Historia ya familia ina umuhimu unapotaka kuchagua wa ubani?

___pennie

Member
Jan 3, 2023
12
155
Kuchagua partner au wa kufanana na wewe ni uamuzi wa kibinafsi na inategemea mambo mengi, ikiwa ni pamoja na mazingira ya familia.

Ingawa kwa uwelewa wangu historia ya familia inaweza kuwa na umuhimu kwa baadhi ya watu, si lazima iwe kigezo pekee.

Mambo mengine kama vile tabia, maadili, malengo, na hisia za kibinafsi pia huchangia katika uchaguzi wa mchumba au partner wa kuishi nae au kuwa na mahusiano nae. Kwa nyie wadau, familia ina umuhimu gani ikija kwenye swala la kuchagua partner?🥰
 
Nadhani unatakiwa pia uchunguze historia ya familia ya mtu unaetaka kuanza nae safari ya maisha yako, na ni muhimu sana... kuna baadhi ya familia wanaamini sana mambo ya kishirikina yani hawawezi kufanya chochote bila kwenda kwa waganga, wakiumwa, wakitaka kuanzisha biashara au wakikutana na shida Yoyote ile kimbilio lao la kwanza ni kwa waganga... Asa kwa nature ya familia kama hiyo hamuwezi mkafanya mambo ya msingi na ya maendeleo kwasababu wengi hua wanaishia kuwa masikini... so be careful
 
Kuchagua partner au wa kufanana na wewe ni uamuzi wa kibinafsi na inategemea mambo mengi, ikiwa ni pamoja na mazingira ya familia.

Ingawa kwa uwelewa wangu historia ya familia inaweza kuwa na umuhimu kwa baadhi ya watu, si lazima iwe kigezo pekee.

Mambo mengine kama vile tabia, maadili, malengo, na hisia za kibinafsi pia huchangia katika uchaguzi wa mchumba au partner wa kuishi nae au kuwa na mahusiano nae. Kwa nyie wadau, familia ina umuhimu gani ikija kwenye swala la kuchagua
Ni jambo la muhimu zaidi kumjua mwenzio upande wake wa familia na asili yao pamoja na tamaduni zao,
Mana swala la ndoa haliangalii muonekano wa nje tu bali unachangamana/kuunganisha familia mbili tofauti zinakua kitu kimoja hivyo ni lazima tamaduni zenu zisitofautiane sana
 
Back
Top Bottom