Historia ya Jenerali Tumainiel Kiwelu

Historia ya Jenerali Tumainiel Kiwelu

Alitolewa nachingwea Jion akicheza mpira akaitwa Dar es salaam alipofika akaitwa Ikulu akafikia Kuapishwa bila ya kujua anakuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ!
Kwny Vita vya Kagera aliitwa Ikulu saa 7 usk akatakiwa aelekee eneo la Mapambano CDF wake Abdallah Twalipo nae tayari alikuwa eneo la Mapambano.
Sheria yake Mkipanda nae Gari Moja wote Marufuku kuzungumza na simu zenu wote lazima ku swtch off kutokumchanganya dereva.
Alielekea Vitani Mkewe akiwa na ujauzito Mkubwa akajifungua wakati Afande Tumainiel akivuka Mto kagera Mtoto akapewa jina la Kagera.
Ndie aliekuwa Msaidizi wa Bregadia Generali Hashim Mbita kupiganisha vita vya ukombozi Sourthern of sahara!
Umenichanganya kidogo haoo kuhusu kuzima simu zisimchanganye dereva. Wakati huo hatukuwa na simu. Au unazungumzia simu za upepo yaani radio call?
 
Umenichanganya kidogo haoo kuhusu kuzima simu zisimchanganye dereva. Wakati huo hatukuwa na simu. Au unazungumzia simu za upepo yaani radio call?

Hayo ni Maelezo yake Mwenyewe, Pitia Raia Mwema pia kumbuka mpaka leo yupo hai jee hamiliki simu? kasema huo ni utaratibu wake kwa nini wewe uhusishe na zamani tu kama vile baada ya zamani haishi wala hana kanuni ya maisha?
 
Hajaharibu ni fact.........Kamanda wa muda mrefu....kafanya mengi ila hajawa recognised countrywide kuja tu obama tayar kapewa na njia.....hiv kule USA kuna hata barabara ya nyerere kwa walioenda?...

Mtu kama Nandi Azikiwe wa Nigeria kapewa barabara ya Posta mpya( Azikiwe Avenue) kabisa, Mwai Kibaki wa Kenya kapewa ya Morocco sijui wanamchango gani kwa taifa hili na tumeacha kuenzi wazalendo wengi wa Taifa hili
 
Huyu bwana ni mchapa kazi kweli, kwenye mikutano yake ndio utapenda, maana yeye hakuwa na mambo ya CCM OYEEEEEEEE!!!, alikuwa anahutubia kwa Kuuliza maswali wahusika, ole wako ukose majibu. Jamaa nilikaa naye kule BKB alikuwa hana mke takribani miaka nane niliyokaa pale, alikuwa anakula rest house, alipostaafu alienda kukaa bunazi, nadhani bado yuko hapo. Kwa ufupi hayo ndio ninayoyajua juu yake.
 
Leo nimeona mahojiano yenye ya mwandishi Livingstone Ruhere na Jenerali Tumaniel Kiwelu kwenye gazeti la Raia Mwema la jana ambae anaweza kuileta hapa naomba afanye hivyo kwa faida ya wana JF na kizazi cha sasa.

Mimi nimekuwa nikimsikia huyu mtu akisifika kwa uzalendo na uchapakazi.
Alipokuwa mkuu wa mkoa Tabora akajenga uwanja wa Mpira Ali Hassan Mwinyi stadium, enzi hizo ndo ulikuwa uwanja best Tanzania..haukuisha moja ya sababu alihamishwa kabla hajaumalizia.

Na alipoenda mkoa wa Rukwa akajenga uwanja mwingine wa mpira Nelson Mandela stadium ulikuwa mzuri kuliko uwanja wa Uhuru wa Dar..

Ukitazama jinsi alivyoweza kufanya kitu ambacho viongozi wa kitaifa hadi wasubiri misaada ya nchi za nje na bajeti kuubwa ndo wanaweza fanya hata robo. Yeye ilikuwa tu 'akiamua kitu anaanza tu hadi mwisho'..

Sasa hayo ni ya miaka ya 80 kabla ya hapo ndo kuna yale ya Vita vya Uganda na mengine zaidi ya jeshini.

Kuna kitu nimekiona leo..kumbe huyu Jenerali alikuwa msomi na mkufunzi jeshini ilikuwa kidogo tu asome kile chuo maarufu England cha kijeshi Sandhurst..

Hawa wazalendo wachache sana ambao tunapaswa kuwa na mitaa yenye majina yao sio mitaa inaitwa Barrack Obama...

Mkuu uwanja wa Mirambo haukusimamiwa Lawrence Gama?
 
baada ya Nduli Amin Kutuvamia ilikuwa si kazi rahisi kumpiga adui ndani ya nchi yetu jukumu la kutoa au kuchora ramani ya mapambano na kujenga daraja lililokuwa limevunjwa na vita ikiendelea haikuwa kazi ndogo wala rahisi.ni General Kiwelu wakati huo akiwa Major General na Brigadier KITETE sasa marehemu ambae alijulikana kama Supersonic Kitete ndo walitengeneza mpango wote huo . Habari zaidi tafuta kitabu cha vita ya kagera , Kagera hadi Arua
 
Huyu bwana ni mchapa kazi kweli, kwenye mikutano yake ndio utapenda, maana yeye hakuwa na mambo ya CCM OYEEEEEEEE!!!, alikuwa anahutubia kwa Kuuliza maswali wahusika, ole wako ukose majibu. Jamaa nilikaa naye kule BKB alikuwa hana mke takribani miaka nane niliyokaa pale, alikuwa anakula rest house, alipostaafu alienda kukaa bunazi, nadhani bado yuko hapo. Kwa ufupi hayo ndio ninayoyajua juu yake.
Ana mke mkuu na watoto watatu, wawili wa kike na mmoja wa kiume...familia yake ipo dar...
 
sasa hivi viwanja vya soka huko mikoani mbona ccm wanasema ni vyao,lakini historia inasema wakuu wa mikoa ndo walivijenga kupitia nguvu ya wananchi,,,nadhani kuna haja viwanja hivi viondolewe kwenye mikono ya ccm.
 
Mi namkumbuka alipokuwa RC huku Kagera, alipambana kisawasawa na watu wavivu, aliagiza kila kijana lazima awe na shamba analolima mazao. Vilevile alipambana kisawasawa na wafanyakazi wavivu na walevi hasa walimu waliokuwa wamekubuhu kwa ulevi.
Jaman jitihada zake ndo wangukua nazo viongozi wote,hasa Marais wa wakati ule tungekua mbali.
 
Ukiambiwa story ya Mzee Ally Hassan Mwinyi kuhusu Matumizi yake ya simu leo utabisha kwa kuwa wakati anastaafu kuwa Rais wa Jamhuri simu za Mkononi zilikuwa hazijaingia nchini?
Usitumie nguvu sana, hao akina Mhe, Ally Hassan Mwinyi waliokuwa na uwezo wa kumiliki na kutumia smu za mkononi walikuwa wangapi na walikuwa wanawasliana na nani hapo Tanzania hadi waweze kumchanganya dereva ? Je, Mej. Tumaniel Kiwelu alikuwa anatumia usafiri wa umma ?
 
sasa hivi viwanja vya soka huko mikoani mbona ccm wanasema ni vyao,lakini historia inasema wakuu wa mikoa ndo walivijenga kupitia nguvu ya wananchi,,,nadhani kuna haja viwanja hivi viondolewe kwenye mikono ya ccm.
Wakati huo ulikuwa wa Chama Kushika Hatamu na chama kilichokuwa kimeshika hatamu ni ccm.
 
Sina uhakika sana km ndio aliyehusika na ujenzi wa kiwanja Tbr kwani naona km marehemu Mtazama Lawrence Gama kwa Rukwa sijui kbs
 
Hayo ni Maelezo yake Mwenyewe, Pitia Raia Mwema pia kumbuka mpaka leo yupo hai jee hamiliki simu? kasema huo ni utaratibu wake kwa nini wewe uhusishe na zamani tu kama vile baada ya zamani haishi wala hana kanuni ya maisha?
Basi wewe ndio unekosea mtiririko wako wa kuripoti, halo ulionyesha kana vile tabia hiyo alikuwa nayo akiwa safarini kwenda vitani
 
Back
Top Bottom