GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 58,957
- 115,552
Kutenguliwa ni jambo moja, lakini kutenguliwa ukiwa katikati ya shughuli za nafasi uliyotenguliwa kwayo ni jambo lingine, hiki ndicho kilichomkuta aliyekuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ambaye si mara yake ya kwanza.
Taarifa ya kuondolewa kwa Nape katika wadhifa huo ilitolewa jana Jumapili Julai 21, 2024, akiwa katikati ya hotuba kwenye hafla ya utoaji tuzo za wanawake wa kidigitali zilizofanyika katika ukumbi wa Mlimani City, jijini Dar es Salaam ambako alikuwa mgeni rasmi. Shughuli hiyo ilikuwa ikirushwa mubashara na kituo cha televisheni cha TV E.
Baada ya taarifa za kuondewa kwenye wadhifa huo, mbunge huyo wa Mtama (CCM), Mkoa wa Lindi amesitisha kwa muda akaunti yake kijamii ya X (zamani Twitter). Kusitisha kwake, kumeibua mijadala ya kumsaka na kuhoji imekuwaje.
Mtandao wa X, Nape ndiyo miongoni mwa maeneo aliyokuwa akitumia kuwasilishana na kuchangia mijadala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa.
Hii ni mara ya pili kwa mwanasiasa huyo anakumbwa na utenguzi katika mazingira yanayofanana, aliwahi kuondolewa katika Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo akiwa kwenye harakati za kupokea ripoti ya kamati aliyoiunda ya kuchunguzi tukio la uvamizi wa kituo cha redio cha Clouds mwaka 2018.
Chanzo: mwananchi_official
Mama kweli Wewe balaa yaani Mtu yuko zake Shughulini huku Wewe tayari umeshamla Kichwa na Twitter kaifunga.