Nadhan yupo nyumbani kwake. Huwa anaishi maeneo ya bukoba karibu na mpaka wa tz na ug. Eidha upande wa karagwe au misenyi. Sina uhakika VIZURI. Ila yupo huko KAGERA.Nadhani tulio wengi tutakuwa tunamkumbuka Kamanda Gen.Tumainiel Kiwelu.Kamanda huyu ambaye mbali na Jeshi pia amewahi kuwa Mkuu wa baadhi ya Mikoa kama vile Rukwa n.k.Akiwa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa hakika aliupaisha kimaendeleo Mkoa ule kwa maamuzi yake ktk kila jambo aliloamini ni Maendeleo.Nakumbuka mambo machache aliyoyafanya kati ya mengi ikiwa ni pamoja na
1.Kukamilisha ujenzi wa Jengo la ghorofa la Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na kuhamia
2.Kujenga Uwanja wa Nelson Mandela kwa kuwashirikisha wananchi wote na ni moja ya viwanja vizuri.
Akiwa Jeshini ni mmoja wa makamanda waliokuwa mstari wa mbele kumpiga Nduli Idd Amin alipoivamia Nchi yetu.Je wadau yupo wapi Kiongozi na Shujaa huyu?
Huyu mzee aliingia kingi kwenye mbwembwe za Jiwe sasa kilichotokea ukabidi aufyata mkia katikati ya makalio.
Kipindi Kichaa Jiwe anakuanza urais wake huyu Kiwelu alikuja kwa kasi huku asijue kwamba zile nguvu za Jiwe zilikuwa ni moto wa kibiriti maana unawakaa waaahhhhh unazima vuuuupu. Sasa Jiwe akija na zile sera zake za kufananishwa na Nyerere kwamba tangia Nyerere hakuwahi kutokea kiongozi kama yeye sasa kiongozi huyo ni Jiwe mtekaji. Huyu mzee akaingia Kingi kwamba viongozi waliopita walikuwa ni hopeless kabisa sasa Jiwe ndo Moses atakaye watoa utumwani shubaamit
Kilichomkuta lazima afyate mkia kama bibi yetu hapa FaizaFoxy kwani unamsikia tena.
Anyway hii ndio bongo aache kukurupuka najua atakuwa keshajifunza kuacha kupaparikia mtu
Huyu Mzee alikuwa mkuu wa Mkoa wakati wa Awamu ya Kwanza msichangaye mamboAcha kudanganya. Unapamba kwa uongo fatilia history ya mzee huyu. Labda kama ni mwingine. But huyu sio kama ulivoelezea
amekuwa mkuu wa mkoa wa kagera kipindi cha mzee Mkapa, baada ya Mohamed Babu, huyu mkuu wa mkoa aliyewatandika Viboko walimu kwenye shule kadhaa huko muleba na Bukoba vijijini,Huyu Mzee alikuwa mkuu wa Mkoa wakati wa Awamu ya Kwanza msichangaye mambo
Kikwete style yake ilikua ipo tofauti kidogo, kuna Kipindi alimchomoa Magufuli Wizara ya Ujenzi kwamba alikua hafai
Leo nimeona mahojiano yenye ya mwandishi Livingstone Ruhere na Jenerali Tumaniel Kiwelu kwenye gazeti la Raia Mwema la jana ambae anaweza kuileta hapa naomba afanye hivyo kwa faida ya wana JF na kizazi cha sasa.
Mimi nimekuwa nikimsikia huyu mtu akisifika kwa uzalendo na uchapakazi.
Alipokuwa mkuu wa mkoa Tabora akajenga uwanja wa Mpira Ali Hassan Mwinyi stadium, enzi hizo ndo ulikuwa uwanja best Tanzania..haukuisha moja ya sababu alihamishwa kabla hajaumalizia.
Na alipoenda mkoa wa Rukwa akajenga uwanja mwingine wa mpira Nelson Mandela stadium ulikuwa mzuri kuliko uwanja wa Uhuru wa Dar..
Ukitazama jinsi alivyoweza kufanya kitu ambacho viongozi wa kitaifa hadi wasubiri misaada ya nchi za nje na bajeti kuubwa ndo wanaweza fanya hata robo. Yeye ilikuwa tu 'akiamua kitu anaanza tu hadi mwisho'..
Sasa hayo ni ya miaka ya 80 kabla ya hapo ndo kuna yale ya Vita vya Uganda na mengine zaidi ya jeshini.
Kuna kitu nimekiona leo..kumbe huyu Jenerali alikuwa msomi na mkufunzi jeshini ilikuwa kidogo tu asome kile chuo maarufu England cha kijeshi Sandhurst..
Hawa wazalendo wachache sana ambao tunapaswa kuwa na mitaa yenye majina yao sio mitaa inaitwa Barrack Obama...
KIHWELU❎
Chawa wa magufuli upooNinqchompenda magufuli ni kwamba kwake mambo ya kina mama na matukio yao hayawezi kimkwamisha kufaanya kazi na watu wenye uwezo
Alinifurahisha zaidi alipokuwa anafungua barabara ya mpakani na kenya alisema ikiisha hii barabara wazee wa kazi mnaweza kuwa na mke mmoja tanzania mungine huku kenya...
Actually Magufuli ni jembe...mwanaume halisi hatishiwi na vivuli vya kanga...
Magufulii...ita kanali masawe kwenye safu yako....
Hebu tusubirie wakati wa Mazishi naona watoto wake wote wa Dar na kwengineko watakuwepo maana Dodoma alikuwa na Mke wa pili na watoto wawili mmoja wa kiume yupo Jeshini na mmoja wa Kike yupo CRDB DodomaAna mke mkuu na watoto watatu, wawili wa kike na mmoja wa kiume...familia yake ipo dar...
kuna sehemu tulijikwaaaMtu kama Nandi Azikiwe wa Nigeria kapewa barabara ya Posta mpya( Azikiwe Avenue) kabisa, Mwai Kibaki wa Kenya kapewa ya Morocco sijui wanamchango gani kwa taifa hili na tumeacha kuenzi wazalendo wengi wa Taifa hili
Kwa Hilo tukio la mchele alitia doa rekodi yake.Kwanini utupe chakula?alikuwa mkuu wa Mkoa wa kagera mwaka, 2001-2005 aliwacharaza Nshomile viboko Kwa kujifanya wanajua sheria mpaka kumkosoa mkuu wa Mkoa, aliagiza kila Shule ya primary ipande mit.
1. Alimcharaza Mwalimu mkuu wa Shule muleba alipoo mkuta kilabuni muda wa Kazi
2. Alipokuwa Katika Semina Shinyanga dereva wake akajipendekeza kununua mpunga Kwa kuwa alikuwa ametumwa Na rafiki zake Huko bukoba, kihwelu Alivotoka mkutanoni Akaona magunia kwenye gari akakaa kimya, alivyofika msituni biharamulo, akamuuliza dereva ule mzigo wa nan, dereva kimya, akamwambia shusha na wakauacha porin, wakenda bukoba bila kitu, lakini baadae ya wiki akamuita dereva akamrudishia hela na kumuonya asirudie,
3. Kwenye miradi ya maendeleo lazima wOte mchangie ni lazima, alikuwa Hana mchezo, nashangaa Kikwete alimtoa.
Je,1994 Mkapa alikuwa rais?Mkuu The Boss nikusahihishe kidogo: uwanja wa Ali Hassan Mwinyi haukujengwa na Jenerali Kihwelu bali ulijengwa kwa michango ya wananchi wa Tabora chini ya uongozi wa Mkuu wa Mkoa marehemu Lawrence Gama. Nakumbuka nilikuwa Tabora miaka hiyo na lengo la ujenzi lilikuwa ni kuadhimisha miaka 11 ya kuzaliwa CCM sherehe ambazo kitaifa zilifanyika Tabora. Nakumbuka vizuri kwa sababu nilicheza gwaride la chipukizi kwenye sherehe zile. Jenerali Kihwelu aliteuliwa na Mkapa kuwa Mkuu wa Mkoa nadhani kuanzia mwaka 1994. Naomba kuwasilisha.