Baraza la habari Tanzania (MCT): Uhuru wa vyombo vya habari nchini unaimarika

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,033
Baraza la Habari Tanzania (MCT) limetoa taarifa ya tathmini ya uhuru wa vyombo vya habari nchini kati ya kipindi cha mwezi Januari hadi Juai 2022.

Taarifa hiyo imeeleza kupungua kwa kiasi kikubwa kwa matukio ya ukiukwaji wa haki za waandishi wa habari ukilinganisha na miaka iliyopita.

“Tumekuwa tukishuhudia mabadiliko kutoka kwa utawala ambao ulibana uhuru wa vyombo vya habari na wamiliki wa vyombo vya habari hadi kuvifuta mpaka utawala wenye kuanzisha mchakato wa kupitia sheria za vyombo vya habari ili kurekebisha sheria kandamizi kwa uhuru wa vyombo vya habari.

Kuthibitisha hilo, Februari 10, 2022, wakati akitoa leseni kwa magazeti manne yaliyokuwa yamefungiwa, Waziri Nape Nnauye aliweka wazi kuwa kufunguliwa kwa vyombo vya Mawio, Tanzania Daima, Mseto na MwanaHALISI yalikuwa ni maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan.” Imeeleza sehemu ya taarifa hiyo

MCT imeeleza utayari wa mawaziri kufanya maongezi na wadau wa habari kama ishara njema hasa ikilinganishwa na hali ilivyokuwa katika utawala uliopita ambapo MCT ilihangaika bila mafanikio kwa muda wa miaka mitatu kupata nafasi ya kukutana na Waziri wa Habari, Sanaa, Michezo na Utamaduni bila mafanikio wala barua kujibiwa, lakini ndani ya utawala wa Rais Samia, katika kipindi cha miezi mitatu Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI) ulikuwa umekutana na Waziri wa iliyokuwa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Waziri wa Katiba na Sheria ili kujadili mfumo wa kisheria unaoongoza vyombo vya habari na baadae walikutana pia na waziri wa sasa wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Haya ni mabadiliko makubwa na ya kuungwa mkono.

1.png
2.png
3.png

Nimeambatanisha hapa taarifa nzima ya MCT kwa ajili ya rejea na kutoa nafasi ya mjadala mpana zaidi.
 
Pamoja na mengine mengi ni dhahiri kuwa katika kipindi kifupi cha awamu ya Sita vyombo vya habari vinapumua na kufanya kazi kwa uhuru zaidi
 
View attachment 2314050View attachment 2314052View attachment 2314053

Nimeambatanisha hapa taarifa nzima ya MCT kwa ajili ya rejea na kutoa nafasi ya mjadala mpana zaidi.
Mama anaupiga mwingi sana maana Kwa miaka 6 Tanzania ilikuwa na anguko la uhuru wa vyombo vya habari mpaka Rais Samia Suluhu Hassan alipo ingia madarakani na kulidhibiti suala la kufinya/kunyima vyombo vya habari uhuru wa kutoa habari kwa jamii
Pamoja na mengine mengi ni dhahiri kuwa katika kipindi kifupi cha awamu ya Sita vyombo vya habari vinapumua na kufanya kazi kwa uhuru zaidi
 
Uhuru umeongezeka maana mnapewa bahasha na mkuu wa nchi, mtaanzaje kuponda na hicho ndo mlichokuwa mnahitaji? Acheni njaa
 
uhuru wa habari uko wapi maisha yapo juu mafuta ya gari yapo juu hakuna anaelalamika ni kusifia tu waandishi wengine mnampigia mama simu usiku wa manane mnaomba pesa
 
Uhuru umeongezeka maana mnapewa bahasha na mkuu wa nchi, mtaanzaje kuponda na hicho ndo mlichokuwa mnahitaji? Acheni njaa
Unajua maana ya hiki ulichokiandika? Au tu ubongo na mikono vimeachana njia panda ya Segera? Shirikisha ubongo kabla ya vidole kuchezea keyboard.🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom