Historia ya jina la Mwigulu Nchemba

Status
Not open for further replies.
sasa kupora mke wa mtu na kuvunja ndoa kisha kutelekeza familia halafu ukawa na kadi mbili za vyama tofauti kuna uhusiano gani na mtu kuwa msukuma au mhaya, acha kuchanganya madesa wewe

Munyanga sijui ni akili kufikiria kwa makalio ulitaka uolewe wewe mbona mnamfatilia sana Dr Slaa,kadi mbili mbona Wasira anazo mbili hamsemi,Nape anayo ya CCJ hamsemi na Sita je mbona mnakuwa na wivu wa kijinga tafuteni cha kuongea na si kila wakati CHADEMA ila Mwigulu ni Kilaza
 
Jina sahihi la huyu mwigizaji ni lipi? Mwigulu Nchemba ni jina la kisukuma na yeye ni mnyiramba au hilo ndio jina la kisanii ndo maana usanii mtupu kila sehemu... mimi namsihi arudie jina lake halisi la Lameck Mkumbo kama anataka kutumikia jamii na sio usanii huu anaotufanyia...

by mwanakidagu.
ndio maana huyu jamaa huwa ni kilaza.mwaka huo huo nimemaliza shule,nami nilipasua pepa la std 7.na kupangwa moshi tech.miaka hyo kufaulu kwenda kuld ilikuwa issue!.mimi nilisoma mugundu.ps.
 
Enzi zetu zile za Mwalimu majina kama haya yalikuwapo tele, tuliyaita majina ya "Makweta" kutokana na Jackson Makweta aliyekuwa waziri wa elimu enzi hizo.

Kulikuwa na wakristo wenye majina yote ya kiislam kama wazanzibari, nakumbuka kuna mwenyekiti wa Ukwata alikuwa anaitwa Hussein Ramadhani Ally, mimi nilisoma na Prosper Valentin (mwislamu huyu) halafu kulikuwa na wachagga kibao wenye majina ya kiiraqw.

Nafikiri kama huyo mwenye jina lake halisi hajalalamika, tuiache hii ishu kama ilivyo maana ina historia ndefu ambayo kama haijaathiri kitu hakuna sababu ya kuichokonoa.
This is fraud!
 
Wewe ndo unadhani hoja hii haina mashiko kwa sababu fikira zako zina makengeza. Yaani kuiba jina la mtu na kulifanya kuwa lako si kosa. Nyinyi ndo wazee wa kuchakachua aka magamba. Tunataka atuambie what transpired him be called Mwigulu Nchemba wakati ana majina yake halisi? CCM wizi mtupu hadi kwenye majina
Hii hoja haina mashiko.
 
Mwigulu Lameck Mkumbo Madelu Nchemba (Msukuma orijino wa Iramba-teheteheeee) aka Chief nikiwa nasoma nae Advanced Level Mazengo High School alikua ndio Mwanafunzi mkubwa kuliko wanafunzi wote. Nimeamini kweli alifisadi Elimu na anaweza kuwa Case study wa Kupora Elimu za watu. Katika jamii yetu ya Tanzania watu kama hawa wapo wengi sana na sikuzote ndio wamekua watendaji wabovu, wanaojidai na waonezi wakubwa wa watu (Mfano mdogo tu Police waliotumia vyeti vya watu ndio wanaoongoza kwa kutesa na kuua). Huyu jamaa aliyetambulishwa na kilaza mwenzake kama msuma original wa Iramba ukimsikiliza siku zote hoja anazotoa Bungeni na Hata kwenye vipindi mbariri vya kwenye TV utagundua tu hana tofauti na Lusinde.

  1. Tulipo kua Mazengo aliwahi tukanwa na RIP Mzee Shedy (aliyekua mpishi mkuu wa shule) kwa kulazimisha kubeba nyama nyigi kwenye ndoo. Aliitwa na aliyekuwa mkuu wa shule (Mgohamwenda) na kuambiwa awajali kwanza form One kwani ni wadogo na wanahitaji kukua kwa kupata chakula safi
  2. Alikua anauelewa mdogo sana-so aliamua kukesha madarasani ili kushindana na kipanga Nashoni. Lakini alishindwandwa.
  3. Tulipo kua Mlimani aliendelea kukesha na ndipo nikaprove anauelewa ndogo saana, bila ya kukesha usiku na mchana anafeli. mfano siku moja Mwalimu alifundusha na papo hapo akatoa testi, huyu jamaa mwenye majina matano akashika mkia.
  4. Kama yeye ni mchumi grade A aweke matokeo yake ya Advanced Level kwani alikua anasoma EGM. na siku zote huwa anasema yeye ni mchumi bora kuliko zitto aangalie perfomance ya mwenzake na ujibuji wa hoja kati yake na Zitto.
  5. Natabili atapotea kisiasa mapema sana kwa sababu ameiingilia siasa kwa pupa kama Lusinde std 7.
 
:target:haa haaa...MWIGURU MCHEMBA kama MULUGO....haa haaa wataumbuka! wanawatukana vichaa huku wakiwa ndani ya jumba la vioo wanategemea nini!
:target:
 
Jina sahihi la huyu mwigizaji ni lipi? Mwigulu Nchemba ni jina la kisukuma na yeye ni mnyiramba au hilo ndio jina la kisanii ndo maana usanii mtupu kila sehemu... mimi namsihi arudie jina lake halisi la Lameck Mkumbo kama anataka kutumikia jamii na sio usanii huu anaotufanyia...
ni kweli kabisa kwani jina Mwigulu Nchemba ni la kisukuma na bahati mbaya kabisa ni kwamba mh. hana jina hata moja la kiasili yake au kabila lake hususani kabisa la kinyiramba.
 
Ukweli ni kwamba kipindi cha nyuma,serikali ya akina mwigulu ilipuuza elimu,sekondari zilikua chache sana kiasi kwamba kujiunga na kidato cha kwanza ilikua ngumu sana.wengi walihitimu std7 lakini hawakuchaguliwa na si kwasababu walifeli,ila shule zilikua chache.waliojitathmini na kutoyakubali matokeo,walirudia darasa na kweli walifanya vizuri,sasa wapi ilipo dhambi ya mwigulu nchemba?angefanya nini kama sio hivyo alivyofanya?je,angeendelea kua mjinga badala ya kupambana na ujinga kadili alivyoweza?je,mtoa hoja ulitafakari haya? Sasa,tafakari!
 
Kulingana na mtoa hoja,Mwigulu hajaiba jina,ila mwenye jina aliacha shule! sasa je,Mwigulu aliibaje hapo? Kwanini mwenye jina hajajitokeza? mnaomuukumu Mwigulu ni sawa na wale waliomshtaki Lema,hawakua na haki kisheria kwani haki zao hazikuvunjwa na Lema!

Nampongeza Mwigulu kwa kuitumia nafasi iliyopatikana.Je,asingerudia tungempata wapi kijana anayejiamini kama yule leo hii ktk siasa? Au watu mnajadili vyama na si uwezo wa mtu mmojammoja?
 
ebu kila mtu achunguze ukoo wake kikweli n a atuambie kama hakuna majina haya
 
Enzi zetu zile za Mwalimu majina kama haya yalikuwapo tele, tuliyaita majina ya "Makweta" kutokana na Jackson Makweta aliyekuwa waziri wa elimu enzi hizo.

Kulikuwa na wakristo wenye majina yote ya kiislam kama wazanzibari, nakumbuka kuna mwenyekiti wa Ukwata alikuwa anaitwa Hussein Ramadhani Ally, mimi nilisoma na Prosper Valentin (mwislamu huyu) halafu kulikuwa na wachagga kibao wenye majina ya kiiraqw.

Nafikiri kama huyo mwenye jina lake halisi hajalalamika, tuiache hii ishu kama ilivyo maana ina historia ndefu ambayo kama haijaathiri kitu hakuna sababu ya kuichokonoa.

Dah mkuu umehit... Hayo ulosema are very true mtu ana jina la 'Kikristo' lakini swala 5 na the other way round. Inawezekana ni majina yao but kwa kweli kalikuwepo kamchezo ka kutumia majina ya watu. So 'faza haus' je lile jina lake? Ntaulizia kila kiongozi sasa.. Utumie jina la mtu mwingine kwa nini? Si ukomae na la kwako hata ukifeli utarudia tu.. But enzi za mwalimu it was tight to do so ndo maana watu wakaamua kuchukua majina ya watu wengine. Huu ni uongo na hatutaki viongozi waongo! Ujiite Rutashobya wakati wewe ni Katembo.. Wanaowajua wengine waseme as long as it is true na sio uzushi!! Mikwara yooote na matusi kumbe yeye ni Lameck????? Huyu msumbati vipi?
 
jamani hebu tuangalie hoja alizo toa mwigulu leo aliwa star tv,kadai kua" shibuda na zitto walipo tangaza kugombea urais waliitwa na uongozi wa chadema akiwemo mlezi ambae ni mzee mtei,na kuwaonya kwa hoja kua ni mapema mno na watakigawa chama sasa iweje mbowe amtangaze Slaa bila vikao vya chama?"hii ndio ilikua hoja ya mwigulu mi napata taharuki kwakua uongozi unaonekana kua na agenda ya siri,kwanini hawa waonywe halafu mbowe apongezwe?huoni kama anazidi kuithibiisha ile propaganda ya kua chadema ana ukaskazini mwingi na double standard.naungana na baregu na kitila mkumbo kusema kua mwkt kakosea na huku ni kukigawa chama.tuwe wakweli tunahitaji demokrasia ya kweli.
shibuda alitangaza akiwa ccm akambiwa atakufa, lini aliitwa na mtei? Kuandika ungo ndio ukweli? Au bado unashabikia majambazi na wezi wa nchi hii? (viongozi wa Ccm)
 
kAMA HOJA IMETOLEWA NA MWIGULU NA INAHUSU CHADEMA,INAHITAJI KUIFANYIA UTAFITI KABLA YA KUICHUKULIA MAAMUZI,MAANA SI RAHISI KWA MWIGULU KUISIFIA CDM KAMA ILIVYO KWA CDM KUISIFIA CCM! TANZANIA DAIMA LA LEO(3-1-2013),MBOWE AMEKANUSHA MANENO HAYO KUA ALISEMA SLAA NDIE MGOMBEA! NANI MKWELI KATI YA MBOWE NA MWIGULU? NINI KIMEMSUKUMA MWIGULU KULIZUNGUMZIA HILI WAKATI KWAO PIA WAPO WALIOTANGAZA NA WENGINE PIA WANAONYWA WASIFANYE HIVYO?

KWANINI MWIGULU ASIZUNGUMZIE HATUA WALIZOFIKIA KTK KUVUA YALE MAGAMBA MAWILI SUGU? MBONA YAMEACHWA NA KUTUNUKIWA VYEO VYA JUU!?

ILA UKWELI NI KWAMBA(KWA MAONI YANGU) CDM INATAKIWA KUJIANGALIA SANA,HAO CCM WANATAKA KUPENYEZA MAJUNGU ILI TU KUIUA CDM.ISIPOKUA MAKINI,HAKIKA ITAPOROMOKA NA KUANGUKIA PUA!

NAPE ALITULETEA HOJA YA KADI YA SLAA,BAVICHA WAKAGAWIKA, MASKINII! LEO WAMEONA ILE IMECHUJA,WANADANDIA HII YA MBOWE! NDIO,SIKU YA KUFA NGEDERE MITI YOOTE HADI MITIKI HUTEREZA!

NI KWELI KWAMBA CDM IJITAHIDI KUJITOFAUTISHA NA CCM KWA KAULI,VITENDO NA MUONEKANO! VINGINEVYO,ITAKUA TU SAW NA KINYWAJI CHA ZAMANI NDANI YA CHUPA MPYA!
 
Huo ndio uchakachuaji uliopitiliza ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) hadi upo kwenye majina ya viongozi wake ambao kiukweli hawapatikani kwa njia za kiuhalali bila kuminya walalahoi na maskini waliopitiliza ili wao waweze kutamalaki kisiasa. Watu wa aina ya Lameck Mkumbo a.k.a. Mwigulu Nchemba (Naibu katibu mkuu CCM-BARa) wapo wengi juzi tumesikia habari za aina hizi kwa Naibu Waziri wa Elimu aliyefahamika kwa majina ya Philipo Mulugo wakati ana majina yake halisi....haya ni matone mawili katika bahari.....yapo ...mengi yasiyovulika....CHUKUA HATUA...
Pengine tuulizane na tukubaliane kama hizi ndyo aina mpya UJASIRIAMALI...
Na haya yanatokea toka shule za msingi hasa pale mtu anapohitimu drs la saba kwenda Sekondari school...
NI WAULIZE KWA MTINDO HUU WA AINA YA WATAALAM HAWA.... TUTAFIKA....???????
NAWAZA KWA SAUTI PEKEE WALA SIYO MENGINEYO....
 
Hizi shutuma zina muda murefu sana, na sababu mtuhumiwa mwenyewe ni member humu bila shaka atakuwa ameziona. Tunachoshangaa ni huu ukimya wake hadi sasa, kitu kinachotufanya tuamini kuwa shutuma hizi ni za kweli.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom