Waarabu waliapa kurudi Zanzibar, Je yanaoendelea ni mapinduzi ya Afrabia?

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
Je mnakumbuka kitabu cha Dr. Harith Ghassany aliyeandika kitabu chake cha Kwaheri Ukoloni kwaheri Uhuru, ambacho Mzee wetu Mohamed Said(Yumo humu) alikuwa ni research assistant wa kitabu hicho. Mzee wangu Mohamed Said najua una mengi ya kuzungumzia kitabu kile ambacho kwa kiasi kikubwa kilinifahamisha mengi kuhusu mapinduzi ya Zanzibar.

Hata hivyo, mada yangu ya leo sio kuhusu mapinduzi ya Zanzibar wala Muungano maana kitabu kile kina sentensi nzuri niliyoihifadhi tangu nipate kukisoma "Muungano umeficha siri za mapinduzi" kama nitakuwa nakumbuka vyema. Mapinduzi ya Afrabia yameelezewa vizuri sana katika kitabu kile cha Daktari nguli wa falsafa (PhD)

Katika Chapter ya 18, Dr. Harith ametuwekea Mahojiano yalisajiliwa Cairo mwaka 1975 na hayakufanywa na mwandishi wa kitabu. Mahojiano yalikuwa ya Marehemu Sheikh Ali Muhsin wa mwaka 1975 ambapo
ndio kwanza alipotoka jela ni tafauti na Sheikh Ali Muhsin wa siasa za baadae za Zanzibar katika kipindi cha siasa za vyama vingi.

Ali Muhsin alikuwa waziri wa mambo ya nje ya Zanzibar kabla ya mapinzudi, ambapo baadae alishikiliwa jela Tanganyika kabla ya kuachiwa mwaka 1974.

Katika mahojiano hayo, zaidi ya mara moja Ali Muhsin amezungumza zaidi ya mara moja kuwa "Inna aaidun! Tutarudi" Soma uk 239 & 241
Screenshot 2023-06-21 at 15-45-47 kwaheri-ukoloni-kwaheri-uhuru.pdf.png

Screenshot 2023-06-21 at 15-46-28 kwaheri-ukoloni-kwaheri-uhuru.pdf.png

Sijui kuhusu harakati za Afrabia zimefikia wapi, kwa wasiojua, Afrabia ni muungano wa Africa na Arabia, ambao kwenye kitabu wameandika

"Kwa ajili ya Wazanzibari na Watanganyika kwa ujumla wao ili kitabu hichi
kiwawezeshe kuzibadilisha nafsi zao. Waweze kuona fursa za mapenzi na neema zilizopo kwao wao na kwa ndugu na majirani zao wa jadi, na kisha wafanye kazi kwa pamoja katika kujenga Muungano Mpya na uhusiano mkongwe baina ya Waafrika na Waarabu—Afrabia—utakaosimama juu ya ukweli na hivyo kuimaliza kabisa mitikisiko na misukosuko ya muda mrefu." Uk Viii
Screenshot 2023-06-21 at 15-48-53 kwaheri-ukoloni-kwaheri-uhuru.pdf.png

Je, yanayoendelea ni harakati za mapinduzi ya Afrabia?

Sign OLS
 
Hata Joseph Goebbels mwaka 1945 baada ya Ujerumani kutandikwa kisawasawa na warusi alisema kwamba ufashisti utarudi Ujerumani. Sasa inakaribia miaka 100 na wajerumani hawataki kabisa kusikia kitu kinaitwa siasa za kimapinduzi. Ukweli mchungu ni kwamba utawala wa kisultani wa Zanzibar ulikuwa umejaa nuksi ya damu, utumwa na ubaguzi, vitu ambavyo mbele ya Mungu ni laana kubwa.
 
"Utamaduni wa undugu kati ya waarabu na waafrika"

ina maana waafrika na waarabu ni ndugu wa muda mrefu!!?ina maana Biashara ya watumwa KIHISTORIA waarabu wamesingiziwa!!?

ufafanuzi tafadhali ndugu zangu!!!
 
Hata Joseph Goebbels mwaka 1945 baada ya Ujerumani kutandikwa kisawasawa na warusi alisema kwamba ufashisti utarudi Ujerumani. Sasa inakaribia miaka 100 na wajerumani hawataki kabisa kusikia kitu kinaitwa siasa za kimapinduzi. Ukweli mchungu ni kwamba utawala wa kisultani wa Zanzibar ulikuwa umejaa nuksi ya damu, utumwa na ubaguzi, vitu ambavyo mbele ya Mungu ni laana kubwa.
Unaweza kutaja jina la sultan WA mwisho wa Zanzibar?
 
Hata Joseph Goebbels mwaka 1945 baada ya Ujerumani kutandikwa kisawasawa na warusi alisema kwamba ufashisti utarudi Ujerumani. Sasa inakaribia miaka 100 na wajerumani hawataki kabisa kusikia kitu kinaitwa siasa za kimapinduzi. Ukweli mchungu ni kwamba utawala wa kisultani wa Zanzibar ulikuwa umejaa nuksi ya damu, utumwa na ubaguzi, vitu ambavyo mbele ya Mungu ni laana kubwa.

watanganyika bana, munatesa sana na Zanzibar
 
Back
Top Bottom