamini vazi la Taifa nafikiri tuchague tu vazi la kabila Moja iwe ndiyo vazi letu mfano vazi la kimasai basi ndio liwe vazi letu hata huko nje tukienda tujulikane hivyo yatosha tu au kaniki kiunoni kama wazee wa kigogo tukubaline inatosha lkn hii kujaza langi ya bendera Kila sehemu inaonekana wazi ubongo wetu umestack kabisa.
 
Rubbish serikali ! of what use vazi la taifa. watu mnahangaika na petty issues wakati nchi iko gizani. Rubbish
 
Back
Top Bottom