Historia ya Jenerali Tumainiel Kiwelu

Historia ya Jenerali Tumainiel Kiwelu

Ndo mwanzilishi wa chuo cha maafisa wa jeshi cha monduli...pia namkumbuka akiwa mkuu wa mkoa wa rukwa aliwahi mkumchapa viboko mwalim wa kike pale s/msingi LAELA viboko 8 mbele yetu wanafunzi...kiukweli czani kama kuna mkuu wa mkoa kwa sasa anayeweza kufikia level ya mzee kiwelu kiutendaji
 
Mkuu enzi za wakati wa Tunainiel Kiwelu simu za mkononi zilikuwepo? Au unamaanisha radio call?

Hiyo ni Tabia ya Afande Kihwelu sio akiwa Jeshini tu bali hata leo, Rejea Raia Mwema ya Wiki hii Ujisomee Mahojiano.Inaelezwa Historia yake kwa Jumla sio Maisha ya zamani Jeshin kabla ya Ujio wa Simu za Mkononi.
 
alikuwa mkuu wa Mkoa wa kagera mwaka, 2001-2005 aliwacharaza Nshomile viboko Kwa kujifanya wanajua sheria mpaka kumkosoa mkuu wa Mkoa, aliagiza kila Shule ya primary ipande miti
1. alimcharaza Mwalimu mkuu wa Shule muleba alipoo mkuta kilabuni muda wa Kazi
2. alipokuwa Katika Semina Shinyanga dereva wake akajipendekeza kununua mpunga Kwa kuwa alikuwa ametumwa Na rafiki zake Huko bukoba, kihwelu Alivotoka mkutanoni Akaona magunia kwenye gari akakaa kimya, alivyofika msituni biharamulo, akamuuliza dereva ule mzigo wa nan, dereva kimya, akamwambia shusha na wakauacha porin, wakenda bukoba bila kitu, lakini baadae ya wiki akamuita dereva akamrudishia hela na kumuonya asirudie,
3. kwenye miradi ya maendeleo lazima wOte mchangie ni lazima, alikuwa Hana mchezo, nashangaa kikwete alimtoa
Kikwete style yake ilikua ipo tofauti kidogo, kuna Kipindi alimchomoa Magufuli Wizara ya Ujenzi kwamba alikua hafai
 
Leo niomeona mahojiano yenye ya mwandishi Livingstone Ruhere na Jenerali Tumaniel Kiwelu
kwenye gazeti la Raia Mwema la jana
ambae anaweza kuileta hapa naomba afanye hivyo
kwa faida ya wana JF na kizazi cha sasa

Mimi nimekuwa nikimsikia huyu mtu akisifika kwa uzalendo na uchapakazi
Alipokuwa mkuu wa mkoa Tabora akajenga uwanja wa Mpira Ali Hassan Mwinyi stadium
enzi hizo ndo ulikuwa uwanja best Tanzania..haukuisha moja ya sababu alihamishwa kabla hajaumalizia

Na alipoenda mkoa wa Rukwa akajenga uwanja mwingine wa mpira Nelson Mandela stadium
ulikuwa mzuri kuliko uwanja wa Uhuru wa Dar..
ukitazama jinsi alivyoweza kufanya kitu ambacho viongozi wa kitaifa hadi wasubiri misaada ya nchi za nje na bajeti kuubwa ndo wanaweza fanya hata robo

Yeye ilikuwa tu 'akiamua kitu anaanza tu hadi mwisho'....

Sasa hayo ni ya miaka ya 80
kabla ya hapo ndo kuna yale ya Vita vya Uganda na mengine zaidi ya jeshini

kuna kitu nimekiona leo..kumbe huyu Jenerali alikuwa msomi na mkufunzi jeshini
ilikuwa kidogo tu asome kile chuo maarufu England cha kijeshi Sandhurst ..

Hawa wazalendo wachache sana ambao tunapaswa kuwa na mitaa yenye majina yao
sio mitaa inaitwa Barrack Obama......

Mkuu The Boss nikusahihishe kidogo: uwanja wa Ali Hassan Mwinyi haukujengwa na Jenerali Kihwelu bali ulijengwa kwa michango ya wananchi wa Tabora chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa marehemu Lawrence Gama. Nakumbuka nilikuwa Tabora miaka hiyo na lengo la ujenzi lilikuwa ni kuadhimisha miaka 11 ya kuzaliwa CCM sherehe ambazo kitaifa zilifanyika Tabora. Nakumbuka vizuri kwa sababu nilicheza gwaride la chipukizi kwenye sherehe zile. Jenerali Kihwelu aliteuliwa na Mkapa kuwa Mkuu wa Mkoa nadhani kuanzia mwaka 1994. Naomba kuwasilisha.
 
Mkuu The Boss

Sijalisoma hilo gazeti la Raia Mwema lakini naweza kutoa habari za General Kiwelu kama ifuatavyo.
Mambo matano usiyoyajua juu ya General Kiwelu.

1. Mwanzilishi wa TMA - Monduli wakati akianzisha chuo hakikuwa na majengo unayoyaona leo wanafunzi walilala kwenye mahema.

2. General Kiwelu ndiye aliyeandaa mipango ya vita vya Kagera (Uganda War) kwa maana ya mobilazation baada ya maandalizi alirejeshwa makao makuu ya Jeshi Chief of Staff na kumwachia General Musuguri kuongoza uwanja wa mapambano.

3. General Kiwelu ndiye General (Four Star General) pekee TPDF ambaye hakuwahi kuwa mkuu wa majeshi CDF.

4. General Kiwelu ndiye mwanajeshi pekee TPDF kuwahi kuwa Chief of Staff mara mbili.

5. General Kiwelu mara mbili alistahili kuwa CDF lakini suala la ukanda lilimgharimu.Rejea historia ya mapinduzi ya kijeshi maofisa wengi waliotoka kanda ya Kaskazini wasomi wa enzi hizo za Gen Sarakikya waliondolewa TPDF na kupelekwa kuongoza mashirika ya umma eg KAMATA,Mkonge,Fibreboard..........

6. General George Waitara alikuwa mwanafunzi wa General Kiwelu TMA Monduli baadae akaja kuwa mkuu wa majeshi huku Gen Kiwelu akiendelea kuwekwa kando.Fikiria mwanafunzi wako unamfundisha A,BC za jeshi baadae anakuja kuwa mkuu wako wa kazi na salute unamtwangia.Hii ilikuwa aibu ya siasa za wakati uleeee ambazo wakuu karibu wote wa majeshi CDF walilazimika kutoka mkoa wa Mara.Gen David Musuguri,Gen Mwita Kyaro,Gen George Waitara.
 
Nakumbuka wakati ni mkuu wa mkoa wa shinyanga na marehemu Luhanga wakati huo alikuwa mkuu wa mkoa wa mwanza,walikuwa marafiki sana, mmoja wapo akitaka kwende kumtembelea mwenzie ilikuwa wanapokea mpakanikani mwa mikoa husika
 
Mkuu The Boss nikusahihishe kidogo: uwanja wa Ali Hassan Mwinyi haukujengwa na Jenerali Kihwelu bali ulijengwa kwa michango ya wananchi wa Tabora chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa marehemu Lawrence Gama. Nakumbuka nilikuwa Tabora miaka hiyo na lengo la ujenzi lilikuwa ni kuadhimisha miaka 11 ya kuzaliwa CCM sherehe ambazo kitaifa zilifanyika Tabora. Nakumbuka vizuri kwa sababu nilicheza gwaride la chipukizi kwenye sherehe zile. Jenerali Kihwelu aliteuliwa na Mkapa kuwa Mkuu wa Mkoa nadhani kuanzia mwaka 1994. Naomba kuwasilisha.
Mwaka huo 1994 Mkapa alimteua Gen Kiwelu kuwa Mkuu wa mkoa?kwa mamlaka yapi?
 
Alishakuwa pia mkuu wa mkoa wa tanga na aliheshimika sana. Hana utani na kazi. Wachapakazi wa aina hii serikali ya awamu iliyopita haikuwahitaji. Sawa na mkuu wa mkoa wa kagera aliyetolewa wakati serikali hiyo inamalizs muda wakr. Wana Kageara watakubaliana na mimi kuwa alikuwa mchapakazi aliyeprndwa na wanakagera. Hakuwa na makuu na hakujikweza kwa ukuu wake kama tunavyoona siku hizi! Najua wenzangu mtamtaja jina.
 
jamaa angefaa kwenye uongozi huu sema umri tu umeenda, nakumbuka alivyo kua mkuu wa mkoa wa shinyanga watu walinyooka, kuingia ofisi yoyote ghafla ni kawaida kwake
 
Alitolewa nachingwea Jion akicheza mpira akaitwa Dar es salaam alipofika akaitwa Ikulu akafikia Kuapishwa bila ya kujua anakuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ!
Kwny Vita vya Kagera aliitwa Ikulu saa 7 usk akatakiwa aelekee eneo la Mapambano CDF wake Abdallah Twalipo nae tayari alikuwa eneo la Mapambano.
Sheria yake Mkipanda nae Gari Moja wote Marufuku kuzungumza na simu zenu wote lazima ku swtch off kutokumchanganya dereva.
Alielekea Vitani Mkewe akiwa na ujauzito Mkubwa akajifungua wakati Afande Tumainiel akivuka Mto kagera Mtoto akapewa jina la Kagera.
Ndie aliekuwa Msaidizi wa Bregadia Generali Hashim Mbita kupiganisha vita vya ukombozi Sourthern of sahara!
Safi mkuu....hapa nimejifunza sana..Hongera stori nzuri
 
Mkuu The Boss nikusahihishe kidogo: uwanja wa Ali Hassan Mwinyi haukujengwa na Jenerali Kihwelu bali ulijengwa kwa michango ya wananchi wa Tabora chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa marehemu Lawrence Gama. Nakumbuka nilikuwa Tabora miaka hiyo na lengo la ujenzi lilikuwa ni kuadhimisha miaka 11 ya kuzaliwa CCM sherehe ambazo kitaifa zilifanyika Tabora. Nakumbuka vizuri kwa sababu nilicheza gwaride la chipukizi kwenye sherehe zile. Jenerali Kihwelu aliteuliwa na Mkapa kuwa Mkuu wa Mkoa nadhani kuanzia mwaka 1994. Naomba kuwasilisha.
1994??? Mkapa???? Huyo
Mkapa alikuwa Rais wa nchi gani mkuu?
 
Back
Top Bottom