Kwa kupindi hiki siwezi kusema kwa nini barabara fulani inaitwa Mwai Kibaki au Obama, ila kwa enzi hizo kuna mitaa ya:
1. Sekeou Toure (Senegal) Drive - Oysterbay
2. Patrice Lumumba (DRC) - Kariakoo
3. Kenyatta Drive (Kenya) - Oysterbay
4. Nelson Madela Road, uwanja wa Nelson Mandela
6. Mtaa wa Samora, uwanja wa Samora
7. Shule msingi Mugabe - Sinza, orodha ni ndefu
, nilibahatika kwenda Butiama, pale kijijini kuna watu wanaitwa, Jumbe, Kawawa, Mugabe, Samora, Kwame, Kambona, Kenyatta, Obote, Lumumba, Kaunda, Sekou, etc
Pia, nasikia mzee Kaunda ana mtoto anaitwa Kambarage,
Kwa wakati ule hao jamaa viongozi walikuwa ni ndg kuliko viongozi, ila kwa hali ya sasa sifahamu haya majina ya mitaa na majengo yanaitwa kwa vigezo gani, inawezekana isiwe rahisi sana kukukuta mjukuu wa Kikwete au Magufuli akiitwa jina say Muhongo, Tundu Lissu, Besigye, Zuma, Nkurunzinza, etc