Historia ya Israel kupiga hospitali, shule na makazi ya watu na kukanusha kisha ukweli kudhihirika

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,505
51,106
Israel imefanya mauaji ya kutisha huko Gaza kwa kulipua hospitali ya kanisa inayotoa msaada kwa wapalestina huko Gaza.

Mwanzoni aliyewahi kuwa msaidizi wa Netanyahu katika mambo ya Media akatweet kulipongeza jeshi la Israel kwa kupiga hiyo hospitali na kuua watu ambao yeye anasema ni maadui wa Israel.

Baada ya kuona backlash ya ulimwengu na kugundua kuwa hiyo incident inafanya kazi kinyume cha maslahi ya kipropaganda ya Israel, akafuta hiyo tweet, hata hivyo tayari watu walishaicapture na kuihifadhi. Tweet yenyewe ni hii hapa chini.

1697704816149.png

Ukiachilia mbali tukio hilo la mauaji ya Madakatari, manesi , na wagonjwa na raia waliokwenda kutafuta hifadhi katika hospitali hiyo, Huko Nyuma Israel imewahi kufanya mauaji katika hospitali, shule na makazi ya watu na siku zote mbinu yake imekuwa ni ileile ya kujitetea kwa ajili ya damage control.

1. Kwanza wanasema tuna ushahidi wa video kuwa roketi zilirushwa kutokea sehemu hiyo, wataleta picha za mgando kujaribu kuonyesha kuwa wana ushahidi
2. Au wakiona ushahdi umebuma watasema IDF ilionya watu waondoke maeneo hayo
3. Siku chache baadae, au miezi michace baadae hukiri na kusema well, ni sisi tuliendesha hiyo operesheni

Unaweza kuona katika video hii historia ya Israel kupiga hospitali na shule na kisha kukataa kuhusika mwanzoni, baadae ukweli ukidhihiri wanakuja na kusema ni kweli tulifanya mauaji hayo.

TAZAMA VIDEO HII HAPA CHINI:

View: https://www.youtube.com/watch?v=i9TwBqDe_I0&ab_channel=MiddleEastEye
 
Sasa kama magaidi walioua watu wao wanajificha miongoni mwa raia unataka wafanye nini na hivi tayari ni vita.

Wakati Russia anafanya hivyo nchini Ukraine mnashangilia sana kwa kusema wanajeshi wa Ukraine wanajificha miongoni mwa raia na kuunga mkono Russia lkn ikiwa kwa wapalestina ni laana kali, sasa unafiki gani huu.

Kwa sababu ya unafiki huohuo, hamtaki kabisa kuongelea matukio yaliyopelekea hivi vita kuanza kwa sababu itawatia wapalestina hatiani, sasa kwa kuwa magaidi wa kipalestina hawataki amani basi ngoja vita viumane tuone ni nani ataumia zaidi na pia ndio lugha wanayoielewa.
 
Inaelekea hujaelewa kinachozungumziwa hapa
 
Hamas Wanajificha Kanisani? Kiongozi wa Kanisa la Orthodox palestina kaongea kuhusu Uonevu WA Israel kaishi siku moja tu kwa amani siku inayofuatiwa Poisoned Tayari yupo Hospitali.

Mkuu Washukuru Sana Palestina wanachukua attention ya Hao watu, wakiwamaliza Palestina wewe ndio unafuatia.
 
Kama ni Israel kapiga ni sawa tu,hao wapalestina waliua wayahudi kwenye tamasha mbona hamkusema na kulaani badala yake mlipongezana.
Kama ni watoto na kule walikufa watoto,kama ni wanawake na kule walikufa wanawake. Unafiki tu umejaa kwenye mioyo ya wanadamu
 
Back
Top Bottom