Historia ya Jenerali Tumainiel Kiwelu

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,281
117,176
Leo nimeona mahojiano yenye ya mwandishi Livingstone Ruhere na Jenerali Tumaniel Kiwelu kwenye gazeti la Raia Mwema la jana ambae anaweza kuileta hapa naomba afanye hivyo kwa faida ya wana JF na kizazi cha sasa.

Mimi nimekuwa nikimsikia huyu mtu akisifika kwa uzalendo na uchapakazi.
Alipokuwa mkuu wa mkoa Tabora akajenga uwanja wa Mpira Ali Hassan Mwinyi stadium, enzi hizo ndo ulikuwa uwanja best Tanzania..haukuisha moja ya sababu alihamishwa kabla hajaumalizia.

Na alipoenda mkoa wa Rukwa akajenga uwanja mwingine wa mpira Nelson Mandela stadium ulikuwa mzuri kuliko uwanja wa Uhuru wa Dar..

Ukitazama jinsi alivyoweza kufanya kitu ambacho viongozi wa kitaifa hadi wasubiri misaada ya nchi za nje na bajeti kuubwa ndo wanaweza fanya hata robo. Yeye ilikuwa tu 'akiamua kitu anaanza tu hadi mwisho'..

Sasa hayo ni ya miaka ya 80 kabla ya hapo ndo kuna yale ya Vita vya Uganda na mengine zaidi ya jeshini.

Kuna kitu nimekiona leo..kumbe huyu Jenerali alikuwa msomi na mkufunzi jeshini ilikuwa kidogo tu asome kile chuo maarufu England cha kijeshi Sandhurst..

Hawa wazalendo wachache sana ambao tunapaswa kuwa na mitaa yenye majina yao sio mitaa inaitwa Barrack Obama...
 
Sidhani kama uwanja wa ali hassan mwinyi alisamamia gen kiwelu kama sikosei uwanja huo wa tabora alikuwa mzee Gama.

Nelson Mandela kweli kabisa ni mzee kiwelu. Na alipokuwa RC rukwa kweli alifanya kazi kubwa sana hasa kusaidia wakulima kupata soko la mahindi.

Nakumbuka alileta mpaka malori ya Jwtz kuja kuongeza nguvu ya kusombelea mahindi yaliyo kuwa vijijini na kuyatoa swanga kupaleka mpanda.

Huyu mzee ni jamii ya viongozi kama mh rais magufuli ni mtu wa kazi tu.

Sijui alipohamishiwa kupelekwa kagera lakini nilisikia alipambana sana na majambazi kwa mafanikio makubwa na alipunguza sana utekwaji wa magari yanayo ingia na kutoka kagera.

Na mtemi kweli kweli mm nilimpenda sana kwa utendaji wake wa kazi alipo kuwa rukwa.
 
Alitolewa nachingwea Jion akicheza mpira akaitwa Dar es salaam alipofika akaitwa Ikulu akafikia Kuapishwa bila ya kujua anakuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ!

Kwny Vita vya Kagera aliitwa Ikulu saa 7 usk akatakiwa aelekee eneo la Mapambano CDF wake Abdallah Twalipo nae tayari alikuwa eneo la Mapambano.

Sheria yake Mkipanda nae Gari Moja wote Marufuku kuzungumza na simu zenu wote lazima ku swtch off kutokumchanganya dereva.
Alielekea Vitani Mkewe akiwa na ujauzito Mkubwa akajifungua wakati Afande Tumainiel akivuka Mto kagera Mtoto akapewa jina la Kagera.

Ndie aliekuwa Msaidizi wa Bregadia Generali Hashim Mbita kupiganisha vita vya ukombozi Sourthern of sahara!
 
Naam
Sidhani kama uwanja wa ali hassan mwinyi alisamamia gen kiwelu kama sikosei uwanja huo wa tabora alikuwa mzee gama.
Nelson mandela kweli kabisa ni mzee kiwelu.
Na alipokuwa rc rukwa kweli alifanya kazi kubwa sana hasa kusaidia wakulima kupata soko la mahindi.
Nakumbuka alileta mpaka malori ya Jwtz kuja kuongeza nguvu ya kusombelea mahindi yaliyo kuwa vijijini na kuyatoa swanga kupaleka mpanda.
Huyu mzee ni jamii ya viongozi kama mh rais magufuli ni mtu wa kazi tu.
Sijui alipohamishiwa kupelekwa kagera lakini nilisikia alipambana sana na majambazi kwa mafanikio makubwa na alipunguza sana utekwaji wa magari yanayo ingia na kutoka kagera.
Na mtemi kweli kweli mm nilimpenda sana kwa utendaji wake wa kazi alipo kuwa rukwa.
Naam nakumbuka ilikuwa ni kipindi ambacho Gama alikuwa mkuu wa Mkoa wa Tabora ndipo uwanja ulijengwa na timu ya Mirambo ilikuwa tishio
 
Alitolewa nachingwea Jion akicheza mpira akaitwa Dar es salaam alipofika akaitwa Ikulu akafikia Kuapishwa bila ya kujua anakuwa Mnadhimu Mkuu wa JWTZ!
Kwny Vita vya Kagera aliitwa Ikulu saa 7 usk akatakiwa aelekee eneo la Mapambano CDF wake Abdallah Twalipo nae tayari alikuwa eneo la Mapambano.
Sheria yake Mkipanda nae Gari Moja wote Marufuku kuzungumza na simu zenu wote lazima ku swtch off kutokumchanganya dereva.
Alielekea Vitani Mkewe akiwa na ujauzito Mkubwa akajifungua wakati Afande Tumainiel akivuka Mto kagera Mtoto akapewa jina la Kagera.
Ndie aliekuwa Msaidizi wa Bregadia Generali Hashim Mbita kupiganisha vita vya ukombozi Sourthern of sahara!
Mkuu enzi za wakati wa Tumainiel Kiwelu simu za mkononi zilikuwepo? Au unamaanisha radio call?
 
Tulikuwa tunamkabali sana shy huyu jamaa kila akija home ilikuwa full kula tu. Namkumbuka mwingine somebody banduka sema nilikuwa mtoto sana.
 
alikuwa mkuu wa Mkoa wa kagera mwaka, 2001-2005 aliwacharaza Nshomile viboko Kwa kujifanya wanajua sheria mpaka kumkosoa mkuu wa Mkoa, aliagiza kila Shule ya primary ipande mit.

1. Alimcharaza Mwalimu mkuu wa Shule muleba alipoo mkuta kilabuni muda wa Kazi

2. Alipokuwa Katika Semina Shinyanga dereva wake akajipendekeza kununua mpunga Kwa kuwa alikuwa ametumwa Na rafiki zake Huko bukoba, kihwelu Alivotoka mkutanoni Akaona magunia kwenye gari akakaa kimya, alivyofika msituni biharamulo, akamuuliza dereva ule mzigo wa nan, dereva kimya, akamwambia shusha na wakauacha porin, wakenda bukoba bila kitu, lakini baadae ya wiki akamuita dereva akamrudishia hela na kumuonya asirudie,

3. Kwenye miradi ya maendeleo lazima wOte mchangie ni lazima, alikuwa Hana mchezo, nashangaa Kikwete alimtoa.
 
Leo niomeona mahojiano yenye ya mwandishi Livingstone Ruhere na Jenerali Tumaniel Kiwelu
kwenye gazeti la Raia Mwema la jana
ambae anaweza kuileta hapa naomba afanye hivyo
kwa faida ya wana JF na kizazi cha sasa

Mimi nimekuwa nikimsikia huyu mtu akisifika kwa uzalendo na uchapakazi
Alipokuwa mkuu wa mkoa Tabora akajenga uwanja wa Mpira Ali Hassan Mwinyi stadium
enzi hizo ndo ulikuwa uwanja best Tanzania..haukuisha moja ya sababu alihamishwa kabla hajaumalizia

Na alipoenda mkoa wa Rukwa akajenga uwanja mwingine wa mpira Nelson Mandela stadium
ulikuwa mzuri kuliko uwanja wa Uhuru wa Dar..
ukitazama jinsi alivyoweza kufanya kitu ambacho viongozi wa kitaifa hadi wasubiri misaada ya nchi za nje na bajeti kuubwa ndo wanaweza fanya hata robo

Yeye ilikuwa tu 'akiamua kitu anaanza tu hadi mwisho'....

Sasa hayo ni ya miaka ya 80
kabla ya hapo ndo kuna yale ya Vita vya Uganda na mengine zaidi ya jeshini

kuna kitu nimekiona leo..kumbe huyu Jenerali alikuwa msomi na mkufunzi jeshini
ilikuwa kidogo tu asome kile chuo maarufu England cha kijeshi Sandhurst ..

Hawa wazalendo wachache sana ambao tunapaswa kuwa na mitaa yenye majina yao
sio mitaa inaitwa Barrack Obama......
Rukwa alianzisha pia misitu ya kupanda na akatenga baadhi ya maeneo kama hifadhi (karibu na Malangali). Sumbawanga kuna Kiwelu Road. Alikuwa mchapakazi asiyependa Longolongo.
 
Leo niomeona mahojiano yenye ya mwandishi Livingstone Ruhere na Jenerali Tumaniel Kiwelu
kwenye gazeti la Raia Mwema la jana
ambae anaweza kuileta hapa naomba afanye hivyo
kwa faida ya wana JF na kizazi cha sasa

Mimi nimekuwa nikimsikia huyu mtu akisifika kwa uzalendo na uchapakazi
Alipokuwa mkuu wa mkoa Tabora akajenga uwanja wa Mpira Ali Hassan Mwinyi stadium
enzi hizo ndo ulikuwa uwanja best Tanzania..haukuisha moja ya sababu alihamishwa kabla hajaumalizia

Na alipoenda mkoa wa Rukwa akajenga uwanja mwingine wa mpira Nelson Mandela stadium
ulikuwa mzuri kuliko uwanja wa Uhuru wa Dar..
ukitazama jinsi alivyoweza kufanya kitu ambacho viongozi wa kitaifa hadi wasubiri misaada ya nchi za nje na bajeti kuubwa ndo wanaweza fanya hata robo

Yeye ilikuwa tu 'akiamua kitu anaanza tu hadi mwisho'....

Sasa hayo ni ya miaka ya 80
kabla ya hapo ndo kuna yale ya Vita vya Uganda na mengine zaidi ya jeshini

kuna kitu nimekiona leo..kumbe huyu Jenerali alikuwa msomi na mkufunzi jeshini
ilikuwa kidogo tu asome kile chuo maarufu England cha kijeshi Sandhurst ..

Hawa wazalendo wachache sana ambao tunapaswa kuwa na mitaa yenye majina yao
sio mitaa inaitwa Barrack Obama......

Umeongea vzr, ila mwisho umeharibu kwa Obama.
 
Back
Top Bottom