Historia ya Jakaya Kikwete

Kasomi

JF-Expert Member
Sep 3, 2014
11,036
20,337
Leo ni siku ya kuzaliwa ya Kikwete mwana wa Msoga, tujaribu kurejea historia yake.

Jakaya Mrisho Kikwete alikuwa rais wa nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu tarehe 21 Desemba 2005 hadi tarehe 5 Novemba 2015.

HISTORIA YAKE
Amezaliwa 7 Oktoba 1950 katika kijiji cha Msoga, kata ya Lugoba, tarafa ya Msoga, jimbo la uchaguzi la Chalinze, Wilaya ya Bagamoyo, mkoa wa Pwani.

Lugha ya mama ilikuwa Kikwere.

Alizaliwa katika familia ya wanasiasa. Babu yake Mzee Mrisho Kikwete alikuwa chifu wa Wakwere. Baba yake alikuwa Mkuu wa Wilaya Pangani, Same na Tanga.

Jakaya Kikwete amesimulia hadithi ya kifamilia ya kuwa wakati mama yake alipokuwa mja mzito naye, babu alitamka kuwa ikiwa mtoto atakuwa wa kiume atampatia urithi wa cheo chake.

Masomo Na Elimu
Miaka 1958 – 1961 akasoma Shule ya Msingi Msoga, halafu 1962 – 1965 Shule ya Kati (Middle School) Lusonga, halafu Shule ya Sekondari Kibaha akiongeza A-level huko Shule ya Sekondari Tanga.
Pia alishawahi kusoma shule kama Karatu primary na Tengeru

Kuanzia mwaka 1972 alisoma uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akimaliza kwa kupata digrii yake mwaka 1978.

Akajiunga na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Jakaya aliposoma Shule ya Sekondari ya Kibaha alikuwa mwenyekiti wa wanafunzi na pia wa Vijana wa TANU. Katika Shule ya Sekondari Tanga alikuwa Kiranja Mkuu na pia kiongozi wa timu ya mpira. Katika UDS alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa halmashauri ya wanafunzi.

Kupanda ngazi katika siasa
1mwaka huu alikuwa mkulima wa Msoga. Mwaka 1988 akateuliwa kuwa mbunge na waziri msaidizi. Mwaka 1990 alichaguliwa kuwa mbunge wa Bagamoyo/Chalinze akirudishwa kila uchaguzi hadi mwaka 2000. Akawa waziri akipita katika wizara za maji na fedha.

Mwaka 1995 alijaribu kuchaguliwa kuwa mgombea wa urais upande wa CCM. Inasemekana ya kwamba Mwalimu Julius Nyerere alimwomba wakati ule kumwachia nafasi Benjamin Mkapa aliyeteuliwa na Halmashauri Kuu ya CCM. Kikwete akawa Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali zote mbili za Mkapa.

Mwaka 2005 alifaulu kuteuliwa mgombea wa CCM kwa nafasi ya rais akashinda uchaguzi wa Desemba 2005 akizoa 80% za kura zote.

Miaka kumi ya urais
Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 alitangazwa tena mshindi ingawa kwa asilimia ndogo zaidi na kwa wasiwasi kuhusu uwezekano wa matokeo kuchakachuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi aliyoiteua mwenyewe. Katiba ya nchi hairuhusu kukata rufaa dhidi ya tangazo la tume hiyo.

Katika miaka mitano iliyofuata, rais aliendelea kusafiri sana nje ya nchi, kiasi kwamba alikaa ughaibuni siku nyingi kuliko zile alizokaa nchini Tanzania.

Hali ya mwisho ya nchi ilifananishwa na mwandamizi wake John Magufuli kuwa kama "shamba la bibi", ambamo kila mtu anaweza kuchuma anavyotaka. Pia rais mpya alilalamika kwa kukuta hazina haina fedha, mbali na madeni ya kimataifa kufikia kiasi cha karibu Shilingi za Tanzania milioni 1 kwa kila mwananchi.

Heri ya kuzaliwa mzee wa Msoga
 
Degree ya uchumi miaka 6, alikuwa kilaza huyu ndio maana Magufuli alikuwa anamtukana hadharani
Mmmh kuna sehemu JPM alimtukana? Mbona mara nyingi alikuwa akimsifia na kusema bila JK asingekuwa Rais?

Pia ni JK ndiye aliyeweka jina la JPM no. 1 kati ya majina 5 ya wagombea Urais mwaka 2015, ana mchango mkubwa. Hakuna sehemu JPM alimtukana.
 
Mmmh kuna sehemu JPM alimtukana? Mbona mara nyingi alikuwa akimsifia na kusema bila JK asingekuwa Rais?

Pia ni JK ndiye aliyeweka jina la JPM no. 1 kati ya majina 5 ya wagombea Urais mwaka 2015, ana mchango mkubwa. Hakuna sehemu JPM alimtukana.
Magufuli hakuwa chaguo la Kikwete, Magufuli lilikuwa chaguo la Mkapa.

Magufuli kumtaja Kikwete ni kumpa heshima tu sababu wapo eneo moja
 
Magufuli hakuwa chaguo la Kikwete, Magufuli lilikuwa chaguo la Mkapa.

Magufuli kumtaja Kikwete ni kumpa heshima tu sababu wapo eneo moja
Kumbe! Basi nimejua leo, ila JK alikuwa na mamlaka ya kukata jina lake ila hakukata kwani alimpenda. Pia alipokuwa Rais alikuwa na uwezo wa kutompa au kumtumbua uwaziri ila hakufanya hivyo. Alichochea mno ukuaji wa JPM kisiasa.
 
Kumbe! Basi nimejua leo, ila JK alikuwa na mamlaka ya kukata jina lake ila hakukata kwani alimpenda. Pia alipokuwa Rais alikuwa na uwezo wa kutompa au kumtumbua uwaziri ila hakufanya hivyo. Alichochea mno ukuaji wa JPM kisiasa.
Yeye alikuwa anamkubali Magufuli kama kiongozi ila kuhusu kuwa rais halikuwa chaguo lake ndio maana hata kwenye kampeni yeye hakujihusisha.
 
Yeye alikuwa anamkubali Magufuli kama kiongozi ila kuhusu kuwa rais halikuwa chaguo lake ndio maana hata kwenye kampeni yeye hakujihusisha.
Ila mbona hakukata jina lake? Kwani wakati huo ndio alikuwa Rais na angeweza kufanya hivyo, hebu jibu hili swali basi!
 
Historia yake yake ya kazi gani?
Nchi imeyumba sana tangu huyu kiumbe awe rais na aliyemrithisha.
Watanzania tungekuwa wasafi mioyoni, JK ndiye rais angefaa kumwagiwa maji machafu, na viatu popote apitapo.
Sababu tunapenda mserereko, ufisadi, majungu na siasa chafu...tunamtukuza.
Huyu ndiye rais fisadi, na bomu kuliko wote..
Na anaendelea kutawala hadi sasa kwa awamu ya pili.
Bila shaka salamu hizo zimemufikia
 
Back
Top Bottom