Historia ya Jenerali Tumainiel Kiwelu

Historia ya Jenerali Tumainiel Kiwelu

Alishakuwa pia mkuu wa mkoa wa tanga na aliheshimika sana. Hana utani na kazi. Wachapakazi wa aina hii serikali ya awamu iliyopita haikuwahitaji. Sawa na mkuu wa mkoa wa kagera aliyetolewa wakati serikali hiyo inamalizs muda wakr. Wana Kageara watakubaliana na mimi kuwa alikuwa mchapakazi aliyeprndwa na wanakagera. Hakuwa na makuu na hakujikweza kwa ukuu wake kama tunavyoona siku hizi! Najua wenzangu mtamtaja jina.
Fabian Massawe
 
Sidhani kama uwanja wa ali hassan mwinyi alisamamia gen kiwelu kama sikosei uwanja huo wa tabora alikuwa mzee Gama.

Nelson Mandela kweli kabisa ni mzee kiwelu. Na alipokuwa RC rukwa kweli alifanya kazi kubwa sana hasa kusaidia wakulima kupata soko la mahindi.

Nakumbuka alileta mpaka malori ya Jwtz kuja kuongeza nguvu ya kusombelea mahindi yaliyo kuwa vijijini na kuyatoa swanga kupaleka mpanda.
Huyu mzee ni jamii ya viongozi kama mh rais magufuli ni mtu wa kazi tu.
Sijui alipohamishiwa kupelekwa kagera lakini nilisikia alipambana sana na majambazi kwa mafanikio makubwa na alipunguza sana utekwaji wa magari yanayo ingia na kutoka kagera.

Na mtemi kweli kweli mm nilimpenda sana kwa utendaji wake wa kazi alipo kuwa rukwa.
Naomba katika hao wazalendo aongezwe Mzee Athman Kabongo aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa miaka ya 80. Mzee kwa uchapakazi alikuwa kiwango cha lami!!!
 
alikuwa anaposafiri kutoka kagera hadi dar haongei yeye ni ishara tu tena kwa kutumia coup stick.siku moja alishuka kwenye gari kwa ajili ya short call sasa aliposhuka upepo ukafunga mlango wa dereva,dereva akajua jenerali kaingia akaanza kuendesha gari kuangalia pemben mzee hayupo akarudi reverse kumchukua.jenerali hakuongea naye wiki nzima na akipigiwa saluti ni kuitikia na ishara tu
Hui ni chai isiyo na vitafunwa hii...
 
Leo nimeona mahojiano yenye ya mwandishi Livingstone Ruhere na Jenerali Tumaniel Kiwelu kwenye gazeti la Raia Mwema la jana ambae anaweza kuileta hapa naomba afanye hivyo kwa faida ya wana JF na kizazi cha sasa.

Mimi nimekuwa nikimsikia huyu mtu akisifika kwa uzalendo na uchapakazi.
Alipokuwa mkuu wa mkoa Tabora akajenga uwanja wa Mpira Ali Hassan Mwinyi stadium, enzi hizo ndo ulikuwa uwanja best Tanzania..haukuisha moja ya sababu alihamishwa kabla hajaumalizia.

Na alipoenda mkoa wa Rukwa akajenga uwanja mwingine wa mpira Nelson Mandela stadium ulikuwa mzuri kuliko uwanja wa Uhuru wa Dar..

Ukitazama jinsi alivyoweza kufanya kitu ambacho viongozi wa kitaifa hadi wasubiri misaada ya nchi za nje na bajeti kuubwa ndo wanaweza fanya hata robo. Yeye ilikuwa tu 'akiamua kitu anaanza tu hadi mwisho'..

Sasa hayo ni ya miaka ya 80 kabla ya hapo ndo kuna yale ya Vita vya Uganda na mengine zaidi ya jeshini.

Kuna kitu nimekiona leo..kumbe huyu Jenerali alikuwa msomi na mkufunzi jeshini ilikuwa kidogo tu asome kile chuo maarufu England cha kijeshi Sandhurst..

Hawa wazalendo wachache sana ambao tunapaswa kuwa na mitaa yenye majina yao sio mitaa inaitwa Barrack Obama...
Nakumbuka alikua mkuu wa mkoa wa kagera miaka ya 2003's Ule ujambazi wa pori la rusahunga n.k ulidhibitiwa vilivyo. Amani ikarejea.
 
Huyu ndio angefaa kuwa Waziri wa mambo ya ndani
 
kikwete hakupenda watu wenye akili
alikuwa mkuu wa Mkoa wa kagera mwaka, 2001-2005 aliwacharaza Nshomile viboko Kwa kujifanya wanajua sheria mpaka kumkosoa mkuu wa Mkoa, aliagiza kila Shule ya primary ipande mit.

1. Alimcharaza Mwalimu mkuu wa Shule muleba alipoo mkuta kilabuni muda wa Kazi

2. Alipokuwa Katika Semina Shinyanga dereva wake akajipendekeza kununua mpunga Kwa kuwa alikuwa ametumwa Na rafiki zake Huko bukoba, kihwelu Alivotoka mkutanoni Akaona magunia kwenye gari akakaa kimya, alivyofika msituni biharamulo, akamuuliza dereva ule mzigo wa nan, dereva kimya, akamwambia shusha na wakauacha porin, wakenda bukoba bila kitu, lakini baadae ya wiki akamuita dereva akamrudishia hela na kumuonya asirudie,

3. Kwenye miradi ya maendeleo lazima wOte mchangie ni lazima, alikuwa Hana mchezo, nashangaa Kikwete alimtoa.
 
umemaliza laela mwaka gani
Ndo mwanzilishi wa chuo cha maafisa wa jeshi cha monduli...pia namkumbuka akiwa mkuu wa mkoa wa rukwa aliwahi mkumchapa viboko mwalim wa kike pale s/msingi LAELA viboko 8 mbele yetu wanafunzi...kiukweli czani kama kuna mkuu wa mkoa kwa sasa anayeweza kufikia level ya mzee kiwelu kiutendaji
 
hizi fix ha ha ha.....
alikuwa anaposafiri kutoka kagera hadi dar haongei yeye ni ishara tu tena kwa kutumia coup stick.siku moja alishuka kwenye gari kwa ajili ya short call sasa aliposhuka upepo ukafunga mlango wa dereva,dereva akajua jenerali kaingia akaanza kuendesha gari kuangalia pemben mzee hayupo akarudi reverse kumchukua.jenerali hakuongea naye wiki nzima na akipigiwa saluti ni kuitikia na ishara tu
 
Sidhani kama uwanja wa ali hassan mwinyi alisamamia gen kiwelu kama sikosei uwanja huo wa tabora alikuwa mzee Gama.

Nelson Mandela kweli kabisa ni mzee kiwelu. Na alipokuwa RC rukwa kweli alifanya kazi kubwa sana hasa kusaidia wakulima kupata soko la mahindi.

Nakumbuka alileta mpaka malori ya Jwtz kuja kuongeza nguvu ya kusombelea mahindi yaliyo kuwa vijijini na kuyatoa swanga kupaleka mpanda.
Huyu mzee ni jamii ya viongozi kama mh rais magufuli ni mtu wa kazi tu.
Sijui alipohamishiwa kupelekwa kagera lakini nilisikia alipambana sana na majambazi kwa mafanikio makubwa na alipunguza sana utekwaji wa magari yanayo ingia na kutoka kagera.

Na mtemi kweli kweli mm nilimpenda sana kwa utendaji wake wa kazi alipo kuwa rukwa.
Hapo umeharibu, kuchanganya habari za Magufuli na mtu tunayemheshimu. Futa hiyo Magufuli

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mara tuu vita ya kagera ilipoanza.jenerali Tumainieli Kiwelu wakatihuo akiwa Brigedia Aliitwa ikulu na Amiri jeshi Mkuu Rais Nyerere. Mwalimu alimweleza kwa ufasaha sababu ya kuitwa kwake na Kisha akapewa dhamana ya kuwa War operation commander,na maramoja akatakiwa Kwenda uwanja wa mapambano. Ndio alikua Masterminder wa vita kwenye hatua za awali, na kwa kiasi kikubwa tactics zake ndo zilifanikisha kukombolewa kwa Kagera na baadae Uganda nzima.Baada ya majeshi ya Tanzania kuvuka Kagera nafasi yake ilichukuliwa na Meja jenerali David Musuguri. na yeye akarudishwa command post HQ.
 
Nadhani tulio wengi tutakuwa tunamkumbuka Kamanda Gen.Tumainiel Kiwelu.Kamanda huyu ambaye mbali na Jeshi pia amewahi kuwa Mkuu wa baadhi ya Mikoa kama vile Rukwa n.k.Akiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa hakika aliupaisha kimaendeleo Mkoa ule kwa maamuzi yake ktk kila jambo aliloamini ni Maendeleo.Nakumbuka mambo machache aliyoyafanya kati ya mengi ikiwa ni pamoja na
1.Kukamilisha ujenzi wa Jengo la ghorofa la Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na kuhamia
2.Kujenga Uwanja wa Nelson Mandela kwa kuwashirikisha wananchi wote na ni moja ya viwanja vizuri.
Akiwa Jeshini ni mmoja wa makamanda waliokuwa mstari wa mbele kumpiga Nduli Idd Amin alipoivamia Nchi yetu.Je wadau yupo wapi Kiongozi na Shujaa huyu?
 
Huyu mzee aliingia kingi kwenye mbwembwe za Jiwe sasa kilichotokea ukabidi aufyata mkia katikati ya makalio.

Kipindi Kichaa Jiwe anakuanza urais wake huyu Kiwelu alikuja kwa kasi huku asijue kwamba zile nguvu za Jiwe zilikuwa ni moto wa kibiriti maana unawakaa waaahhhhh unazima vuuuupu. Sasa Jiwe akija na zile sera zake za kufananishwa na Nyerere kwamba tangia Nyerere hakuwahi kutokea kiongozi kama yeye sasa kiongozi huyo ni Jiwe mtekaji. Huyu mzee akaingia Kingi kwamba viongozi waliopita walikuwa ni hopeless kabisa sasa Jiwe ndo Moses atakaye watoa utumwani shubaamit

Kilichomkuta lazima afyate mkia kama bibi yetu hapa FaizaFoxy kwani unamsikia tena.

Anyway hii ndio bongo aache kukurupuka najua atakuwa keshajifunza kuacha kupaparikia mtu
 
Nadhani tulio wengi tutakuwa tunamkumbuka Kamanda Gen.Tumainiel Kiwelu.Kamanda huyu ambaye mbali na Jeshi pia amewahi kuwa Mkuu wa baadhi ya Mikoa kama vile Rukwa n.k.Akiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa hakika aliupaisha kimaendeleo Mkoa ule kwa maamuzi yake ktk kila jambo aliloamini ni Maendeleo.Nakumbuka mambo machache aliyoyafanya kati ya mengi ikiwa ni pamoja na
1.Kukamilisha ujenzi wa Jengo la ghorofa la Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na kuhamia
2.Kujenga Uwanja wa Nelson Mandela kwa kuwashirikisha wananchi wote na ni moja ya viwanja vizuri.
Akiwa Jeshini ni mmoja wa makamanda waliokuwa mstari wa mbele kumpiga Nduli Idd Amin alipoivamia Nchi yetu.Je wadau yupo wapi Kiongozi na Shujaa huyu?

Hivi anaitwa Kiwelu au Kihwelu?
 
Back
Top Bottom