Mtu wa Pwani
JF-Expert Member
- Dec 26, 2006
- 4,184
- 671
naam nimekisoma hiki kitabu kilichoandikwa na Dr Ghassan kwa kweli kina mengi ya kustaajabisha na ambayo yalikua hayajulikani na pia kuna migongano ya historia tuijuayo na hii
tukisomeni na kuchangia juu ya historia hii mpya kama ilivyoandikwa na mzanzibari huyu
Wewe Mwehu wa Pwani, soma kwanza hii makala na ukome kutuletea post za kifala hapa jamvini:
ZANZIBAR UTATA MTUPU
Kwa wanafiki na wenye uchu wa madaraka hili linaweza kuchukuliwa kama swali la uchochezi, swali la kutaka kuvuruga amani na utulivu wa watanzania. Wenye upeo wa kuangalia Tanzania ya miaka ijayo, hili ni swali la msingi.
Tusiangalie amani na utulivu wa leo na kesho na kusahau kwamba Tanzania itaendelea kuwepo miaka mingi inayokuja. Tunaweza kuweka pembeni maswali muhimu kwa lengo la kutaka leo hii tuishi kwa amani na utulivu huku tukijua kwamba kila lifunikwalo kwa nguvu hufumuka na kusababisha maangamizi.
Historia haiwezi kutusamehe kwa kosa letu la makusudi la kuviandalia vizazi vijavyo maangamizi ya kuchinjana na kuikimbia nchi yao kuishi uhamishoni.
Ushindi wa CCM wa pointi moja unaacha maswali mengi zaidi ya majibu. Yako matukio mengi yanayowasukuma baadhi ya watu ndani na nje ya nchi kutilia mashaka ushindi huu. Siku moja kabla ya kutangaza ushindi;
wafuasi wa CUF kwa kujua wameshinda walizunguka kituo cha kutangaza matokeo ya kutangazia kura kwenye Hoteli ya Bwawani kwa lengo la kuishinikiza Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) , iwatangaze washindi.
Hali ya hewa ilibadilika; Jeshi likaanza kujiandaa, baadhi ya sehemu zikawa zinalindwa na wanajeshi. Marais wastaafu wa Muungano Mzee Mwinyi aliingia Zanzibar kimya kimya ili kuhakikisha kosa halifanyiki la CCM kuachia madaraka. Vigogo wengine wa CCM nao
walifika Zanzibar kwa lengo lile lile.
Kilichokuwa wazi ni kwamba ushindi wa kura haukuwa na maana tena.
Muhimu ilikuwa ni kuyalinda mapinduzi matukufu ya mwaka 1964. Wazanzibari wenyewe wanasema ushindi wa kura si neno; la msingi nikupewa. Maana yake unaweza kushinda usipewe!
Pamoja na ukweli kwamba hata mimi wakati huo nilikuwa Zanzibar nikifuatilia matukio yote haya kwa karibu, sitajadili yote haya kwenye makala haya.
Siku za mbeleni baada ya vumbi kutulia na shughuli za kawaida kuendelea, baada ya kushuhudia baraza jipya la mawaziri na uteuzi mwingine nitajitosa kujadili Zanzibar, Muungano na hatima ya vyama viwili vikubwa vya CCM na CUF.
Wiki iliyopita Mheshimiwa Rais Ali Mohamed Shein, alifanya uteuzi wa baraza la wawakilishi kwa kuwachagua sita wa CCM na wawili wa CUF, kwa vyama vinavyozidiana pointi moja tu, uchaguzi huo haukuwa na uwiano hata kidogo.
Bado ni mapema; subira yavuta heri! Leo nijadili jambo la wazi kabisa ambalo hata wachambuzi na vyombo vya habari makini vimekataa kulijadili.
Nalo ni kwa nini Profesa Lipumba amepata kura nyingi kule Zanzibar zaidi ya Seif Sharif Hamad? Wakati Lipumba ana zaidi ya asilimia 60, Seif Sharif Hamad ana asilimia 49.1.
Hili ni muhimu sana kujadili maana mwishowe linaweza kutujibia swali letu la nani alishinda Zanzibar. Tunaweza kufahamu wazi ni nani alishinda na hakupewa na ni nani alishindwa akapewa.
Inawezekana kabisa kwamba watu waliompigia kura Lipumba, ambao wazi ni wale wa CUF, hawakumpigia kura Seif.
Hili linawezekana maana kura ni siri ya mtu na inafuata mapenzi yake kwa yule anayemtaka, lakini si kwa Zanzibar ambako kura ya rais wa Zanzibar ni muhimu zaidi ya kura ya Rais wa Muungano.
Inawezekana kabisa mtu akampigia Seif na asimpigie Lipumba na si kinyume chake. Kwa Wazanzibari, Zanzibar inakuja kwanza na muungano ni baadaye.
Hata hivyo, kama CUF, walimpigia kura Shein na kumtosa Seif, basi CCM ingeweza kuchukua walao kiti kimoja kule Pemba.
CUF, ilifanikiwa kujinyakulia viti zaidi ya vitatu Unguja, lakini CCM ikaambulia patupu hata kule anakozaliwa Shein mwenyewe. Hata kama mtu hukusomea sayansi ya siasa, anaweza kuona ukinzani unaojitokeza wazi wazi katika hoja hii ninaojaribu kuileta hapa.
Hoja ninayotaka kuijenga hapa ni kwamba kama kilichofanyika kule Zanzibar ni uchakachuaji, basi waliofanya hivyo ni wanafunzi wa kuchakachua na si watu makini, maana wangehakikisha wanaondoa utata huu ambao kama si leo hata kesho wenye akili timamu watasimama na kuhoji, kwanini Seif apate asilimia 49.1 na Lipumba apate zaidi ya 60 wakati wapiga kura ni wale wale wa chama cha CUF?
Haiwezekani watu wale wale wamchague mbunge wa CUF, mwakilishi wa CUF na Diwani wa CUF na kukataa kumchagua rais wa nchi wakati shauku yao kubwa ilikuwa ni kuiongoza kwa mara ya kwanza serikali ya Umoja wa kitaifa. Katika akili ya kawaida hili haliwezekani.
CUF wanajua wameshinda, lakini hawakupewa. CCM wanajua wazi kabisa kwamba CUF wameshinda lakini hawako tayari kuwapa; na si kweli kwamba CUF wameamua kunyamaza kwa vile wana imani ya kuingizwa kwenye serikali ya umoja wa kitaifa.
Na si kweli kabisa kwamba Maalim Seif, amekuwa msaliti wa CUF kwa kujua kwamba ataingizwa serikalini kuwa Makamu wa kwanza wa Rais. Kuwafikiria hivyo Maalim Seif na viongozi wenzake wa CUF ni kuwavunjia heshima na kuwakosea haki.
Hawa wameonyesha uzalendo, busara na hekima. Wameitanguliza Zanzibar badala ya kutanguliza masilahi yao binafsi. Kama CUF, wangesimama kidete kudai ushindi wao kwa nguvu; Zanzibar ingeshuhudia machafuko makubwa zaidi ya yale ya 2002.
Swali langu ni je uvumilivu huu wa Seif Sharif Hamad wa kushinda akakubali kushindwa ili kuepusha shari utaendelea hadi lini? Vizazi vijavyo vitakuwa na uvumilivu huu? Na je
kwa nini uvumilivu huu uwe wa upande mmoja kana kwamba kule Zanzibar kuna watu ambao wana haki zaidi ya wengine? Kwanini CCM isijifunze kukubali kushindwa? Kwa nini dhana nzima ya Mapinduzi Daima isiwe na maana mpya ya mapinduzi katika maisha ya kila siku ya Mzanzibari;
kufukuza umasikini, kufukuza ujinga kwa kuhakikisha kila Mzanzibari anapata elimu bora; kujenga uchumi bora na imara. Mapinduzi ya 1964 pamoja na umuhimu wake ambao unajenga historia isiyofutika umepitwa na wakati.
Kuyalazimisha mapinduzi haya katika nyakati hizi tulizomo ni kutaka kuzalisha maasi ya leo na ya vizazi vijavyo.
Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!
Harith Ghassany
info@kwaherikwaheri.com
Usambazaji wa kitabu hichi kwa mfumo wa Free Electronic Downloading unafanyika chini ya mkataba wa Creative Commons Attribution-NonCommercial-ShareAlike 3.0 ambao uko chini ya Sharia za nchi ya Marekani.
Kwa mujibu wa Mkataba na Sharia hii, mtu anayekichukuwa kitabu hichi kupitia mfumo huu ana uhuru pia wa kukigawa, kukirudufu na kukisambaza chini ya masharti yafuatayo:
Kwa maelezo zaidi, tafadhali tembelea: http://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/3.0/us/
- Kulitaja jina la mwandishi wa kitabu kwa njia isiyohalalisha matumizi binafsi ya kitabu
- Kutokitumia kwa makusudi ya kibiashara wakati kinauzwa katika mfumo wa kitabu
- Kutokubadilisha, kugeuza, au kuongeza chochote kwenye kitabu hichi
Kitabu hichi kinatolewa bure katika mfumo huu ili msomaji anufaike na baadaye naye akipendekeze kwa mwenzake ili hatimaye ujumbe wa kusimamisha amani uliomo kitabuni uwafikie walio wengi.
Hata hivyo, mwandishi wa kitabu hiki anafahamu kwamba raha hasa ya kitabu ni kuwamo mikononi mwa msomaji, maana kitabu ni miongoni mwa vitu adhimu na vikongwe kabisa katika urathi wa mwanaadamu.
Kwa hivyo, licha ya kutolewa fursa hii ya mfumo wa kukisoma bure kitabu hichi kupitia kwenye mtandao, ni matarajio ya mwandishi kuwa wako watakaopendelea wawe nacho mikononi na kukisoma kwa nafasi zao. Kwa vile walengwa wa mfumo huu wa Free Electronic Downloading ni Wazanzibari na Watanganyika wa kawaida, basi ipo haja kwa wale wenye uwezo, wakiwa ndani ama nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kutoa mchango wa kuvinunua vitabu ama kupitia mtandao wa kitabu, http://kwaherikwaheri.com au moja kwa moja kutoka http://lulu.com na kuwafikishia walimu na wanafunzi walioko kwenye skuli na vyuo vya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Skuli, vyuo, maktaba, taasisi na watu binafsi wanaweza kumuandikia moja kwa moja mwandishi kupitia mtandao wa kitabu http://kwaherikwaheri.comikiwa watahitaji kupata msaada wa wafadhili watakaojitokeza kusaidia. Wafadhili ambao hawatopenda majina yao kujulikana, wamuarifu mwandishi. Majina yao yatahifadhiwa na mwandishi anatanguliza shukrani za dhati kwa ukarimu wao.
Mwandishi pia anatanguliza ombi na shukrani maalum kwa watakaoweza kusaidia kuviwezesha vituo vya mitandao vilivyopo Tanzania Zanzibar na Tanzania Bara kutoa muda maalum wa huduma za mtandao kwa bei nafuu kwa ajili ya wale watakaopenda kukisoma, kukichukua na ama kukihifadhi kitabu hiki kwenye vyombo vyao.
Kuanzia hivi sasa, Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru! kimo machoni mwako. Fungua kurasa zake, zama na zamia kwenye bahari yake na ibuka na lulu zilizomo ndani yake.
Mnakaribishwa nyote—walio karibu na walioko mbali.
Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru!
Zanzibar na Mapinduzi ya Afrabia
Copyright 1431 Anno Hegirae / 2010 Anno Domini by Harith Ghassany
Library of Congress Cataloging-in-Publication Data
Mapinduzi ya Zanzibar, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ukweli na Mapatano, Zanzibar na Oman, Afrabia, Masomo ya Afrabia.
English translation of title:
Goodbye Colonialism, Goodbye Freedom! Zanzibar and the Afrabia Revolution
Keywords:
Zanzibar Revolution, Union of the Republic of Tanzania, Truth and Reconciliation, Zanzibar and Oman, Afrabia Studies.
Printed in the United States of America