Umeme wakatika Unguja nzima, hitilafu iko Bara

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,828
Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) limetangaza kuwa Wananchi wa maeneo yote ya Unguja wamekosa huduma ya umeme leo Ijumaa ya December 8, 2023 kuanzia saa 4:15 asubuhi hadi sasa ambapo ZECO imesema tatizo hilo limesababishwa na hitilafu iliyotokea Tanzania Bara ambapo Wataalamu wa Shirika la Umeme (TANESCO) wanafuatilia tatizo hilo.

ZECO imesema maeneo yote ya Unguja kwa sasa yanakosa huduma ya umeme na imeomba radhi kwa usumbufu unaoendelea kujitokeza.
 
Wazanzibar mmekuwa mkilalamika kwamba mnataka Muungano uvunjike kwa sababu Tanganyika inawanyonya, kumbe umeme wote mnategemea kupata kutoka huku bara??!!!??
Anzisheni vyanzo vyenu vya umeme na mjitegemee wenyewe.
 
Majamaa yamekata umeme halafu ninakaz ya moto watu kwenye mahafali nategemewa Mimi kukamilisha shughuli Yao halafu wazee wa megawatt wamefanya Yao saiv simu yangu ya moto
 
Hii ndo manaa halisi ya Muungano

Uku kwetu mbna kawaidaa tu

au huko ninch jiran?
#Tanganyika yetu🇹🇿
 
Habari ndugu mteja asante kwa kuwasiliana nasi kupitia ukurasa huu na pole kwa changamoto, tafadhali tufahamishe changamoto yako kwa utatuzi zaidi.^OK
Sijui kwanini hii comment yenu imenichafua (Kuniuzi).

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Daaah watu mshazijua hadi ratiba zote za mgau

TANESCO jana mchana mlikata, usiku ilipoanza mvua mmekata mkatuletea mida ya asubuhi

Kufika saa 4 mmekata tena

Sa ndio nini?

Hata Ray C anayesifika kwa kiuno bila mfupa huwa hakati kama nyie
Bila ratiba unaweza shinda njaa, maana shughuli za kutatua faults kama umeme hamna ni ngumu wakati mwingine
 
Back
Top Bottom